Tundu Lissu ametaka madaraka ya Rais yadhibitiwe

kishumbaz

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
904
1,243
kuna mjadala KTN wa demokrasia Afrika, namuona Raisi wetu Tundu lissu live.

=====

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu ameshauri kuangaliwa upya kwa madaraka ya Rais wa Tanzania ili yadhibitiwe kwa kutoa nguvu kwa taasisi za uamuzi.

Akizungumza leo Jumapili Januari 27, 2019 wakati akihojiwa katika kipindi cha Demokrasia Afrika cha kituo cha televisheni ya KTN ya Kenya, Lissu ambaye bado yuko nchini Ubeligiji alikokwenda kutibiwa, amesema madaraka makubwa aliyonayo Rais yamevuruga mfumo wa chaguzi.

“Kwa utaratibu uliojengwa katika nchi za Afrika, wateule wake wanakuwa wateule wa Rais, kwa sababu ni wateule wa Rais wanawajibika kwa Rais, hawawajibiki bungeni na kwa wananchi wanaowaongoza. Lazima tutengeneze taasisi ambazo zinakubalika,” amesema Lissu.

Ameongeza, “Rais asiwe na mamlaka peke yake ya kuteua wajumbe wa tume, asiwe na mamlaka ya kuteua majaji wa mahakama zetu na watu wote wanaosimamia mamlaka na wanawajibika kwa Rais.”

Lissu ametoa mfano wa Katiba ya Kenya, amesema Rais wa sasa wa Kenya hawezi kuwa na mamlaka aliyokuwa nayo Jomo Kenyatta au Rais Daniel Moi. Lazima tuwe na taasisi zinazodhibiti mamlaka ya Rais.

Akizungumzia madaraka hayo katika mchakato wa uchaguzi, Lissu amesema wajumbe wote wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na wajumbe la Katiba waliteuliwa na Rais.

“Ukiacha watu wachache wasiokuwa wana CCM waliokuwa katika lile Bunge (Bunge la Katiba), asilimia 75 ya wajumbe walikuwa wa CCM, ukijumlisha na wabunge wa CCM. lile bunge lilikuwa la CCM

“Hoja yangu kwamba mamlaka ya Rais yadhibitiwe na taasisi zinazowajibika moja kwa moja kwa wananchi mfano wake mzuri kabisa ni kukwama kwa mchakato wa Katiba ya Tanzania,” alisema Lissu.

Katika mahojiano hayo alikuwepo pia Seneta wa Kilifi nchini Kenya, Stewart Madzayo ambaye naye alisisitiza umuhimu wa tume za uchaguzi kukubalika kwa wananchi alipokuwa akijadili uchaguzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

“Tukienda kwenye kura, tume lazima ziwe Wakenya wote wamekubaliana kwamba huyu na huyu ni sawa wasimamie. Kwa sababu tume ni kitu muhimu inaweza kufanya watu wamwage damu. Tume ni kitu muhimu ikiwa hapa, ikiwa Congo ikiwa na Tanzania,” alisema Madzayo.

Chanzo:Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
 
Back
Top Bottom