Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Freeman mbooE vs kundu lissu wote cdm,
mbavu sana!!!
utaicheza tu pimbi wa lumumba
Screenshot_2019-01-26_190907.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thanks to a translator...bilashaka Lumumba sasa wameelewa vizuri mahojiano kati ya Lissu na Stephe. Kwa uelewa huo hatutasikia tena kiongozi wao polepole akisema Stephe ni mfuasi wao
 
Mkuu sasa hivi Tindu Lissu anajijenga ili agombee urais, hapa lazima apanuwe wigo zaidi, asijifungie kwenye professional yake tu atakuwa anaongea kama mwanasheria mbobezi sio mgombea urais mtarajiwa. Na wengi watamchukulia hivyo kwamba anajua sheria sana lakini hawezi kugombea urais.
Kwa sababu ameshajipambanua anaweza kugombea sasa aanze kujenga hoja za urais kama mambo mengine sio fani yake ndio anatakiwa aanze kutengeneza team ya washauri wake binafsi sio WA chama ili waanze kutengeneza mikakati na hoja.
Hii itamsaidia sana kuanza kuwavutia wananchi maana ana advantage ya kujulikana Kwa hiyo wananchi watamsikiliza kirahisi zaidi.
Pili, chadema wanatakiwa wabadili mbinu badala ya kupambana kisiasa Kwa kuponda yanayofanywa na CCM waanze kuja na sera zinazo ongelea ni nini watafanya kuendeleza pale CCM walipoishia, mfano shirika la Air Tanzania wamepata ndege mpya wenyewe waje na mikakati ya jinsi gani watalikuza zaidi Kwa kuboresha kuhakikisha linaongeza ndege zaidi, linaongeza safari za nje zaidi, linaendeshwa kibiashara zaidi bila kutegemea mkono wa rais, au sgr waseme ni jinsi gani wataboresha utendaji wake, wataongeza njia zaidi kwenda maeneo mengine.
Hii itawajenga zaidi kwa wananchi bila hata kukimbizana na virungu Kwa siasa za sasa hivi.
Mara nyingi vyama vya upinzani vinasema lazima vifiche sera zao zisije kuchukia na CCM, hayo mawazo waachane nayo, kwani wakisikika wao ndio wametoa wazo halafu CCM wakafanya then wataanza kuonekana wao ndio wanaoendesha gari na CCM wanafuata hapo wataanza kujijenga Kwa misingi.
Alibugi stepu pale alipomkosoa Mwalimu Nyerere tena ndani ya bunge maalum la katiba. Bado Mwalimu ni idol wa wanasiasa wengi kuanzia wazee waliomshuhudia akiwa hai mpaka vijana wanaoibuka miaka hii.
Sijawahi kumsikia akiongelea shida za waliompigia kura, siku zote yeye yupo kwenye mijadala ya kuponda serikali na sera zake.
Watu hawamfahamu kama mwanasiasa, wanamfahamu kama mwanasheria. Ndani ya muda huu uliobaki anao mtihani wa kuanza kuongea mambo ambayo watu hawajamzoea kumsikia akiyaongea.
 
Maana nijuavyo mimi Mtu ukipata janga au furaha fulani mwisho wa siku ukiulizwa ilivyotokea lazima ujibu.
Lissu aliita waandishi wa habari akasema kuna Gari namba fulani inanifuatiria kila niendako, napokea sms za vitisho kutoka namba fulani, siku ya tukio na tukio lilipotokea, Ni mchana akiwa anaelekea kula ndani ya nyumba za Seriali, ndani ya geti, ulinzi kwanini uliondolewa muda ule? anahoji na kafungu CCTV Camera? anaulizwa, anajiuliza pia na yeye, sasa kwanini tusimtafute aliye mpiga Risasi Lissu? tuachane na Lissu kulalamika kwake, kumjibu Serikali nzima hasa makada wa CCM, hamwoni mnajenga picha mpya.
 
Huyu alikuwa Mkosoaji, na anaendelea kuwa mkosoaji wa Serikali inayoongozwa na CCM, kwa mnayo yaongea mnatuaminisha kuna kitu nyuma yake,

1)Serikali yenu imemnyika matibabu
2)Kuna makada wa CCM anajivika utetezi wa Serikali

Kuna mambo mengi ya kufikirisha kuweni makini, ikiwezekana zuieni hiyo tabia, kauli zinatofautiana sana katika kutetea tafuteni mtu makini wa kudili na hili sio jambo dogo, nchi inachafuka sana,
 
huyu alikuwa Mkosoaji, na anaendelea kuwa mkosoaji wa Serikali inayoongozwa na CCM, kwa mnayo yaongea mnatuaminisha kuna kitu nyuma yake,

1)Serikali yenu imemnyika matibabu
2)kuna makada wa CCM anajivika utetezi wa Serikali

kuna mambo mengi ya kufikirisha kuweni makini, ikiwezekana zuieni hiyo tabia, kauli zinatofautiana sana katika kutetea tafuteni mtu makini wa kudili na hili sio jambo dogo, nchi inachafuka sana,
unakikumbuka kisa cha Mnara wa Babeli ?
 
Hiyo busara wameondoka nayo akina comred kinana!
Hawa akina Bashiru Na pole pole watupu sana
 
Walitegemea nae atanyamaza kama kina Kibada, Mkatoliki Roma, au Dr Ulimboka na MO sasa. Ajabu ndio wanazidi kujivua nguo jana mwingine kavua huko Dom. Kumbe Kipenzi cha Watanzania Sokoine Edward Moringe mtu ya Monduli juu aliuawa sio kama tulivuoaminishwa miaka yote/ama kupigwa risasi Tundu Lisu mchana akiwa maeneo yanayolindwa na Polisi wenye bunduki lakini wanaondoka ili kuwapisha wauaji, na baada ya tukio tung'oe CCTV camera, uchunguzi hakuna, marufuku kumwombea, na marufuku kumlipia matibabu eti NI AJALI KAMA ajali nyingine. Hii inapotoka kwa Mhadhiri wa chuo kikuu Bora kabisa katika ukanda huu tena chenye history ya kuwapika wasomi Bora kabisa Africa na Dunia, huwezi kupinga. Maana unajua anachokisema na anauhakika kumbuka pia ni kiongozi mkubwa wa chama dola so yuko well informed. Pole Lisu kwa ajali/pole Sokoine na family kwa assassination
 
Tujiulize aliyempiga risasi yuko wap?
J e kwa nini wenye mamlaka hawashuguliki na aliyempiga risasi?
Je mwajiri wake amefanya nini kusaidia maisha ya mtumishi wake?
je serikali imemhakikishia vip usalama wake vip atakaporejea?
 
Tujiulize aliyempiga risasi yuko wap?
J e kwa nini wenye mamlaka hawashuguliki na aliyempiga risasi?
Je mwajiri wake amefanya nini kusaidia maisha ya mtumishi wake?
je serikali imemhakikishia vip usalama wake vip atakaporejea?
Walio pamoja na wauaji, waonevu, watumia vibaya mamlaka hawako na Mungu na walichonacho ni siku na sio "future". Tupo hapa kushuhudia anguko la shetani n ushetani. Hii ya Lissu Itakua case study
 
Siyo kila kitu hujibiwa.
Wakati mwingine kujibu kunadhihirisha ujinga na hata upumbavu.
Mtu mwenye akili nzuri haongelei kila jambo.
 
Wanabodi, mimi nilidhani Lissu hatarejea
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, "Kwa Mliomsikia Tundu Lissu Kwenye Hard Talk, Jee Unadhani Atarejea Nchini?. Mimi kwa upande wangu, I seriously doubt kama atarejea, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa mwenye uthubutu na ushujaa mkubwa kuliko hata ushujaa wa Nelson Mandela!.

Nimesema hivyo kwa sababu nimemsiliza kwa makini Tundu Lissu, him being a Lawyer, kwa yale aliyoyasema, kwa tuhuma alizoshusha bila ushahidi, I seriously doubt if Tundu Lissu will ever return home during this era, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa kuliko Nelson Mandela.
Hongera zake.

Paskali
Final Update
Tundu Lissu leo amerejea nyumbani Tanzania, hivyo naomba kuthibitisha humu kuwa Tundu Lissu ni Jasiri na Shujaa Kuliko Nelson Mandela.

Hivyo sasa, kufuatia kurejea huku, ule ushauri wangu nilioutoa kwake kabla hajashambuliwa, sasa utekelezwe.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Shujaa Kamanda Tundu Lissu, karibu nyumbani.
Mungu ni mwema amekutendea muujiza, hivyo endelea kutimiza ndoto yako, Mungu aliyekuponya ni Mungu mwenye uwezo, anaweza kabisa kulifanya "Jiwe Walilolikataa Waashi, Likafanywa Jiwe Kuu la Pembeni"

I wish him all the best.
Paskali
 
Back
Top Bottom