Uchaguzi 2020 Tundu Lissu achambua mifuko ya Jamii na fao la kujitoa, CCM jibuni hoja hizi

Nikikumbuka ka milioni 3 kangu kamepotelea nssf huko..hasira zilipanda zikashuka nikatulia. Lisu amenikumbusha kidonda cha uchungu...CCM wameng'ang'ania pesa yangu tangu 2016.. Wakidai bado nachangia alafu hakuna mchango unaoingia tangu mwaka huo. CCM nikiwafikiriaga naona Lucifa pure, hasa nikitembea mabarabarani nikiona mabandiko yake huwa naona kama nimeingia kuzimu Lucifa anajinadi kila kona...natembea full kukemea kwa Jina la Yesu.tokaa!
 
Tatizo la wafanykazi wa Tanzania ni midabwada, watu hopeless and stupid ! Kuna wale ambao wana ka upenyo ka kupata bakishishi/marupurupu kazini, haya ya mifuko hayawahusu, "wanafidia" huku wanakochota. Kundi la walimu (siyo wote tafadhali, ila wengi wao wako hivyo) ni kundi la academic failures ambao walipata Div 4 na hivyo kujiona "afadhali" wanapata hata hicho kidogo! WAMEGAWANYIKA katika makundi ya imani/itifaki mbali mbali. Mapolisi/wanajeshi ni academic failures, wao wanaona kama wamekuwa favoured na hiyo wanashukuru hata kidogo hicho wanachokipata, wanapata virushwa rushwa, wanaona ahueni. Kuwaunganisha siyo kazi rahisi! Wanahitaji mental liberation!
Duu!! Mkuu hapa kuna ukweli mchungu
 
Wakakope.
Hizo fedha hazipo zilishapigwa kitambo,wanaokoteza michango ndipo wawalipe kwa mafungu.Ndiyo maana waliunganisha mifuko bila kuwashirikisha wenye mifuko(wafanyakazi) wa umma na binafsi.
Kiukweli hii mifuko ya hifadhi ya jamii ilishafilisika.
 
CCM hawana uwezo wa kuzijibu hizo hoja.Mwenyekiti wao mwenyewe anakimbia mdahalo 😂😂😂😂
 
Ila Magufuli na serikali yake mmewadhulumu watumishi wasio na hatia. Mtu afanye kazi miaka kadhaa na baada ya hapo apoteze ajira na huku ana michango yake NSSF anateseka na njaa na watoto Wake, halafu unamwambia eti asubiri atimize miaka 55.!?
Huu ni unyama, ni uporaji na unyonyaji.
Viongozi hawaoni hili kwa kua wanalishwa na kuhudumiwa na kodi za wavuja jasho lakini huu ni ukatili mkubwa sana kwa watumishi walipoteza ajira zao ili hali akiba zao waliojiwekea zibazuiluwa NSSF kuwanufaisha wakubwa.
Wao wanajilipa baada ya miaka 5 tu!
 
Huu ni msumari wa moto.
CCM hawatajibu lolote la maana, sana sana watasema kuweni wazalendo kwa nchi yenu.
Ukoo wa panya!
Hawawezi kujibu kwasababu hakuna hoja yoyote aliyotoa. Kwa taarifa yako, HAKUNA FAO LA KUJITOA kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii dunia nzima isipokuwa Tanzania. Na Tanzania iliwezekana kwasababu ya Sera Nzuri ya Chama cha Mapinduzi. Kwahiyo namshukuru sana Tundu Lissu kwa kutetea Sera Nzuri za CCM!!!
 
Huu ni msumari wa moto.
CCM hawatajibu lolote la maana, sana sana watasema kuweni wazalendo kwa nchi yenu.
Ukoo wa panya!


hahaha sasa cha ajab nn apo, kwan ulidhan pesa zinachukuliwa ili zitunzwe? hio ni financial service means they can do anything about your money, ni sawa na benki tu wanavokopesha watu pesa na bado waliokopa wanashindwa kurudisha! ni kitu cha kawaida
 
hahaha sasa cha ajab nn apo, kwan ulidhan pesa zinachukuliwa ili zitunzwe? hio ni financial service means they can do anything about your money, ni sawa na benki tu wanavokopesha watu pesa na bado waliokopa wanashindwa kurudisha! ni kitu cha kawaida

Acha kurukaruka kama maharage kwenye sufuria...jibu hii hoja ya mdau hapo chini.
Wabunge wakimaliza kipindi chao wanalipwa pesa yao yote haraka kabisa bila kuzungushwa na pia bila kuambiwa wasubiri wafikishe miaka sitini.

Kwanini huo utaratibu wao maalum wa kupata mafao usitumike kwa wafanyakazi wote?

Suala ni tuache siasa za aina gani. Hawa wanasiasa wanaojivika uzalendo uchwara kuhusu hela za wafanyakazi wao wenyewe wametengenezewa utaratibu maalum ambapo wanakatwa na NSSF halafu baada ya kumaliza ubunge wanarudishiwa pesa zao.
 
Nadhani hii nadharia ya fao la kujitoa inaficha tatizo la msingi lililopo kwenye nguvu kazi ya taifa, watu wafukuzwe kazi hovyo kwa sera mbovu ukimbilie kuwalipa fao la kujitoa, nani kakwambia nssf ni tigopesa muda wowote unarusha?

Hebu tujiulize nchi zingine wanafanyaje? Ujerumani na Uingereza fedha za NSSF ndizo hutumika kusomesha watoto wa wafanyakazi, sisi watoto wanaenda kukopeshwa fedha kwenye saccos ya serikali inayoitwa bodi ya mikopo.

Ujerumani hamna mfanyakazi anayejenga nyumba ya kuishi, ukipata ajira na kupata namba ya NSSF unaenda kukopa nyumba na dhamana yako ni hiyohiyo nssf yako. sisi kila mtu ni civil engineer, kila mtu anamiliki kampuni ya ujenzi, kila mfanyakazi ukimuuliza mfuko mmoja wa simenti unatoa tofali ngapi wote watakupa jibu sahihi si daktari wala mwalimu wa history, leo hii kila mfanyakazi angekopa nyumba nhc kwa kutumia nssf yake hakuna mtu angehangaika na fao la kujitoa.

Leo kila mfanyakazi anamiliki kamkweche kalikoshindikana japan na uarabuni, zote hizi wananunua kwa cash, japan wanakotengeneza magari hamna mfanyakazi anaenunua gari kwa cash wote wanakopeshwa kwa kutumia namba zao za NSSF.

Hivi huyu kijana tunayemhangaikia kupewa fao la kujitoa angekuwa na nyumba ya mkopo kutoka nssf angekuwa na gari la mkopo wa nssf angekuwa anasomeshewa mtoto na nssf angehangaika na fao la kujitoa kweli?
 
Watupe chetu bana wengine tangu 2017 tunazifuatilia,longo longo nyingi mpaka sasa bila bila kesho natimba tena ofisini kwao kufuatia mafao yangu. Sometimes mtu unajuta kuzaliwa nchi yenye laana kama hii ya Tanzania aseee.


Serikali naichukia sana hii.
 
Sasa shughuri ndokwaanza imeanza tunasubiri tuambiwe ripoti za CAG za miaka yote Mitano,tunataka tuambiwe matumizi ya Serikali yasasa yamepungua ama la ! Maana tulikuwa gizani kipindi chote Cha miaka5,tunataka kujua kwanini Deni linekuwa kwa Kasi nahuku tukiwa namakusanyo Bora kuliko awamu zote,pia tunataka tufahamu utekelezaji wa ilani yao ni kwakiasi gani wametekeleza? ili tupate kuona Kama tunaweza waamini tena TL tunaamini utatueleza yote huwenda wenye wajibu wakusema wasiseme,,
Makusanyo bora kuliko awamu zote ? Kwa kiasi fulani ni kweli lakini vipi kuhusu matumizi yake ?Tuna shida ya matumizi yasiyo na tija kama nchi
 
Kiukweli huu utofauti wa wenzetu miaka mitano tu wanapata chao 240ml halafu sisi walala hoi milioni 2/3/4/5/10 unaambiwa usubiri au utafute kazi nyingine sijui hawaelewi kwamba wanatupandikizia chuki na uwekaji huu wa matabaka.
Hapa ndipo ninapoichukia sheria ya hifadhi ya jamii Tanzania
 
Back
Top Bottom