Tundu Lissu adai Hayati Magufuli ndiye aliyeagiza shambulio la kupigwa risasi dhidi yake Dodoma

Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 Lissu amesema aliyetoa mari, masaa mawili kabla hajapigwa risasi alisema kulikua na mtu anahutubia na kwenye hotuba yake alikuwa anapokea ripoti ya Bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite, moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba hiyo ni;

"Wale wanaopinga nchi wakati tupo kwenye vita ya kiuchumi nyie wanajeshi mnajua huwa wanafanywaje, hawastahili kuishi."

Ambapo masaa mawili baadae Lissu alishambuliwa Dodoma, akisema bayana kuwa anayemuongelea ni Hayati John Pombe Magufuli, ambapo hata baada ya tukio hilo Rais Magufuli hakuwahi kusema chochote juu ya shambulio hilo.

View attachment 2504783
Ukweli ndiyo huo
 
Kwahiyo yeye alikuwa anapinga nchi? Kwanini amehusianisha kauli hii na yeye? Inamaana inside his heart anajua alikuwa anapinga nchi ila hataki mpinga nchi afanywr anacho stahili, is it what he meant?

Mh. Sana punguza jazba, tumia busara, now he is gone, badala ya kupigia mistari presuppositions/assertions za wenye hisia ya unachokisema, tumia weledi kuongoza then all things will fall inline...Kila la heri Mh. Sana, ni ushauri tu!
 
Kazi mnayo. Vumilieni tu. Kosa kubwa lilofanyika ni kumshambulia na kumiss target.hilo kosa litawakost
1) Mwaka huu ni wangapi tangu Tundu Lissu apigwe risasi?

2) Amefanya nini?

3) Kimetokea kitu gani?

4) Yeyekitenfo hichi kimemsaidia nini mbali ya kuvunjwa miguu?

5) Na baada ya yeye nani mwingine amepigwa risasi na amevunjwa miguu?

Itusaidie kufikiri na kufanya critical path analysis.

Tusikatae maneno ya Lissu kuwa hayana maana na pia tusishangilie tukio zima kama Mazuzu.
 
Ni aibu serikali kutumia risasi nyingi kiasi hicho kumuuwa mtu mmoja. Hata kama ni taifa masikini sana na ambalo halina wasomi haliwezi kufanya ujinga huo. Ukitumia akili vizuri ni kuwa "serikali haikuhusika".
 
Pia rais ni taasisi. Sasa mtu huko atoke anakotoka. Halafu aanze kusema rais ni muuaji. Hiyo inaleta taswira gani kwa wananchi kuhusu taasisi hiyo ya urais? Tundu lisu katukosea watanzania tulio wengi.
Sema amekukosea wewe, siyo Watanzania. Kama Rais alikuwa muuaji kwa nini asisemwe?

Tena siyo iishie tu kusemwa bali lazima siku moja ije taarifa kamili inayoonesha na kutaja wazi wahusika wote. Tunafahamu yeye alitoa maagizo, kuna waliosimamia utekelezaji, kuna waliotekeleza, kuna waliohusika na ninyi mnaojitihidi kumtetea muuaji, ninyi ni sehemu ya wale wauaji. Nyote itabidi majina yenu yawekwe wazi, na uhusika wa kila mmoja wenu katika shambulio lile na mauaji mengine ambayo yalifanywa kwa waliokuwa wakimkosoa muuaji.
 
Unaweza kumuua kichaa? Mbowe alivyosema alivamiwa kumbe mlevi tu ilikuwa sahihi? Kwanini Lissu hataki dereva wake ahojiwe? Ikitokea suala hili likaenda mahakamani atakataa asihojiwe? Kwanini?
Si yupo maneno maneno ya nini kila siku wakati mtendewa yupo fanyeni taratibu za kisheria ashughulikiwe la sivyo maneno ya uongo hayatasaidia kitu.
 
CCM na CDM watakavyo malizana kwenye majukwaa ya siasa watajua wenyewe..

Hila humu JF kwa sie ambao tunaelewa Magufuli hakuwa perfect ila dhamira yake ilikuwa njema kwa Tanzania awezi dhalilishwa kamwe. Either the culprit ni CDM au CCM.

Bora Magufuli kuliko (bi tozo + JK) binafsi nipo tayari kunyofolewq kucha kwa kauli hiyo ata pliers zikiwa mbele yangu.
Rais muuaji hatakiwi Tanzania.
 
Pia rais ni taasisi. Sasa mtu huko atoke anakotoka. Halafu aanze kusema rais ni muuaji. Hiyo inaleta taswira gani kwa wananchi kuhusu taasisi hiyo ya urais? Tundu lisu katukosea watanzania tulio wengi.
Kutomhuaisha Magufuli na shambulio la Lissu ni kumkosea Mungu. Tena utubu mapema.
 
Back
Top Bottom