Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Sheria haingalii hilo. Tatizo mnatanguliza sana feelings badala ya reality. Hakuna aliyesema atakufa njaa, lakini aache kulalamika kwa vitu ambavyo viko wazi kabisa. Nyie na mtu wenu bado hamuelewani kabisa
Kwanini mnateseka si mumuache afanye yake,kwani nyie mnaathirika nini? mwacheni aeleze yaliyomtokea,mbona pole pole naye anafanya mahojiano vyombo kibao vya habari? Lissu yupo nje kwa matibabu sasa mlitaka afanya mahojiano na ITV?
 
Swali, jee kwenye hilo la mipango ya kutaka kumuondoa kwenye ubunge, kuna ushirikiano wowote baina ya serekali na baadhi ya viongozi wa Chadema, baada ya Lissu kutangaza nia yake ya kugombea Uraisi kupitia chama chake?

Anything is possible in politics

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali, jee kwenye hilo la mipango ya kutaka kumuondoa kwenye ubunge, kuna ushirikiano wowote baina ya serekali na baadhi ya viongozi wa Chadema, baada ya Lissu kutangaza nia yake ya kugombea Uraisi kupitia chama chake?

Anything is possible in politics

Sent using Jamii Forums mobile app

Viongozi wa CHADEMA wa nini? Yeye TAL atajivua Ubunge mwenyewe kwa mujibu wa sheria. Labda viongozi hao wawe wamemlaghai baada ya kuona ameanza kuwa threat ndani ya chama.
 
Mh. Tundu Lissu kwanza napenda nikupe pole kwa yote yaliyokukuta na kukutakia heri katika matibabu yako ya mwisho mwisho kabla ya kurejea nyumbani. Nijikite kwenye mada husika. Kwa sasa toka umeanza kutembea huko nchi za nje na kuanza kuongea na marafiki kuhusu shambulio lililokuacha na kilema cha maisha, kumetokea kelele nyingi na vitisho na hata upotoshaji kwamba unaichafua nchi kwa kuongea na marafiki. Napenda nikutie moyo, usiwe na hofu na hizi kelele kwani wanaopiga kelele ni wale wale walioona ni sawa kwa yaliyokukuta na wengine hawakuwa tayari hata kuona unapata matibabu stahiki kutokana na nafasi yako. Nina hakika hakuna mahali popote uliposema umeshambuliwa na watanzania bali watu wenye nia ovu, ambao hawakutaka wewe uendelee kuishi kwa sababu wanazozijua wao. Hatuna shaka na uzalendo wako na wala hatusubiri wao watuambie nani ni mzalendo na yupi sio, kwani ndani ya miaka hii 20 iliyopita wazalendo wa kweli na walinda vyeo tunawafahamu.

Wote tuna uelewa wa kutosha na tunajua kwamba unaongea na marafiki na ni haki yako kufanya hivyo popote ndani ya dunia hii. Hao wazungu inaoonekana ni nong’wa wewe kuongea nao wote wana mahusiano mazuri na nchi yetu na wana miradi mbalimbali hapa nchini. Iweje ukiongea nao wewe ndio iwe kosa? Je ni kosa wewe kutafuta marafiki toka nje? Spika huyu anayejifanya anakuita leo yeye ndio kajificha nyumba ya sheria ili usipate matibabu. Nitashangaa sana kama utatii amri yake ya kurudi nyumbani bila kumaliza matibabu na ratiba zako, kwani hana nia njema na wewe na hofu yake ni wewe kupata marafiki toka nje. Iwapo alishindwa hata kuja kukutembelea ukiwa kwenye matibabu, iweje leo ageuke kukupangia ni lini urejee? Anakutisha kwamba usiporudi hutakuwa mbunge, kwani ungefariki baada ya shambulio ungekuwa mbunge? Ubunge ni nini mbele ya uhai wako? Je anadhani wewe umepanga kuwa mbunge wa maisha mpaka uogope kuukosa huo ubunge? Yeye ndio anapaswa kuutetemekea huo uspika maana anaweza kupata matibabu yoyote ayatakayo dunia hii na kwa muda wowote. Wewe hujatibiwa na hela ya bunge, hivyo ni kama umeshatolewa kwenye huo ubunge, na iwapo atakutoa itakuwa ni marudio tu. Wanajificha eti uje kuwatetea wananchi wa jimbo lako, ni kweli, lakini kodi mpaka leo wananchi wa jimbo lako wanalipa, kuna madiwani nk hao wanatosha kusimamia maendeleo ya hao watu wako. Asikutishe mtu kuhusu wewe kuongea na mzungu maana wao hawana hati miliki ya kuongea na wazungu, kwani wamejaa hapa nchini.

Sasa hivi nia yako ni kugombea urais, jitahidi kutafuta marafiki huko nje ili ukiwa rais uwe na marafiki wengi utakaoshirikiano nao ili kuleta maendeleo ndani ya nchi hii. Angalizo muhimu, asikudanganye mtu, kwa mwenendo wa uchaguzi ulivyo hapa nyumbani, sioni wewe kutangazwa kuwa mshindi bila msaada wa hao marafiki wa huko ulaya kwani wote tumejionea jinsi box la kura lisivyoheshimiwa. Kumbuka washindani wako wanategemea vyombo vya dola na tume ya uchaguzi kushinda. Hivyo na wewe usipopata marafiki wenye nguvu, unaweza kushinda usitangazwe, lakini kwa msaada wa hao marafiki na nguvu yetu wananchi haki itatendeka hata kwa shingo upande.
Ombi langu kwako, kuwa mzalendo kwa nchi na sio kwa serekali, waeleze hao marafiki fursa zilizopo hapa nchini kama madini, lakini ushirikiano uwe ni win win situation, wahimize waje kutalii hapa nchini kwani tuna vivutio vingi vya utalii. Waambie tunahitaji wawekezaji na ukiingia madarakani utawawekea mazingira mazuri ya wao kuja kuwekeza ili vijana wapate ajira.
 
Haijapata kutokea katika historia, na yumkini haitakuja kutokea ulimwenguni mtu aina ya Tundu Antiphas Mugwai Lissu.

Ni mbunge machachari kutoka Singida Mashariki na mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani Tanzania (chief whip) kupitia Chadema. Iliwahi kusikika kwamba rais na mwenyekiti wa chama cha ccm alionya chama chake kwamba ni kheri wapoteze nafasi ya urais kwa wapinzani kuliko kuruhusu Tundu Lissu atinge bungeni kwenye uchaguzi wa mwaka 2005.

Ni wakili mashuhuri ambaye ameweka historia iliyotukuka ya kuwanasua raia na wasio raia kwa kuwawakilisha mahakamani hasa wanapobambikiziwa kesi au wanaposhitakiwa kwa sheria kandamizi., na mara zote ameigaragaza Jamhuri katika mashauri hayo.

Ni mpinzani mkuu wa rais Magufuli kwa mujibu wa duru za siasa. Katika kipindi cha miaka 2 tu ya utawala awamu ya 5, Lissu ameshtakiwa zaidi ya mara 9 kwa uchochezi. Ndiye mwanasiasa pekee ambaye maagizo na matamko ya rais Magufuli hayamhusu.

Alinusurika katika jaribio lililoshindwa la kumuua hata baada ya kumiminiwa mwilini risasi zaidi ya 40 akiwa Bungeni, Dodoma. Ni mahututi ambaye alijitibu mwenyewe mpaka sasa anasimama kwa miguu yake, licha ya Bunge na Serikali kumsusa na kumuwekea mizengwe ya matibabu.

Anatajwa mitandaoni kuwa mtu mwenye ushawishi zaidi na ameshakiri kuwa tayari kupeperusha bendera ya UKAWA katika uchaguzi mkuu wa kung'oa utawala wa Magufuli 2020.
Tundu_A._Lissu_.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom