johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,820
- 141,722
Nimemuona Tundu Lisu akiwa pale London Uingereza Ameonekana ni mtu mwenye bashasha, mwenye matumaini na spirit ya kutokata tamaa.
Nikawakumbuka wabunge wenzake bila kujali itikadi na hata baadhi ya watendaji waliopigania uzima wake pamoja naye na kwa uchache nimewakumbuka Mbowe, mchungaji Msigwa, Lema, Dr Mwigulu, Dr Mpoki na Lazaro.
Nikawakumbuka pia waliovuka mpaka wa nchi kwenda kumjulia hali pale Nairobi katika hali ya ubinadamu kabisa, mama yetu Samia ambaye ni makamo wa Rais, balozi Pindi Chana na mzee wetu ambaye ni baba wa demokrasia nchini Ally Hassan Mwinyi.
Ninaendelea kutafakari maana hadi hapo sijaona ule uimara thabiti wa mhimili wa bunge. Kwa mfano mtu akisema Lisu alitelekezwa na bunge atakuwa amekosea?..........na kama hajakosea bunge imara linaweza kumtelekeza mbunge wake kwa sababu yoyote ile akiwa katika hali ya umahututi?
Sisi sote ni ndugu, niishie hapo.
Maendeleo hayana vyama!