Tundu Lissu achukua fomu kugombea Makamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa

Mbona Sumaye kapigiwa kura ya Hapana na alikuwa mgombea pekee? Si ndiyo demokrasia hiyo? Ama hujui? Sembuse Mbowe anapambana na majabali mawili?
Wameweka wagombea vivuli mkuu ,kwanini kuwe na vipindi vingi vya kutawala je? Huyu msukuma akiongeza vipind mtafurahi mkuu
 
Mbowe ametumua akili nyingi na kiufundi wa hali ya juu sana. Kumfanya lissu naibu wake, kumlazimisha Abdallah Safari ajitoe na apishe nafasi.

Lakini Mbowe asitudanganye sisi sio wale nyumbu wake.
1. Hakuwa na nia ya kuachia kamba, bali mbinu za kisiasa za kiafrika. Japokuwa mie siyo mwana cdm, lakini ni mmoja wa watu waliopendelea aendelee kwa wakati, kwani Mbowe hana madhara makubwa kwa chama changu CCM.
2. Kumleta Lissu, kitakisaidia chama changu kurudia misingi yake ya kiutendeji, na atatusaidia kuwaumbua hawa maMBUMBU walio kiteka chama chetu.
3. Mbowe ndiye aliyemjengea mizingwe Sumaye, na amefanya vizuri sana, na tunaomba asirudi nyumbani, CCM sio ward ya hospitali.

Naiombea Chadema uchaguzi tulivu na watuletea siasa zenye tija na kuwaamsha CCM Asilia usinginzini.
Kama haya yanatoka moyoni,Mungu wa mbinguni akubariki na ufahamu wako ukawe bora maradufu.Huwa nawaza kama wewe,tofauti moja tu mimi siyo mfuasi wa chama chochote bali haki.
 
Mbona Sumaye kapigiwa kura ya Hapana na alikuwa mgombea pekee? Si ndiyo demokrasia hiyo? Ama hujui? Sembuse Mbowe anapambana na majabali mawili?

Sumaye kapigiwa kura ya hapana halafu nini kinafuata, Pwani hakutakuwa na Mwenyekiti?

Katiba ya CHADEMA ni mkorogo

Kwa nini Sumaye asipite bila kupingwa?
 
Sumaye kapigiwa kura ya hapana halafu nini kinafuata, Pwani hakutakuwa na Mwenyekiti?

Katiba ya CHADEMA ni mkorogo

Kwa nini Sumaye asipite bila kupingwa?
Mambo ya kupita bila kupingwa yako huko kwenu CCM
 
Safi sana good idea baada ya kunyang'anywa ubunge Lissu alikuwa amepoteza political platform ndio watesi wake walichokitaka kwa kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti sasa atapata tena platform ya kisiasa aanze tena kumkaanga jiwe.
 
Hivi humu jamvini na wagonjwa wa akili nao tunachangia nao mijadala,Max aliangalie hili suala.
Najua mmeiga mengi na Kama mnataka kuiga na hili. Ondoeni kwenye katima ya ccm. Katiba nchi inawahusu wote kwenye vyama na wasio na vyama. Hivo usijitoe ufahamu ukahisi raisi ni kwa ajili ya wanachama wa chama fulani tu.
 
WanaJF

Habari za hivi Punde ni kwamba Jabali la kisiasa Tanzania na Afrika Tundu Antipas Lissu amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa na tayari amekwisha jaza fomu na kuzirejesha.

Akihutubia mkutano mkuu wa Kanda ya Kaskazini hivi Punde,Mwenyekiti wa chama Taifa Freeman Aikael Mbowe ameeleza kuhusu tukio hilo la kishujaa alilofanya Tundu Lissu.

Mbowe amesema Makamu Mwenyekiti wa sasa Professor Abdallah Safari ameomba kupumzika na hivyo Lissu ameona ni wakati muafaka kwake kuomba nafasi hiyo.

Wakati huo huo, Freeman Aikael Mbowe amekubali maombi ya vijana nchi nzima ya kugombea tena nafasi ya Mwenyekiti Taifa na amerejesha fomu yake kwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa.

Akirejesha fomu hiyo huku akishangiliwa kwa mayowe na wajumbe wa mkutano mkuu Kanda ya Kaskazini Mbowe amesema alichukua muda mrefu kutafakari ombi hilo la vijana na alikuwa na nia ya kutogombea tena nafasi hiyo.Hata hivyo amesema alirudisha moyo nyuma baada ya kutizama imani kubwa waliyo nayo wanachadema kwake na kuona akikataa maombi yao itakuwa ni kuwasaliti.

Akizungumzia yaliyotokea katika uchaguzi Kanda ya Pwani Mbowe amesema amesikitishwa na mambo ya uongo yanayoandikwa na baadhi ya watu na akasema kwenye mambo haya ya uchaguzi huwezi kuzuia ajali za kisiasa.Hata hivyo amewahakikishia watanzania kwamba Mhe Sumaye anahitajika ndani ya Chadema kama walivyo wanachama wengine na amesema yaliyotokea yatamalizwa kwa upendo na nidhamu ya hali ya juu ndani ya chama.
Mbowe alipaswa kupumzika.
Hata Nyerere aliombwa kuendelea na urais lakini hakuendekeza hisia za watu.
Tundu lisu alipaswa kuchukua form ya uenyekiti wa Taifa, period
 
Katika hili waandishi wasilaumiwe, tatizo ni sumaye sanasana, anaamini demokrasia mdomoni, akishindwa haitaki tena.
Kwa akili ya kawaida kabisa, huwezi kusema Demokrasia imemtoa Sumaye. Mtu alikua mgombea pekee hana mshindani, maana yake busara ingetumika kwamba amepita bila kupingwa. Katiba ya CDM inasema nafasi za uongozi zitakua za ushindani kwa kupigiwa kura. Sasa tujiulize Sumaye alikua anashindana na nani?
 
Mwenyekiti wa CCM anapigiwa kura ya Ndiyo au Hapana?
 
Mbowe alipaswa kupumzika.
Hata Nyerere aliombwa kuendelea na urais lakini hakuendekeza hisia za watu.
Tundu lisu alipaswa kuchukua form ya uenyekiti wa Taifa, period
Hujui usemacho.Nakushauri kunywa maji ulale
 
Safi sana good idea baada ya kunyang'anywa ubunge Lissu alikuwa amepoteza political platform ndio watesi wake walichokitaka kwa kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti sasa atapata tena platform ya kisiasa aanze tena kumkaanga jiwe.
Kawashika pabaya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom