Tunaye fisadi mzalendo? Rai 02.01.09 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaye fisadi mzalendo? Rai 02.01.09

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamuzu, Jan 10, 2009.

 1. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Tunaye fisadi mzalendo?
  Na Msiba Pakia

  Kufuatia makala yangu katika gazeti hili toleo la juma lililopita niliyosema kwamba “kweli ili CCM iimarike inabidi ivunjike”, yamejitokeza maoni mbalimbali kutoka kwa wasomaji yanayoniunga mkono na mengine yakikosoa mtizamo wangu.

  Wapo ambao wanaonekana wameikinai CCM kiasi cha kuiombea itoweke kabisa na wala siyo kuvunjika ili iimarike. Pia wapo wanaoendeleza kaulimbiu ya kidumu Chama cha Mapinduzi, ingawa hawa wanaonekana kuzubaishwa sana na mazoea.

  Vilevile katika makala yangu hiyo nilionyesha kutokuwa na uhakika kama ufisadi unaojionyesha ndani ya CCM unatokana na ukosefu wa uzalendo. Watangulizi wangu katika mjadala huo, Ayub Rioba na Muhingo Rweyemamu, walionyesha kwamba uzalendo na ufisadi ni vitu viwili visivyokuwa na mkabala mwema, kwa maana ya kwamba fisadi hawezi kuwa mzalendo na mzalendo hawezi kuwa fisadi.

  Katika mawazo yangu kuna picha iliyokuwa inahoji kwamba fisadi hawezi kuwa mzalendo? Kwa mtizamo wangu naona wapo watu wanaoonyesha uzalendo, kwa maana ya kuipenda nchi yao, lakini wakiwa na viashiria vyote vya ufisadi. Pia wapo watu wasioonyesha moyo wa uzalendo lakini wakipimwa kwa vigezo vya ufisadi wanaonekana bado wametakata, bila kuonyesha dalili zozote za kuchafuliwa na viini vya ufisadi. Hilo ndilo ningetaka kulijadili kwa leo.

  Msomaji mmoja alinitumia ujumbe mfupi kwenye simu ya mkononi akisema kwamba “katu mzalendo hawezi kuwa fisadi”. Akasema kwamba kwake yeye uzalendo ni utakatifu wa kisiasa. Eti mtakatifu hana dhambi, kwamba ufisadi ni dhambi sababu ni usaliti kwa wananchi. Akaongeza kwamba mtakatifu akitenda dhambi anakuwa amepoteza sifa za utakatifu, hivyo na ufisadi unampotezea mtu sifa za uzalendo.

  Kwa kiasi kikubwa nakubaliana na mtizamo wa msomaji huyo, ila bado siamini kwamba wote wanaoonyesha tabia ya ufisadi wanakuwa wamepoteza uzalendo wao kwa maana ya kutoipenda nchi yao. Mimi nadhani hiyo si sahihi.

  Sababu kama nilivyoeleza kwenye makala yangu ya juma lililopita ufisadi ni tabia kama zilivyo tabia nyingine kama vile ulevi, ugomvi na kadhalika. Kama tabia hizi nyingine haziwaondolei watu haki yao ya uzalendo kwa nini ufisadi uwe tofauti na tabia hizi nyingine chafu?

  Naomba nieleweke kwamba mimi siutetei ufisadi hata kidogo, ila naangalia haki yao wale wanaobainika kuwa mafisadi ya kwamba tabia yao hiyo inatosha kuwavua uzalendo wao. Tunaweza kuangalia tabia za watu wanaoonekana ni mafisadi kisha tuzilinganishe na za wale wasiokuwa mafisadi ili tuweze kupata ukweli wa nani anapaswa kuonekana mzalendo na ni yupi anausaliti uzalendo.

  Tuchukulie mfano wa fisadi mmoja anayekwapua mamilioni ya fedha kutoka kwenye taasisi fulani ya serikali na kuamua kufungua kiwanda. Anaajiri watu, watu wanapata ajira, analipa kodi na kuzalisha bidhaa zinazotumiwa na wananchi na nyingine kupelekwa kwenye soko la nje ya nchi kwa ajili ya kuliletea taifa hela ya kigeni. Huyu mtu ni fisadi, mtaji wake kaupata kwa njia za ufisadi. Hivi kweli ni haki kusema kwamba mtu wa aina hii si mzalendo kwa vile mtaji wake kaupata kwa njia za ufisadi?

  Kwangu mimi mtu wa aina hiyo, ndiyo ni fisadi, lakini ni fisadi mzalendo. Ni mtu anayetumia kile alichokipata kwa njia za ufisadi kwa ajili ya kuboresha ustawi wa nchi yake na wa wananchi wenzake. Huyu ni fisadi mzalendo.
  Tuchukulie mfano mwingine wa mtu aliyepata nafasi ya kusomea ughaibuni kisha akapata nafasi ya kuajiriwa katika asasi mojawapo ya kimataifa.

  Mtu huyo si fisadi hata kidogo kwa vile nafasi ya masomo anakuwa ameipata kutokana na uwezo wa akili zake, pale hakuna kitu chochote cha ufisadi.

  Vilevile kazi anakuwa ameipata kwa uwezo wa akili zake. Lakini baada ya kuajiriwa anaamua kuchukua uraia wa nchi ya ughaibuni anakofanyia kazi. Uraia wa kule ughaibuni unakuwa mtamu kuliko uraia wake wa asili wa nchi yake. Sasa mtu wa aina hiyo tunaweza kumuita mzalendo kwa vile siyo fisadi?

  Vilevile wapo watu hapa nchini ambao uzalendo wao hautiliwi shaka hata kidogo kutokana na kauli zao katika utendaji kazi wao kitaifa pamoja na hamasa wanazozifanya kwa wananchi ili kuuenzi uzalendo wa nchi yao, lakini wakati huo huo matendo yao yakiwa yanawasuta kwa kuonyesha kila dalili za ufisadi.

  Mfano miaka kadhaa iliyopita nilifika nyumbani kwa mwanasiasa mmoja mkongwe, mwanasiasa niliyekuwa nikiamini ni mjamaa wa kutupwa ambaye mpaka sasa ni kati ya wanasiasa wanaoaminika kwa uzalendo wao. Kusema ukweli sikuamini macho yangu kwa kile nilichokiona nyumbani kwa mtu huyo anayejulikana mitaani kama komredi kutokana na kuonekana alivyozikumbatia falsafa za Kimaxist, yaani anayejionyesha ni muumini mzuri wa ukomunisiti.

  Wakati ule chama tawala kikiwa bado kimeshika hatamu barabara na mwanasiasa huyo akiwa anashikilia moja ya nafasi nyeti ndani ya chama. Nilishangaa kukuta magari yasiyopungua kumi yote yakiwa na namba za CCM, kwa wakati ule, yakiwa yapo kwa ajili ya kuhudumia familia ya kigogo huyo mkomunisiti wa CCM. Yalikuwepo magari yaliyokuwa yamepangwa kwenda shamba, mengine yakisubiri kuwarudisha wageni waliokwenda kutembea pale makwao, na moja likiwa linatumiwa na mtoto wa kigogo huyo kufanya matayarisho ya mandari (pikiniki) kwa kuwazungukia marafiki zake.

  Huyo ni kigogo aliyekuwa na bado anahubiri watu kuachana na vitu vya anasa kama vile kumiliki magari na vitu vya aina hiyo. Yeye anaona kumiliki gari la kwake ni anasa ila kutumia utitiri wa magari yanayohudumiwa na walala hoi kwa ajili yake tu si anasa!

  Katika hali yoyote inayoweza kuelezeka ule ni ufisadi nilioukuta kwa kigogo yule mzalendo asilia. Hiyo ni mifano miwili, lakini ipo mingi ya aina hiyo inayodhihirisha kwamba uzalendo hauzuii ufisadi na wala ufisadi haumuondolei mtu uzalendo au mtu asiyekuwa fisadi kulazimika kuonekana mzalendo.

  Kwa maana hiyo nashindwa kuwaelewa wanaosema kwamba ufisadi unapojitokeza kupitia mlangoni uzalendo utoroka kupitia dirishani.

  Hili ni jambo la kuangalia kwa umakini vinginevyo tunaweza kujikuta tunauchanganya uzalendo na vitu vingine visivyoeleweka.

  mpakia@yahoo.com
  0787 349 765


  © New Habari (2006) Ltd
  All rights reserved
  Huchapishwa na New Habari (2006) Ltd. S.L.P 78235, Dar es Salaam
  rai@newhabari.com
  ------------------------------
  Nasiskia kizunguzungu.
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hii makala ina matatizo makubwa ya kimantiki.

  Moja kati ya sifa za mzalendo ni kuweka maslahi ya taifa mbele ya maslahi yake binafsi (Mfano mzuri ni mtu anaekubali kufa vitani kwa ajili ya kuitetea nchi yake). Fisadi hawezi kwa namna yoyote ile kuwa mzalendo. Hata kama mabilioni aliyoiba ameyawekeza nchini, hilo halitoshi kumnfanya awe mzalendo.

  Ufisadi unaleta athari nyingi kwa taifa ambazo kamwe haziwezi kufidiwa na faida zinaweza kupatikana kwa fisadi kuwekeza pesa alizoibia taifa hapa nchini.
   
 3. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Fisadi anawezaje kuwa Mzalendo??? wakati vijisenti vyake anahangaika kila siku kuvipeleka New Jersey?
   
 4. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Msiba Pakia , ndiyo jina la mwandishi wa makala hiyo. Inasikitisha kwamba waandishi wenye kupenda makombo ya mafisadi wapo tayari kusema au kuandika lolote ili muradi wawafurahishe mabwana zao. Inafaa wajue kwamba kosa ni kosa tu halipambiki!
   
 5. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umechukulia kwamba mtu kuajiri watu, kulipa kodi, kuuza bidhaa nnje ni vegezo tosha vya kuangalia kama mtu ni mzalendo? Una-assume kwamba mtu akiwa anafanya hayo hawezi kuwa ana-jinsi nyingine ya kuhujumu nchi hiyo?

  Itakuwa sawa tukikubaliana kwamba mzalendo ni yule mtu anayeweka maslahi ya nchi yake mbele zaidi kuliko ya nchi nyingine.

  Mimi kwangu mwizi ni mwizi tu, haijalishi akishaiba anapeleka wapi ... hata kama akienda kutoa sadaka.

  Sidhani kama kwa kuumwaga tu uraia wake unaweza ukahitimisha kwamba huyu mtu si mzalendo. Watu wanasababu nyingi tu za kufanya hivyo, ikiwa ni pamoja na nchi anayoipenda mtu kutompenda yeye kama yeye anavyoipenda.

  Kwa ujumla sidhani kama uzalendo ni black and white hivyo. Naamini kila mmoja wetu ana maswala ambayo yuko tayari kuweka maslahi ya nchi mbele na maswala ambayo hayupo tayari. Kwa hiyo kwangu mimi swali sio mtu ni mzalendo ama la, ila mtu ni mzalendo kwa kiasi gani.

  Pengine huyo mtu aliyeumwaga uraia wake anachangia taifa fedha za kigeni zaidi, na kwa dhati zaidi, kuliko wewe unayejifanya kuwa ni mzalendo kwa sababu tu haupo tayari kuumwaga uraia wako.

  Pengine huyu mtu angeung'angani uraia wake na angekuwa hapa, mngekuwa mnambeza kama mnavyowafanya akina W. Slaa.
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180

  Ni kweli mkuu Kamuzu, in fact this is BULL S..T!
  Magazeti yanaandikwa na watu wenye uwezo finyu wa kujenga hoja ya msingi.
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Once fisadi alwayz fisadi!
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Lipstick on a pig ? It remains a pig, period. End of the story.
   
 9. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Hii SIYO MAKALA.Nafikii wote tunajua makala ni nini.
   
 10. B

  Boma Senior Member

  #10
  Jan 12, 2009
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 190
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli huyu atabaki kuwa FISADI kwa vile kaibia umma ingawa bado katumia ile hela kuleta ajira ili aendelee kujitajirisha kwa kuwanyonya wafanyakazi atakaokuwa amewajiri na hata kodi anaweza asilipe yote kwa kukwepa maana " evil mind" haiwezi kumtoka.

  Fisadi mwingine kama Chenge wa kuficha hela nje ya nchi pesa ambazo zingetumika vizuri zingeweza kusaidia kujenga BARABARA ya lami toka mtwara hadi sirari na kuinua kiwango cha uchumi, huyo ni FISADI mbaya zaidi ambaye anatakiwa kuuwawa hadharani kwa risasi.
  hivyo basi FISADI NI FISADI HATA SIKU FISADI HAWEZI KUWA MZALENDO NA WALA MZALENDO AKAWA FISADI ni lazima sifa moja uwe huna (fisadi/mzalendo) ilikuwa na sifa nyingine
   
Loading...