Tundu Lissu afanyiwa upasuaji wa 18

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,497
pic+lissu.jpg

Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amefanyiwa upasuaji wa 18.

Upasuaji huo ulifanyika jana katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako Lissu anaendelea na matibabu tangu Septemba 7, baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa katika makazi yake, area D mjini Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi jana kwa simu, kaka yake Lissu, Alute Mughwai alisema, “Lissu leo (jana) amefanyiwa upasuaji ambao ulianza asubuhi na umemalizika salama. Nimeambiwa muda mfupi uliopita (ilikuwa saa 9.32 alasiri wakati akizungumza na Mwananchi) kuwa ameshatoka chumba cha upasuaji.”

Alute alisema, “Nimeambiwa upasuaji ulikwenda vizuri na sasa atapaswa kupumzika kama siku nne kisha ataendelea na mazoezi kama kawaida.”

Ingawa Alute hakueleza huo ni upasuaji wa ngapi, Oktoba 17 mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari alisema Lissu alikuwa amefanyiwa upasuaji mara 17 hivyo kama hakufanyiwa mwingine huo wa jana utakuwa ni wa 18.

“Lissu mpaka sasa amefanyiwa upasuaji mkubwa mara 17, ameongezewa damu nyingi kuliko mgonjwa yeyote aliyewahi kutibiwa hospitali hiyo ya Nairobi kwa miaka 20 iliyopita,” alisema Mbowe siku hiyo.

Alute alisema mpaka sasa bado hawajaanza mipango ya kushughulikia matibabu ya awamu ya tatu ambayo yalielezwa na Mbowe kuwa yatafanyikiwa nje ya Kenya.

“Nilisema nitazungumza na waandishi, lakini sijafanya hivyo kwani hakuna taarifa zaidi ya hizi na utaratibu wa matibabu ya awamu ya tatu bado hayajaanza ndio maana niko kimya,” alisema Alute.

Chanzo: Mwananchi
 
Naona Chadema baada ya kupiga hela mzigo umeachiwa familia sasa.Tuliambiwa msemaji wa afya ya Lissu hatakuwa mwingine bali Mbowe sasa naona familia imeingilia kati au imetekelezwa na maharamia ya chadema !

UGUA POLE LISSU ILA TAMBUA CDM IMEKUTUMIA TU KAMA CHOMBO CHA KAMPENI ZA KISIASA NA SASA UMEBAKI NA FAMILIA YAKO....WAPIGA SELFIE WOTE WAMEONDOKA NA SASA WATAENDA KUPIGA SELFIE NA DR SHIKA.
 
dawa ya hoja ni kuzijibu; kujaribu kumwondoa muibua hoja hiyo haijawahii kuwa achievement.
 
Naona Chadema baada ya kupiga hela mzigo umeachiwa familia sasa.Tuliambiwa msemaji wa afya ya Lissu hatakuwa mwingine bali Mbowe sasa naona familia imeingilia kati au imetekelezwa na maharamia ya chadema !

UGUA POLE LISSU ILA TAMBUA CDM IMEKUTUMIA TU KAMA CHOMBO CHA KAMPENI ZA KISIASA NA SASA UMEBAKI NA FAMILIA YAKO....WAPIGA SELFIE WOTE WAMEONDOKA NA SASA WATAENDA KUPIGA SELFIE NA DR SHIKA.
Walaaniwe wote waliohusika kumshambulia Lissu hata akiwa nani unayemjua.
 
Naona Chadema baada ya kupiga hela mzigo umeachiwa familia sasa.Tuliambiwa msemaji wa afya ya Lissu hatakuwa mwingine bali Mbowe sasa naona familia imeingilia kati au imetekelezwa na maharamia ya chadema !

UGUA POLE LISSU ILA TAMBUA CDM IMEKUTUMIA TU KAMA CHOMBO CHA KAMPENI ZA KISIASA NA SASA UMEBAKI NA FAMILIA YAKO....WAPIGA SELFIE WOTE WAMEONDOKA NA SASA WATAENDA KUPIGA SELFIE NA DR SHIKA.
IMG-20171116-WA0014.jpg
 
Siyo kosa lako ni laana za marehem mnaowapiga rambirambi zao.
 
Mungu amponye .Ila katika kitu ninachosikitika ni wabunge wa CCM kweli mbunge mwenzao anaumwa hata kwenda kumpa pole wamekatazwa.Nilikuwa na mwona Magu "MKRISTO"mzuri ila kwa hili nimeshangaa sana sana .Nimemwomba Mungu na kumshukuru ila sijaupatia picha utawala huu.

Tumelelewa kwa misingi ya "KUSAMEHE" kupendana na kuheshimiana ili tupate amani na baraka mioyoni mwetu.Sikutegemea kwa miaka niliyo nayo nikione hiki kitu Tanzania.Sijaweza kuamini kabisa kuwa tunaishi kama tunavyoishi sasa.Ila Neno moja tu TUSHUKURU KWA KILA JAMBO.MUNGU NIWAMINIFU .Zaburi ya 41
 
Back
Top Bottom