Tunda la mzeituni

Asante kidogo nimeelewa sema tu walitumia neno tunda kupunguza makali ila kiuhalisia ni ngono
Hapana maana baada ya kula tunda ndiyo adam na eva wakajijua kuwa wako uchi, so haihusiani na tunda la ngono, kama ni tunda la ngono basi wangeshakua wanajijua wapo uchi na wakatamaniana wakalana
 
Kidogo unaeleza vzur
Sema pia umelalia hoja moja yani umeleta mada lakini tayari kichwani una majibu yako, usilalie kwenye hoja kuwa ni tunda la ngono tu, kuna ufafanuzi mzuri umepita huko juu lakini umekataa kukubali, hao watu Adamu na Eva hawakujijua kama wapo uchi ni baada ya kula tunda lile, je walitamaniana vipi wakati walikua hawajui kama kuna uchi
 
Mkuu kitu cha kwanza unachohitaji kujua ni Adamu hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa hapa duniani, jambo hili limechukuliwa kimakosa na watu wengi sana kwamba Adam alikuwa ni mtu wa kwanza kuumbwa.

Pia unatakiwa ujue kwamba sio kila andiko la Biblia au vitabu vitakatifu kama Qur'an laweza kuchukuliwa kama lilivyo (literally) , kuhusu tunda alilokula Adam haina maana ni tunda la dhahiri kama pera, chungwa nk, la hasha. Tunda katika lugha ya kiroho ni matokeo yatokanayo na matendo ya mtu, mfano mtu mwema huzaa matendo mema na mtu mbaya huzaa matendo mabaya, hivyo mti ni sawa na mtu na matunda ni sawa na matendo, hivyo Adam alikatazwa na Mungu kushiriki matendo mabaya ya watu wabaya wa zama hizo, kumbuka Adam hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa bali yeye alikuwa mtu wa kwanza kuwasiliana na Mungu na watu wengine waliomzunguka katika jamii aliyokuwa anaishi wengi wao walikuwa waovu kama Ibilisi.

Hebu tusome jinsi Nabii Yesu (as), bingwa wa kauli za mifano, anavyojenga hoja ya mti na matunda na mwisho akatoa ufafanuzi wake; katika (Luka 6:43-45) Yesu anasema:-

Mti mzuri hauzai matunda mabaya wala mti mbaya hauzai matunda mema, kwakuwa kila mti hujulikana kwa matunda yake, kwakuwa watu hawavuni matini kutoka kwenye miba wala hawavuni zabibu kutoka kwenye-----.

Hapo sasa utaona Yesu kafafanua nini maana ya mti na matunda.
Adamu hakuwa mtu wa kwanza nawe ndiyo umepotoka mzee, kivipi Adamu na Eva hawakuwa sio watu wa kwanza, wakati Mungu alipomuumba Adamu akasema ninaona nikulete msaadizi ambapo Eva alitoka ubavuni mwa Adamu, au unataka kuniambia Eva uzao wake ulitoka wapi
 
Mkuu sio hatutaki kufa ujue nini,


Kuna vitu lazima uvijue ungali hao walau hata nusu uelewa.

Tunapokuwa watoto tunapata mafunzo mengi ambapo ukikua hayabanduki akilini.

Sasa basi no vema ushakua uchambue mojamoja walau.

Mifano kuna ile cinema ya yesu. Watoto wengi wanajua yule ndie halisi lkn sio Bali ni muigizaji tu.

Nazani hata wewe mafunzo ya Adam na hawa uliyasikia hivo si vibaya kuyajua kiundani.
Kuna walokole husema nilikuwa katikati ya maombi nikatokewa na Yesu,muulize Sasa Ni Yesu yupi eti was kwenyevcinema😅
 
Zeituni sio tunda walilokula Adam na Eva. Na isitoshe, halikuwa na jina zaidi ya " Tunda la Mtu uliokuwa katikati ya bustani ya Eden". Acha kupotosha. Maandiko Matakatifu.
Ni kweli kuna upotoshaji Kwenye hili, watu wana weka akili yao tu juu ya ngono
 
Katika Ulimwengu wa kiroho kuna kuchagua na uamuzi unakuwa wa kwako. Maisha unavyoishi unafungua milango mbalimbali unafanya maamuzi wewe kama wewe . Adhabu unayosema ni mtazamo, tulichagua (physical body) maisha ya kimwili yenye mahitaji na hisia na pia inazeeka na kufa, Ndio maana cha kwanza Adam na Eva waligundua wako uchi, wakajifunika. Pia wakaona aibu kwa hali ya kimwili wakajificha waliposikia sauti ya Mungu.
OK Maelezo yangu nimesema walikula tunda la mzeitun ila ukanikatalia ukasema tunda linawakilisha utii,

Mfano umemwambia mwanao usidokoe nyama akadokoa na ukamdaba bahati mbaya bado ilikuwa mdomoni na mdomo umemvimba bila aibu anainamainama wewe Mzazi ukaamua umuadhibu kwa kisa la kutoa kutii, mile ulichomkataza.

Sasa basi na Mimi napenda unifafanulie vizuri KOSA lililowafanya kuvunja utii (tunda) kwa Adam na hawa.
 
Hapana maana baada ya kula tunda ndiyo adam na eva wakajijua kuwa wako uchi, so haihusiani na tunda la ngono, kama ni tunda la ngono basi wangeshakua wanajijua wapo uchi na wakatamaniana wakalana
Asante
 
Tunda hili navyosikia ndio tunda walilokula Adam na Hawa na ndio hilihili Mungu aliwakataza wasile.

Kama ni Kweli hilo ndio tunda lenyewe naomba nielezee kidogo na kama sitakuwa sahihi mnisahihishe.

Kwanijuavyo ni kuwa maana ya lile tunda walilokatazwa ni kutokufanyana, kwa bahati mbaya wakafanyana na Mungu akawaambia mtazaa kwa uchungu nawe mwanaume mtakula kwa jasho ndio ukawa mwanzo wa kuzaliana mpaka leo kisa tunda (utamu)

Jiulize maswali fikirishi acha kusoma BIblia kama kasuku. Kama halikuwa tunda halisi kwa nini Biblia isiandike hivyo? Ona kwamba Biblia inasema Adam akamjua mkewe, wakazaa mtoto. Kwa nini isiseme Adam akamla tunda mkewe wakazaa? Kwa nini Biblia iseme Shekemu akambaka na kumbikiri Dina na ishindwe kusema Adamu akambikiri Hawa au angalau kusema akalala nae, na mwandishi wa hivyo visa ni huyohuyo Musa?

Pili, Hawa alianza kula tunda Adamu akiwa hayupo. Kwa hiyo hawa alifanya ngono na nani sasa, na nyoka? Au alijifanya mwenyewe?

Tatu, amri ya kutokula tunda ilitolewa kwa Adam kabla Hawa hajaumbwa. Kwa hiyo Adamu alikuwa akikatazwa kufanya ngono na nani kabla Hawa hajaumbwa?

Nne, Adam na Hawa wamekula tunda baada ya kuambiwa wazae na kuongezeka. Sasa unamhukumuje mtu uliyemwambia azae kwa kufanya ngoono? Au unatarajia walitakiwa wazae kwa binary fission kama amoeba wa form one?

Kwa hiyo acha story za mitaani sijui tunda ni ngono, sijui ni tende, sijui zeituni, ujinga mtupu. Na kama umeambiwa walifanya ngono kanisani au msikitini kwako basi sasa uelewe unafundishwa uongo.
 
Adamu hakuwa mtu wa kwanza nawe ndiyo umepotoka mzee, kivipi Adamu na Eva hawakuwa sio watu wa kwanza, wakati Mungu alipomuumba Adamu akasema ninaona nikulete msaadizi ambapo Eva alitoka ubavuni mwa Adamu, au unataka kuniambia Eva uzao wake ulitoka wapi


Adam hakuwa mtu wa kwanza KUUMBWA, yeye alikuwa mtu wa kwanza kuongea na Mungu, alikuwa mtu wa kwanza kupewa ufunuo wa kiroho kuwapelekea watu wake katika zama hizo, kifupi Adam alikuwa ndiye mtu wa kwanza kuonyesha njia ya kufuatwa na watu kumuelekea Mungu hivyo unaweza kusema Adam alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa kiroho.

Eva kutoka ubavuni kwa Adamu; hilo ni tamathali ya kiroho, kama katika elimu mbalimbali tunaweza kuona lugha za elimu hizo zikitumika ndivyo hivyohivyo katika dini pia kuna lugha zake, sio kila andiko katika dini huwa linatafsiriwa "moja kwa moja" (literally) kuna baadhi ya maneno ukiyatafsiri kwa njia hiyo utapata maana za hivyo zisizoingia hata kwenye akili ya mwendawazimu, mfano katika Injili Yesu kajiita mzabibu!!!, je ni kweli yeye ni mzabibu??!, hapo ni lazima tutafute tafsiri ya mzabibu kiroho.

Inaposemwa kwamba Eva (Hawa) alitoka ubavuni mwa Adamu maana yake ni kwamba tabia za Eva zililandana na Adam kiasi kwamba kwa kuoana wangeweza kuenenda pamoja katika hali nyingi, hiyo lugha ni sawa na neno la kiingereza linalosema; "We are made out of the same wood" maneno hayo kwa maana ya literally ni:- sisi tumetengenezwa kutoka katika ubao mmoja, tafsiri yake ni :- Sisi tuna sifa na tabia zinazofanana.

Unaposema kwa maana ya mojakws moja kwamba Eva alitoka ubavuni kwa Adamu maana yake ni sawa na kusema Eva alizaliwa na Adam na kisha akaolewa naye!!!, je Adam alioa mwanaye??, kama hakuoa mwanaye, je alioa kiungo chake??, hayo ni maswali ambayo hayana majibu, hivyo dhana ya Eva kutoka ubavuni kwa Adamu haina maana ya moja kwa moja isipokuwa maana yake ndiyo hiyo niliyoieleza hapo juu.

Adamu aliishi takriban miaka 6,000 iliyopita lakini dunia hii ina umri wa bilions ya miaka na watu wa kale waliishi milions ya miaka kabla ya Adamu, sasa huwezi sema kwamba Adam ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuumbwa, juu ya yote Biblia imetaja juu ya kisa cha kaini na Habili, kaini akamuua Habili na kisha akatorokea katika nchi ya Nod na huko akaoa, sasa jiulize huko alioa mtu au jini bila shaka alioa mtu, je huyo mtu alitokea wapi wakati kipindi hicho walikuwepo watu watatu tu duniani???.

Adamu hawezi kuwa mtu wa kwanza kuumbwa.
 
Adamu aliishi takriban miaka 6,000 iliyopita lakini dunia hii ina umri wa bilions ya miaka na watu wa kale waliishi milions ya miaka kabla ya Adamu, sasa huwezi sema kwamba Adam ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuumbwa, juu ya yote Biblia imetaja juu ya kisa cha kaini na Habili, kaini akamuua Habili na kisha akatorokea katika nchi ya Nod na huko akaoa, sasa jiulize huko alioa mtu au jini bila shaka alioa mtu, je huyo mtu alitokea wapi wakati kipindi hicho walikuwepo watu watatu tu duniani???.

Adamu hawezi kuwa mtu wa kwanza kuumbwa.
Mwanzoni Mungu aliruhusu watu waoe dada zao, hivyo Kaini alioa dada yake. Ili kuendeleza uzao, ilibidi Lot azae na watoto wake, na wakati huo haikuwa big deal, Mungu aliruhusu.

Sasa jiulize: Kaini alipooa alikuwa na umri gani?

Kumbuka kwamba Biblia huwa haiongelei watoto wa kike, unaweza kuona ni ubaguzi lakini it is what it is. Hivyo Biblia haiongelei watoto wa kike ambao Adam na Eva walizaa, ambao ni wazi walitawanyika kwenda sehemu nyingine, pamoja na huko nchi ya Nod. Na huenda walishatawanyika miaka mingi labda hata 100, wakati Kaini alipowafuata dada zake huko waliko ili aoe mmoja wao. Hivyo si ajabu Adamu alioa akiwa na zaidi ya miaka 100, wakati labda ana dada zaidi ya 50 waliotawanyika sehemu mbalimbali

Kama unaamini kwamba Mungu aliumba mtu kwa mara ya kwanza aliposema na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa nini huamini mtu huyo alikuwa Adam kama Biblia inavyosema? Na kama Mungu alikuwa ameshaumba watu, kwa nini aseme na tufanye mtu kwa mfano wetu kama vile ndio anafanya kwa mara ya kwanza, na hata kuona ni mpweke kwa kutokuwa na mwenzi, na kumuumba Eva, ikiwa tayari kulikuwa na watu wengine sehemu fulani?

Yaani angalia isivyo na lojiki; Mungu aumbe watu zaidi ya Adam, halafu baada ya hapo aseme na tufanye mtu kwa mfano wetu, na kuumba mtu na kumuweka mbali na wengine aliokwisha waumba, kisha aone huyo mtu mwingine aliyemuumba mbali na wengine, Adam, ni mpweke, badala ya kumpeleka kule waliko watu wengine aliowaumba anaamua kuumba tena, Eva. I say, Biblia sio kitabu kigumu kiasi hicho, ni uwezo wa kutafakari mambo tu.
 
Na huenda walishatawanyika miaka mingi labda hata 100, wakati Kaini alipowafuata dada zake huko waliko ili aoe mmoja wao. Hivyo si ajabu Adamu alioa akiwa na zaidi ya miaka 100, wakati labda ana dada zaidi ya 50 waliotawanyika sehemu mbalimbal


Hadithi yako imejaa maneno haya ya kufikirika; labda, huenda, pengine, nk.

Katika habari ukishaingiza dhana basi hadithi nzima inabeba dhana ya kufikirika.

Unaposema kaini huenda alioa dada yake, nikuulize kwanini leo mtu kuoa dada yake imekatazwa???
 
OK Maelezo yangu nimesema walikula tunda la mzeitun ila ukanikatalia ukasema tunda linawakilisha utii,

Mfano umemwambia mwanao usidokoe nyama akadokoa na ukamdaba bahati mbaya bado ilikuwa mdomoni na mdomo umemvimba bila aibu anainamainama wewe Mzazi ukaamua umuadhibu kwa kisa la kutoa kutii, mile ulichomkataza.

Sasa basi na Mimi napenda unifafanulie vizuri KOSA lililowafanya kuvunja utii (tunda) kwa Adam na hawa.
Voda wakikuambia ili ujiunge na kifurushi basi bonyeza *. ...# usipofanya hivyo basi airtime itatumika kwa gharama kubwa zaidi lakini bado kuna watu wanalalamika wameonewa. Tunda lilisimama badala ya choice kwamba ukichagua hii basi kitakachofuata ni hivi . Kutii ni kuheshimu unachoambiwa.
 
Back
Top Bottom