Tundu Lissu achukua fomu kugombea Makamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
13,933
Points
2,000

Molemo

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
13,933 2,000
WanaJF

Habari za hivi Punde ni kwamba Jabali la kisiasa Tanzania na Afrika Tundu Antipas Lissu amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa na tayari amekwisha jaza fomu na kuzirejesha.

Akihutubia mkutano mkuu wa Kanda ya Kaskazini hivi Punde,Mwenyekiti wa chama Taifa Freeman Aikael Mbowe ameeleza kuhusu tukio hilo la kishujaa alilofanya Tundu Lissu.

Mbowe amesema Makamu Mwenyekiti wa sasa Professor Abdallah Safari ameomba kupumzika na hivyo Lissu ameona ni wakati muafaka kwake kuomba nafasi hiyo.

Wakati huo huo, Freeman Aikael Mbowe amekubali maombi ya vijana nchi nzima ya kugombea tena nafasi ya Mwenyekiti Taifa na amerejesha fomu yake kwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa.

Akirejesha fomu hiyo huku akishangiliwa kwa mayowe na wajumbe wa mkutano mkuu Kanda ya Kaskazini Mbowe amesema alichukua muda mrefu kutafakari ombi hilo la vijana na alikuwa na nia ya kutogombea tena nafasi hiyo.Hata hivyo amesema alirudisha moyo nyuma baada ya kutizama imani kubwa waliyo nayo wanachadema kwake na kuona akikataa maombi yao itakuwa ni kuwasaliti.

Akizungumzia yaliyotokea katika uchaguzi Kanda ya Pwani Mbowe amesema amesikitishwa na mambo ya uongo yanayoandikwa na baadhi ya watu na akasema kwenye mambo haya ya uchaguzi huwezi kuzuia ajali za kisiasa.Hata hivyo amewahakikishia watanzania kwamba Mhe Sumaye anahitajika ndani ya Chadema kama walivyo wanachama wengine na amesema yaliyotokea yatamalizwa kwa upendo na nidhamu ya hali ya juu ndani ya chama.
 
joshydama

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Messages
3,580
Points
2,000

joshydama

JF-Expert Member
Joined May 10, 2016
3,580 2,000

Kwanini Tundu Lissu akili kubwa anazidiwa na Mbowe? TL ilibidi ndiye awe mwenyekiti na siyo Mbowe. CHADEMA ni wanafiki sana.
 
Forum statistics

Threads 1,367,636
Members 521,789
Posts 33,405,697
Top