Tundu Lissu achambua Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari bungeni

Lissu ni moja ya wanasiasa ambao kusema kweli wanazitendea haki taaluma zao na Mungu anamwona kwa jinsi anavyojitoa kueleza ukweli huku taaluma yake ikiwa inamwongoza.Baadhi ya wanasiasa mimi maranyingi huwa nikitafakari kwanini huwa wanakaa kimya pale wanapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo bila ya kukemea nakosa jibu linaloweza kuniridhisha.Mle bungeni kuna watu ambao wanavyojifanya vipofu wa mambo hadi unaweza usiamini kama kweli ni wasomi mahiri kabisa badala yake unaweza ukaamini kua walikariri wakafaulu mitihani yao.Watu kama Mwakyembe,Tulia na wengineo wamo mle wametulia tu,sasa sijui wataacha legacy gani nzuri yakuweza kupunguza matusi pale watakapoaga dunia kama mzee wetu Sitta ambaye pamoja na kuteleza kipindi cha bunge maalum la katiba lakini kuna mambo ambayo aliyafanya kipindi cha nyuma na jamii inayakubali.Live long Lissu.
 
Back
Top Bottom