Tundu Lissu achukua fomu kugombea Makamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa

Aisee sikujua kuwa kuchukua fomu ni tukio la kishujaa.??

Any ways I hope hiyo fomu imejazwa vyema sio kama zile za Uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
M/MUNGU ILINDE CHADEMA NA VIONGOZI WAKE ✌🏾✌🏾✌🏾💪🏾💪🏾💪🏾
 
Tundu Lisu na DJ si ndio walio nunuliwa na maMvi kwa vipande vya fedha na yule aliyehoji ujio wa maMvi ali furushwa kwenye chama. Leo hii Nyumbu wana kushangilia wanaona wanapiga hatua za kisiasa. Kwa hakika aliye waita nyumbu hakukosea hata kidogo.
Afadhali huyo ndiye atakaye weza kulambana na hujuma za jiwe
 
WanaJF

Habari za hivi Punde ni kwamba Jabali la kisiasa Tanzania na Afrika Tundu Antipas Lissu amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa na tayari amekwisha jaza fomu na kuzirejesha.

Akihutubia mkutano mkuu wa Kanda ya Kaskazini hivi Punde,Mwenyekiti wa chama Taifa Freeman Aikael Mbowe ameeleza kuhusu tukio hilo la kishujaa alilofanya Tundu Lissu.

Mbowe amesema Makamu Mwenyekiti wa sasa Professor Abdallah Safari ameomba kupumzika na hivyo Lissu ameona ni wakati muafaka kwake kuomba nafasi hiyo.

Wakati huo huo, Freeman Aikael Mbowe amekubali maombi ya vijana nchi nzima ya kugombea tena nafasi ya Mwenyekiti Taifa na amerejesha fomu yake kwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa.

Akirejesha fomu hiyo huku akishangiliwa kwa mayowe na wajumbe wa mkutano mkuu Kanda ya Kaskazini Mbowe amesema alichukua muda mrefu kutafakari ombi hilo la vijana na alikuwa na nia ya kutogombea tena nafasi hiyo.Hata hivyo amesema alirudisha moyo nyuma baada ya kutizama imani kubwa waliyo nayo wanachadema kwake na kuona akikataa maombi yao itakuwa ni kuwasaliti.
Huyu Tundu bana kumbe alitumiwa nauli kuja Kenya kujaza fomu?khaa
 
CDM WATAFAKARI, WAAMUE, WASIMLAUMU YEYOTE KWA WATAKACHOAMUA.

Hali yao wanaijua CDM; Viongozi waliowafikisha hapo walipo wanawafahamu.
Watafakari sana, waamue. Wakiona wanawafaa wawachague; wakiboronga wasimlaumu mtu, wajilaumu wenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom