Tundu Lissu afanyiwa upasuaji wa 18

..pasuapasua zimekua nyingi sana...sasa sijui ni reconstructive surgery kwa makosa ya huko nyuma ama ni new surgery??... Anyways...lissu anatakiwa apelekwe nje ulaya au marekani kwenye proper expertise na physiotherapy....
 
Lissu utapona na kurudi katika hali yako njema kwa jina kuu lipitalo majina yote - kwa jina la YESU KRISTO Mwana wa Mungu aliye hai
 
Mungu amponye .Ila katika kitu ninachosikitika ni wabunge wa CCM kweli mbunge mwenzao anaumwa hata kwenda kumpa pole wamekatazwa.Nilikuwa na mwona Magu "MKRISTO"mzuri ila kwa hili nimeshangaa sana sana .Nimemwomba Mungu na kumshukuru ila sijaupatia picha utawala huu.

Tumelelewa kwa misingi ya "KUSAMEHE" kupendana na kuheshimiana ili tupate amani na baraka mioyoni mwetu.Sikutegemea kwa miaka niliyo nayo nikione hiki kitu Tanzania.Sijaweza kuamini kabisa kuwa tunaishi kama tunavyoishi sasa.Ila Neno moja tu TUSHUKURU KWA KILA JAMBO.MUNGU NIWAMINIFU .Zaburi ya 41
Sio wote wanaovaa makoti meupe ni madaktari, wengine ni wauza bucha tu mkuu...
 
Mungu ana makusudi na huyu Mtumishi wake mwaminifu.
View attachment 632159
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amefanyiwa upasuaji wa 18.

Upasuaji huo ulifanyika jana katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako Lissu anaendelea na matibabu tangu Septemba 7, baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa katika makazi yake, area D mjini Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi jana kwa simu, kaka yake Lissu, Alute Mughwai alisema, “Lissu leo (jana) amefanyiwa upasuaji ambao ulianza asubuhi na umemalizika salama. Nimeambiwa muda mfupi uliopita (ilikuwa saa 9.32 alasiri wakati akizungumza na Mwananchi) kuwa ameshatoka chumba cha upasuaji.”

Alute alisema, “Nimeambiwa upasuaji ulikwenda vizuri na sasa atapaswa kupumzika kama siku nne kisha ataendelea na mazoezi kama kawaida.”

Ingawa Alute hakueleza huo ni upasuaji wa ngapi, Oktoba 17 mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari alisema Lissu alikuwa amefanyiwa upasuaji mara 17 hivyo kama hakufanyiwa mwingine huo wa jana utakuwa ni wa 18.

“Lissu mpaka sasa amefanyiwa upasuaji mkubwa mara 17, ameongezewa damu nyingi kuliko mgonjwa yeyote aliyewahi kutibiwa hospitali hiyo ya Nairobi kwa miaka 20 iliyopita,” alisema Mbowe siku hiyo.

Alute alisema mpaka sasa bado hawajaanza mipango ya kushughulikia matibabu ya awamu ya tatu ambayo yalielezwa na Mbowe kuwa yatafanyikiwa nje ya Kenya.

“Nilisema nitazungumza na waandishi, lakini sijafanya hivyo kwani hakuna taarifa zaidi ya hizi na utaratibu wa matibabu ya awamu ya tatu bado hayajaanza ndio maana niko kimya,” alisema Alute.

Chanzo: Mwananchi
 
Naona Chadema baada ya kupiga hela mzigo umeachiwa familia sasa.Tuliambiwa msemaji wa afya ya Lissu hatakuwa mwingine bali Mbowe sasa naona familia imeingilia kati au imetekelezwa na maharamia ya chadema !

UGUA POLE LISSU ILA TAMBUA CDM IMEKUTUMIA TU KAMA CHOMBO CHA KAMPENI ZA KISIASA NA SASA UMEBAKI NA FAMILIA YAKO....WAPIGA SELFIE WOTE WAMEONDOKA NA SASA WATAENDA KUPIGA SELFIE NA DR SHIKA.
Think twice my friend
 
Pole sana Tundu Lissu. Sijui waliofanya hivi kama wanapata usingizi. Na kama wanapata usingizi basi tuwaombee Mola awasamehe kwa maana wao sio binadamu wa kawaida.
 
Naona Chadema baada ya kupiga hela mzigo umeachiwa familia sasa.Tuliambiwa msemaji wa afya ya Lissu hatakuwa mwingine bali Mbowe sasa naona familia imeingilia kati au imetekelezwa na maharamia ya chadema !

UGUA POLE LISSU ILA TAMBUA CDM IMEKUTUMIA TU KAMA CHOMBO CHA KAMPENI ZA KISIASA NA SASA UMEBAKI NA FAMILIA YAKO....WAPIGA SELFIE WOTE WAMEONDOKA NA SASA WATAENDA KUPIGA SELFIE NA DR SHIKA.
teh teh aisee wao bora mtu ana umashuhuri hata wa kijinga kama mange kimambi..dr shika jiandae cdm wanakuja..
 
Naona Chadema baada ya kupiga hela mzigo umeachiwa familia sasa.Tuliambiwa msemaji wa afya ya Lissu hatakuwa mwingine bali Mbowe sasa naona familia imeingilia kati au imetekelezwa na maharamia ya chadema !

UGUA POLE LISSU ILA TAMBUA CDM IMEKUTUMIA TU KAMA CHOMBO CHA KAMPENI ZA KISIASA NA SASA UMEBAKI NA FAMILIA YAKO....WAPIGA SELFIE WOTE WAMEONDOKA NA SASA WATAENDA KUPIGA SELFIE NA DR SHIKA.
Mbona uandishi wako ni wa kinafiki unajaribu kuwavuruga wahusika baada ya pyupyu kushindwa na unazungumzia upuuzi wa selfie ukichanganya na pole ya kinafiki wakati haukuwahi kuchangia hata sentimoja.
 
Dah.....
Ataweka rekodi ya mgonjwa aliyepasuliwa Mara nyingi zaidi kwenye hiyo hospitali.........
Aliyeongezwa damu nyingi zaidi kwenye hiyo hospital .....
Aliyelipa gharama kubwa zaidi tokea hospitali ianzishwe
Mtetezi wa wanyonge
 
Ninapo sikia lissu kafanyiwa upasuaji huwa naugua kabisa

Get well soon TL
 
Ujuaji mwingi wakati mwingine si mzuri
Kwanin kila kitu uwe wew tu!?
Wakati mwingine hata kwenye maisha ya kawaida si busara kutafuta sifa na kujifanya mjuaji kwa kila jambo.
Hii inatufunza hata kwenye jamii ukijifanya mjuaji sana lazima watu wakuoneshe kuwa dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Get well lissu.
 
Back
Top Bottom