Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aanza kukumbana na wananchi wakitaka maendeleo ya vitu

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
3,730
2,850
Nimewasikia wananchi wa eneo moja huko Mufindi kama sikosei kwenye mkutano wa ndugu Tundu Lisu kuwa hawana barabara pamoja na maji na wamesema wanaomba akichaghuliwa awatengenezee hivyo vitu.

Nikajiuliza kwa nini hao watu hawahitaji maendeleo ya watu wao wametaka maendeleo ya vitu?

Majibu ya Tundu Lissu ni kwamba, hata yeye anashangaa kwa nini mpaka sasa hawana barabara na maji na kwamba mpaka huko alipotokea mpaka kufika pale jana yake ametembea kwenye njia ya vumbi mpaka alipofika kwenye mkutano akawa amechoka sana hadi kutaka kuahirisha mkutano.

Swali langu kwa Tundu Lissu.
Kama yeye na pesa aliyonayo na magari aliyotumia bado amepata maumivu kwa kupita barabara ya vumbi, je anakubali maendeleo ya vitu ni moja ya kurahisisha maendeleo ya watu?

Anaweza kufahamu kuwa kuna watu pia wanahitaji usafiri wa ndege kuwapeleka sehemu husika na pengine kunusuru maisha yao tofauti na wangetumia barabara wasingepona kutokana na umbali?

Je, unaweza kuwa na mapesa mengi na magari mazuri lakini ili ufike kwako ni lazima ukanyage tope kwa kusukuma gari yako na ukifika kwako huna hata umeme unatumia kibatari na gari yako inakuwa chafu muda wote na ndani mwako vumbi kibao kutokana na barabara ya vumbi ambayo magari yakipita vumbi yote inajaa ndani mwako.

Je, utafurahi na maisha hayo ya uchafu kila siku ila una pesa?

Je, Tundu Lissu akiingia madarakani atatekeleza maombi ya hao wananchi ya barabara na maji waliyoomba au atataka awajaze pesa ili wawe na furaha kwanza?
 
Acha upotoshaji! Watanzania tulio wengi tunataka maendeleo ya vitu yaende sambamba na maendeleo ya watu! Hakuna mfanyakazi atakayekubali kunyimwa haki zake za msingi mfano kupandishwa daraja kwa wakati, kisa eti unajenga barabara au kununua ndege!

Mbona wakati wa JK hizo barabara, madaraja, nk vyote hivyo vilijengwa kila kona ya nchi! Lakini bado ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu, haki za wafanyakazi na makundi mengine katika jamii ziliheshimiwa?

Iweje huyu mtu wenu aone barabara na ndege ni vitu vya muhimu sana kuliko haki za wengine? Mbona hatujawahi kumsikia akijipunguzia mshahara na posho zake?

Hata Rais angekua ni Lissu au Hashimu Rungwe, bado hizo barabara zingejengwa tu. Hilo ni moja ya jukumu la serikali yoyote ile duniani. Na kodi tunazolipa na mikopo ya ndani na nje ya nchi, hufanikisha zoezi hilo.
 
..ameuliza kwanini ujengwe uwanja wa chato badala ya barabara za huko Mufindi.

..ameuliza kwanini lijengwe daraja la baharini la kupunga upepo hapa Dsm badala ya barabara ya Mikumi-Kilombero-Ifakara-Mlimba.
Mbona hajawahi kusema uwanja wa ndege wa Singida usijengwe mpaka Tanzania yote ipate huduma ya maji barabara na umeme na wawe na furaha ndio huo uwanja ujengwe maana haina maana.
 
Nimewasikia wananchi wa eneo moja huko mufindi kama sikosei kwenye mkutano wa ndugu Tundu Lisu kuwa hawana barabara pamoja na maji na wamesema wanaomba akichaghuliwa awatengenezee hivyo vitu.

Nikajiuliza kwa nini hao watu hawahitaji maendeleo ya watu wao wametaka maendeleo ya vitu?

Majibu ya Tundu lisu ni kwamba, hata yeye anashangaa kwa nini mpaka sasa hawana barabara na maji, na kwamaba mpaka huko alipotokea mpaka kufika pale jana yake ametembea kwenye njia ya vumbi mpaka alipofika kwenye mkutano akawa amechoka sana hadi kutaka kuahilisha mkutano.

Swali langu kwa Tundu Lissu.
Kama yeye na pesa aliyo nayo, na magari aliyotumia bado amepata maumivu kwa kupita barabara ya vumbi, je anakubali maendeleo ya vitu ni moja ya kurahisisha maendeleo ya watu?

Anaweza kufahamu kuwa kuna watu pia wanahitaji usafiri wa ndege kuwapeleka sehemu husika na pengine kunusuru maisha yao tofauti na wangetumia barabara wasingepona kutokana na umbali?

Je, unaweza kuwa na mapesa mengi na magari mazuri lakini ili ufike kwako ni lazima ukanyage tope kwa kusukuma gari yako na ukifika kwako huna hata umeme unatumia kibatari na gari yako inakuwa chafu mda wote na ndani mwako vumbi kibao kutokana na barabara ya vumbi ambayo magari yakipita vumbi yote inajaa ndani mwako.

Je, utafurahi na maisha hayo ya uchafu kila siku ila una pesa?

Je, Tundu lisu akiingia madarakani atatekereza maombi ya hao wananchi ya barabara na maji waliyo omba au atataka awajaze pesa iii wawe na furaha kwanza?

Maendeleo ya vitu yaendayo kuboresha maisha ya watu yagusayo maisha ya watu. Kujenga Ikulu mpya Hali toshelevu ya awali ipo, kujenga Chato na Dodoma hivi haviwasaidii watu bali ni hitaji la mtawala na sio kipaumbele Cha wananchi na wala havigusi maisha ya watu sababu si hitaji la lazima.
 
Unadhni hiyo pesa ya Charo na hilo daraja la baharini vingemaliza matatizo ya barabara tanzania nzima?

..bila shaka kungekuwa na unafuu kuliko sasa hivi.

..wewe jiulize wananchi wangapi wanatumia huo uwanja wa ndege wa kimataifa wa chato?

..binafsi angejenga barabara za lami chato au geita nisingemlaumu hata kidogo.

..angewekeza kwenye vyuo vya ufundi badala ya uwanja wa ndege ningeunga mkono uwekezaji huo.

NB:

..daraja la baharini la kupunga upepo Dsm wangeshawishi lijengwe na sekta binafsi. Na wanaotaka kupita huko wangelipia kama tunavyofanya kwenye daraja la kigamboni.
 
Nimewasikia wananchi wa eneo moja huko mufindi kama sikosei kwenye mkutano wa ndugu Tundu Lisu kuwa hawana barabara pamoja na maji na wamesema wanaomba akichaghuliwa awatengenezee hivyo vitu.

Nikajiuliza kwa nini hao watu hawahitaji maendeleo ya watu wao wametaka maendeleo ya vitu?

Majibu ya Tundu lisu ni kwamba, hata yeye anashangaa kwa nini mpaka sasa hawana barabara na maji, na kwamaba mpaka huko alipotokea mpaka kufika pale jana yake ametembea kwenye njia ya vumbi mpaka alipofika kwenye mkutano akawa amechoka sana hadi kutaka kuahilisha mkutano.

Swali langu kwa Tundu Lissu.
Kama yeye na pesa aliyo nayo, na magari aliyotumia bado amepata maumivu kwa kupita barabara ya vumbi, je anakubali maendeleo ya vitu ni moja ya kurahisisha maendeleo ya watu?

Anaweza kufahamu kuwa kuna watu pia wanahitaji usafiri wa ndege kuwapeleka sehemu husika na pengine kunusuru maisha yao tofauti na wangetumia barabara wasingepona kutokana na umbali?

Je, unaweza kuwa na mapesa mengi na magari mazuri lakini ili ufike kwako ni lazima ukanyage tope kwa kusukuma gari yako na ukifika kwako huna hata umeme unatumia kibatari na gari yako inakuwa chafu mda wote na ndani mwako vumbi kibao kutokana na barabara ya vumbi ambayo magari yakipita vumbi yote inajaa ndani mwako.

Je, utafurahi na maisha hayo ya uchafu kila siku ila una pesa?

Je, Tundu lisu akiingia madarakani atatekereza maombi ya hao wananchi ya barabara na maji waliyo omba au atataka awajaze pesa iii wawe na furaha kwanza?
Wewe ni great thinker, ubarikiwe sana
 
Mbona hajawahi kusem uwanja wa ndege wa singida usijengwe mapka tanzania yote ipte huduma ya maji barabara na umeme na wawe na fulaha ndo huo uwanja ujengwe maana haina maana.

..nadhani wananchi wa Singida, na viongozi wao waliowachagua, kwa maana ya wabunge na madiwani, watachagua umeme, maji, na barabara, badala ya uwanja wa ndege.
 
Vitu
Acha upotoshaji! Watanzania tulio wengi tunataka maendeleo ya vitu yaende sambamba na maendeleo ya watu! Hakuna mfanyakazi atakayekubali kunyimwa haki zake za msingi mfano kupandishwa daraja kwa wakati, kisa eti unajenga barabara au kununua ndege!

Mbona wakati wa JK hizo barabara, madaraja, nk vyote hivyo vilijengwa kila kona ya nchi! Lakini bado ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu, haki za wafanyakazi na makundi mengine katika jamii ziliheshimiwa?

Iweje huyu mtu wenu aone barabara na ndege ni vitu vya muhimu sana kuliko haki za wengine? Mbona hatujawahi kumsikia akijipunguzia mshahara na posho zake?

Hata Rais angekua ni Lissu au Hashimu Rungwe, bado hizo barabara zingejengwa tu. Hilo ni moja ya jukumu la serikali yoyote ile duniani. Na kodi tunazolipa na mikopo ya ndani na nje ya nchi, hufanikisha zoezi hilo.
Vitu vingi vilikwama kukamilika watu walikuwa na pesa lakini huduma zilikuwa dini sana, na ndo maana chadema mliandamana kila siku kuwa pesa ya nchi inaibiwa na haifanya kazi na miradi haikamiliki kwa wakati na kwa kiwango sahihi.
Pia hao watumishi walipandishwa madaraja lakini walibaki ni madeni tu.
Na m
 
Back
Top Bottom