Tundu Lissu: Acheni kutunga uongo, mshaurini Rais Samia awataje na kuwakamata walionishambulia

Mwanasheria nguli amekuwa mbogo na kutaka watu kutozua uongo kuwa hamkosoi mama Samia kuwa anakubaliana nae. Bali ametaka watu wamshauri ili waliompiga risasi wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Pia ndugu Lissu amedai kuwa kuliko kuzua uongo bora wamshauri mama Samia ili yeye alipwe haki zake alizoporwa na utawala CCM chini ya hayati JPM.

Lissu amekuwa mbogo baada ya watu wasio wema kuzua kuwa anamsifia mama Samia kwa ukarimu alionyesha baada ya kumtembelea hospitalini huko Nairobi Kenya.

Lissu na Lema plus their immediate families waendelee tu kufugwa na wazungu kama pets. Msimu wa uchaguzi unapofika, maisha yao hayako hatarini, lakini uchaguzi unapoisha na wao kuangukia pua, maisha yao yanakuwa hatarini kuliko ya mpinzani mwingine yeyote! Bure kabisa!
 
..wewe unaweza usione kuwa ni jambo la msingi, lakini wapo wengine kwao ni jambo la msingi.

..kinachotakiwa ni HAKI itendeke na waliofanya unyama dhidi ya Lissu na waliowatuma wakamatwe na kujibu mashtaka mahakamani.

..fikiria kama wewe ungekuwa ndio Lissu, mwanafamilia, rafiki, wote tunastahili kulindwa na kutendewa haki tunapopatwa na tatizo kama lililomtokea.
Unapiga kelele na wapumbavu wasiojielewa.
 
Kama Mama alijipambanua anataka HAKI,hili la Lissu ndio kipimo kikubwa cha haki kutendeka pamoja na mengine.

Wahusika wafunguliwe mashtaka dhidi yao,watetezi wa udhalimu huu wanaiingiza nchi kwenye laana,na balaa.

Watanzania hatutaki kuwa sehemu ya ukiukwaji HAKi wa namna hii.
 
Pia ndugu Lissu amedai kuwa kuliko kuzua uongo bora wamshauri mama Samia ili yeye alipwe haki zake alizoporwa na utawala CCM chini ya hayati JPM.

Lissu amekuwa mbogo baada ya watu wasio wema kuzua kuwa anamsifia mama Samia kwa ukarimu alionyesha baada ya kumtembelea hospitalini huko Nairobi Kenya.

Lakini Mama anastahili sana pongezi kwa ujasiri ule, haikuwa rahisi kwa hali ilivyokuwa, tumeshuhudia wangapi walitenguliwa kutokana na kumtembelea Lissu
 
Askari wa CCM? U mzima kweli wewe! Hata hivyo nakuhakikishia kwamba kama CCM kweli wanao askari wao, haitakuwa ajabu kummiminia mtu risasi hata mia na wasifanikiwe kumuua. Madarakani amekaa miaka karibia sitini lakini hawajawahi kufanikiwa katika malengo yao ya kuikwamua nchi katika umasikini.
Sio kauli yangu ,Hiyo ilikuwa ni kauli ya Rais mnaetaka aunde tume ya kichunguza mauaji ya Lissu.
 
huyu njaa inamtafuna
analalama alipwe nini
Mwanasheria nguli amekuwa mbogo na kutaka watu kutozua uongo kuwa hamkosoi mama Samia kuwa anakubaliana nae. Bali ametaka watu wamshauri ili waliompiga risasi wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Pia ndugu Lissu amedai kuwa kuliko kuzua uongo bora wamshauri mama Samia ili yeye alipwe haki zake alizoporwa na utawala CCM chini ya hayati JPM.

Lissu amekuwa mbogo baada ya watu wasio wema kuzua kuwa anamsifia mama Samia kwa ukarimu alionyesha baada ya kumtembelea hospitalini huko Nairobi Kenya.
 
Ni kweli mama awataje ila na yeye atuambie pesa za Kenyatta alizopewa alizipokea kwa Minajili gani!?
 
Lini hiyo? Hivi mmesahau kuwa wakati wa kampeni Mama yako aliwajibu kwa kuwambia kuwa, hakuna askari wa Serikali ya CCM anaeweza kukosa risasi zaidi ya tatu na akaendelea kubaki kazini?

Endeleeni kujitia moyo sasa, sisi tunawashauri vizuri kabisa kwamba kiki ya Risasi kwasasa haina nguvu tena, badilisheni gia.
Kama mnataka hii Nchi iwe kama Somalia tutafika bila wasiwasi.
 
Kama mnataka hii Nchi iwe kama Somalia tutafika bila wasiwasi.
Hahahaaaa..! We keyboard warrior acha kuchekesha watu hapa, wakuifikisha hii nchi katika level za somalia sio nyinyi ambao mara kadhaa mmeshindwa kuingia road hata baada ya kuhamasishwa na viongozi wa magenge yenu, labda kama unamaanisha kuna nchi ya kusadikika.
 
Ni kweli, mama Samia hebu washughulikie hawa WAHUNI waliokuwa wanateka teka watu kuwatesa hadi baadhi kuwaua bila kufuata misingi ya sheria za nchi.

Kuna mmoja anaranda-randa mitaani hebu anza naye huyo kwanza ili utupe furaha watanzania ya kufungia mwaka 2021.
 
Unapiga kelele na wapumbavu wasiojielewa.

..mdogo-mdogo tutaelewana tu.

..aliyekuwa akifarakanisha Watz hayuko nasi tena.

..sasa Watz tuna nafasi ya kutendeana HAKI.

..Tusipoteze nafasi hii adhimu.
 
Mwanasheria nguli amekuwa mbogo na kutaka watu kutozua uongo kuwa hamkosoi mama Samia kuwa anakubaliana nae. Bali ametaka watu wamshauri ili waliompiga risasi wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Pia ndugu Lissu amedai kuwa kuliko kuzua uongo bora wamshauri mama Samia ili yeye alipwe haki zake alizoporwa na utawala CCM chini ya hayati JPM.

Lissu amekuwa mbogo baada ya watu wasio wema kuzua kuwa anamsifia mama Samia kwa ukarimu alionyesha baada ya kumtembelea hospitalini huko Nairobi Kenya.

====

View attachment 1825167

View attachment 1825169
wewe mwenyewe unawajuwa hutaki kuwataja dreva umemficha huko unataka watu wapige ramli kuwajuwa? wewe ulidhurumu watu wakakufanya hivyo unakuja kubebesha watu mizigoi ya ujinga wako?
 
Back
Top Bottom