Tundu katika kuta za chini za moyo (ventricular septal defect)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
MOYO.png

VSD1.jpg

Makala ya leo ni muendelezo wa magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, na ugonjwa wa leo hujulikana kama Tundu katika moyo, au Tundu katika kuta za ventrikali za moyo, ni ugonjwa ambao hutokea mara nyingi zaidi.
Watoto wenye tundu dogo katika moyo, huweza kukua bila matatizo yoyote, wakati wale wenye tundu kubwa huanza kuonesha dalili mapema.
Vifuatavyo ni vihatarishi ambavyo vinaweza kupelekea kupata tundu katika kuta za chini za moyo

    • Maambukizi ya Rubella katika kipindi cha ujauzito
    • Ugonjwa wa kisukari ambao haujadhibitiwa kwa mama mjamzito
    • Matumizi ya pombe au madawa ya kulevya na baadhi ya dawa za hospitali katika kipindi cha ujauzito
Dalili

    • Rangi ya ngozi, midomo na kucha hubadilika na kuwa bluu
    • Kunyonya au kula kwa shida sana, na ukuaji wa shida
    • Kupumua kwa shida
    • Kuchoka haraka
    • Kujaa miguu na kuvimba tumbo
    • Mapigo ya moyo ya haraka
    • Kwa mtaalamu anaweza kusikia ishara ya ongezeko la sauti ya ziada ya mapigo ya moyo ya mtoto hali ambayo wataalamu huiita holosystolic murmur kwa kutumia kifaa kitaalamu stethoscope
Madhara ambayo yanaweza kutokana na Tundu katika kuta za chini za moyo

    • VSD2_(1).jpg
      Eisenmenger syndrome:
      Ni hali inayotokea wakati shanti ya damu kutoka kushoto kwenda kulia inayotokana na tundu katika kuta za moyo huongeza mtiririko wa damu katika mishipa ya kwenye mapafu na kusababisha shinikizo la damu katika mapafu. Hali hii husababisha kuongezeka kwa shinikizo katika upande wa kulia wa moyo, na kusababisha kubadilika kwa shanti kutoka kulia kwenda kushoto. Matokeo yake ni kuwa damu isiyo na oksijeni ambayo ilitakiwa kwenda kwenye mapafu kwa ajili ya kusafishwa, huchanganyika na damu yenye oksijeni iliyoko upande wa kushoto na kusambaa mwilini.
    • Kiharusi
    • Maambukizi katika kuta za ndani za moyo (endocarditis)
    • Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
Ujauzito na Tundu katika kuta za chini za moyo
Kwa akina mama ambao wamezaliwa na tatizo hili, ambao walitibiwa bila madhara yoyote wanaweza kushika ujauzito bila kupata madhara yoyote kipindi cha ujauzito. Isipokuwa, wale ambao hawakutibiwa au ambao wameshapata madhara, hushauriwa kutoshika ujauzito kwa sababu ya hatari zinazoweza kutokea kipindi cha ujauzito.
Vilevile kwa akina mama waliozaliwa na tatizo hili, uwezekano wa watoto wao kuzaliwa na tatizo hili huwa mkubwa. Kwa mujibu wa taarifa za taasisi ya moyo ya Marekani hatari ya kupata tatizo hili kwa mtoto huongezeka kwa kati ya asilimia 2 hadi 20 iwapo atazaliwa na mama mwenye ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao.
Vipimo

X-ray ya Kifua
ECG
Echocardiogram
Cardiac catheterization
Pulse Oximetry

Matibabu

Wengi wa wagonjwa wa tatizo hili huwa hawahitaji matibabu ya aina yeyote ile kwa vile tatizo hili hujirekebisha katika miaka ya mwanzo ya maisha yao. Hata hivyo kwa wale ambao watahitaji matibabu, hutibiwa kwa tiba au upasuaji kutegemea na ukubwa wa tatizo lenyewe.
    • Tiba huhusisha dawa zifuatazo:
      • ACEI’s ambazo hupunguza kazi ya moyo
      • Cardiac glycosides ambayo huongeza nguvu ya mapigo ya moyo
      • Diuretics ambazo pia hupunguza kazi ya moyo kwa kupunguza maji mwilini
    • Utaratibu wa kuziba tundu umegawanyika katika sehemu mbili, na hufanyika iwapo tundu ni kubwa sana, au tundu halikujirekebisha lenyewe wakati mtoto anapokua, au dawa alizopewa mgonjwa hazikusaidia.
 
VSD1.jpg

Makala ya leo ni muendelezo wa magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, na ugonjwa wa leo hujulikana kama Tundu katika moyo, au Tundu katika kuta za ventrikali za moyo, ni ugonjwa ambao hutokea mara nyingi zaidi.

Watoto wenye tundu dogo katika moyo, huweza kukua bila matatizo yoyote, wakati wale wenye tundu kubwa huanza kuonesha dalili mapema.
Vifuatavyo ni vihatarishi ambavyo vinaweza kupelekea kupata tundu katika kuta za chini za moyo

  • Maambukizi ya Rubella katika kipindi cha ujauzito
  • Ugonjwa wa kisukari ambao haujadhibitiwa kwa mama mjamzito
  • Matumizi ya pombe au madawa ya kulevya na baadhi ya dawa za hospitali katika kipindi cha ujauzito
Dalili

  • Rangi ya ngozi, midomo na kucha hubadilika na kuwa bluu
  • Kunyonya au kula kwa shida sana, na ukuaji wa shida
  • Kupumua kwa shida
  • Kuchoka haraka
  • Kujaa miguu na kuvimba tumbo
  • Mapigo ya moyo ya haraka
  • Kwa mtaalamu anaweza kusikia ishara ya ongezeko la sauti ya ziada ya mapigo ya moyo ya mtoto hali ambayo wataalamu huiita holosystolic murmur kwa kutumia kifaa kitaalamu stethoscope
Madhara ambayo yanaweza kutokana na Tundu katika kuta za chini za moyo

  • VSD2_(1).jpg
    Eisenmenger syndrome:
    Ni hali inayotokea wakati shanti ya damu kutoka kushoto kwenda kulia inayotokana na tundu katika kuta za moyo huongeza mtiririko wa damu katika mishipa ya kwenye mapafu na kusababisha shinikizo la damu katika mapafu. Hali hii husababisha kuongezeka kwa shinikizo katika upande wa kulia wa moyo, na kusababisha kubadilika kwa shanti kutoka kulia kwenda kushoto. Matokeo yake ni kuwa damu isiyo na oksijeni ambayo ilitakiwa kwenda kwenye mapafu kwa ajili ya kusafishwa, huchanganyika na damu yenye oksijeni iliyoko upande wa kushoto na kusambaa mwilini.
  • Kiharusi
  • Maambukizi katika kuta za ndani za moyo (endocarditis)
  • Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
Ujauzito na Tundu katika kuta za chini za moyo
Kwa akina mama ambao wamezaliwa na tatizo hili, ambao walitibiwa bila madhara yoyote wanaweza kushika ujauzito bila kupata madhara yoyote kipindi cha ujauzito. Isipokuwa, wale ambao hawakutibiwa au ambao wameshapata madhara, hushauriwa kutoshika ujauzito kwa sababu ya hatari zinazoweza kutokea kipindi cha ujauzito.
Vilevile kwa akina mama waliozaliwa na tatizo hili, uwezekano wa watoto wao kuzaliwa na tatizo hili huwa mkubwa. Kwa mujibu wa taarifa za taasisi ya moyo ya Marekani hatari ya kupata tatizo hili kwa mtoto huongezeka kwa kati ya asilimia 2 hadi 20 iwapo atazaliwa na mama mwenye ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao.
Vipimo

  • X-ray ya Kifua
  • ECG
  • Echocardiogram
  • Cardiac catheterization
  • Pulse Oximetry
Matibabu

  • Wengi wa wagonjwa wa tatizo hili huwa hawahitaji matibabu ya aina yeyote ile kwa vile tatizo hili hujirekebisha katika miaka ya mwanzo ya maisha yao. Hata hivyo kwa wale ambao watahitaji matibabu, hutibiwa kwa tiba au upasuaji kutegemea na ukubwa wa tatizo lenyewe.
  • Tiba huhusisha dawa zifuatazo:
    • ACEI’s ambazo hupunguza kazi ya moyo
    • Cardiac glycosides ambayo huongeza nguvu ya mapigo ya moyo
    • Diuretics ambazo pia hupunguza kazi ya moyo kwa kupunguza maji mwilini
  • Utaratibu wa kuziba tundu umegawanyika katika sehemu mbili, na hufanyika iwapo tundu ni kubwa sana, au tundu halikujirekebisha lenyewe wakati mtoto anapokua, au dawa alizopewa mgonjwa hazikusaidia.

Shukrani kwa shule iliyotukuka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom