Tundu Lissu afutiwa Mashitaka Mawili

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amefutiwa mashtaka mawili na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kushindwa kukidhi matakwa ya kisheria.

Lissu alipandishwa jana na kusomewa mashtaka ya uchochezi, huku akiunganishwa na wenzake watatu.

Mashtaka yaliyofutwa ni la kwanza na la tatu, kwa kile kilichodaiwa kuwa yalipaswa kuambatana na hati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi wa
Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba baada ya kupitia hoja za upande wa mashtaka na utetezi.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwisho wa siku yanaweza yakafutwa yote. Hakuna lenye msingi, labda serikali iamue tu "kushinda" kesi hiyo kama ile ya mita 200 mwaka jana.
 
Huyu Lissu ni mwanasiasa pili ni mwanasheria anachoongea anakijua maana siasa ndio kazi yake na sheria ndiyo iko hapo anaifahamu,sasa sisi tusubiri matokeo maana hata Mrema alikuwa na kesi nyingi na zote alishinda,mimi sishangai wala kushtuka maana Mahakama ndiko sheria zinapata tafasiri sahihi polisi wao ni kulinda usalama wa raia,ndio maana kesi nyingi zinatoka polisi na kuishia mahakamani tunaambulia kusema Hakimu kapindisha kumbe ni elimu zetu ndogo
 
Polisi nawashauri muwe mnaomba sponsor za kujiendeleza masomo ya ziada, kama Law Enforcement na mengineyo.
Bila hivyo mtaendelea kudhalilishwa na wanasiasa na kuishia kuchekwa mtaani hadi kwenye familia zenu.
 
Tanzania hakuna mtu ambae anaweza kufafanua vizuri kifungu by kifungu na ukaweza kumuelewa vizuri kwenye upande wa sheria ka Dr asha rose migiro na tundulissu tu tuweke pembeni mapenzi ya vyama pembeni wengine wanajiuma uma mpaka kuawelewa kunachukua mda
 
Kuna mpuuzi mmoja alisema ninkazima Lissu afungwe kwa sababu wanasheria wa serikali si wajinga.

Habari hii inadhihirisha wanasheria wa serikali ni wajinga.
Wanasheria wengi wa serikali naona hawako competent na huwa hawajishughulishi sana kama walivyo wanasheria wa kujitegemea.
 
Back
Top Bottom