Tunawezaje kumng'oa Spika katika nafasi yake? Katiba yetu inasemaje?

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Kwa mujibu wa Ibara ya 84(7)(d) na (h) ndiyo ninaona vina angalau kamwelekeo kenye unafuu kuweza kumng'oa Spika kwenye nafasi yake.

84(7)
" (d) if that person is removed from the
office of Speaker by a resolution of
the National Assembly supported by
not less than two-thirds of all"

"(h)if it is proved that person has
contravened the provisions of the law
concerning the ethics of public
leaders"

Kwamba kwa hiyo ya kwanza itokee asilimia Zaidi ya 66 ya wabunge wote wampigie kura ya kutokumwamini - hapa panawezekana tu iwapo vitendo vya Spika vinakuwa vainawakera sana wabunge wenzake na hata jamii kuona kuwa sasa haenendi vile inavyostahili. Kwa Spika huyu dalili hizo mpaka sasa ni ndogo ingawa kwa mbaaali mwelekeo umeanza kuja. Anachotakiwa kukifanya Spika huyu kwa sasa ni kuongeza tu umakini na kuleta mahusiano mazuri ya mihimili.

Kwa mfano Mahakama ikiamua tu yenyewe "suo moto" kutoa tafsiri ya kile anachofanya Spika kwa kuendekeza wale wabunge 19 basi Mahakama itakuwa imejipatia sifa sana na itaweza kurahisishia wabunge kumgeuka Bosi wao na hata uwezekano wa kumpigia kura za kutokuwa na Imani naye itakuwa ni mterero tu. Kwa hiyo kwa hapa Spika ama anapaswa kuwa mnyonge wa Mahakama au Mahakama yenyewe kufumbia macho jambo hilo ili ionekane ipo "docile" katika kusimamia "enjoyment" ya haki za kiraia au kisiasa.

Inawezekana pia Rais au watendaji wengine wakubwa kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali n.k wakalianzisha kuwa kinachofanyika na Spika sio heshima kwa Katiba yetu - matamko ya hao yanaweza yakawa chachu kwa wabunge kufikisha asilimia zaidi ya 66 za kumpigia kura za kumkosea Imani Spika huyu. Ubaya wa hili linaweza pia likawageukia watendaji wa sababu wabunge nao wanaweza wakageuza kibano cha ama kukosa Imani na Rais mwenyewe au Waziri Mkuu. Hivyo njia rahis zaidi ni hiyo ya kupitia Mahakama.

Katika Kipengele (h) hapo pia chombo kinachohusika na maadili kinaweza kuamua "suo moto" kumchukulia hatua Spika. Chombo hiki kinaweza kusema kuwa uvunjifu wa maadili wa Spika ni ile kutoheshimu Katiba ya Nchi kwa kuendelea kuikanyaga kanyaga. Uvunjifu wa maadili sio tu kuhusishwa na mambo ya ubadhilifu wa mali za umma. Hata kutumia madaraka vibaya pia ni ukosefu wa maadili.

Spika Ndugai ameshaonesha wazi kuwa ni mtu anayetumia vibaya madaraka yake. Ushahidi upo wa kutosha na sio tu kwa ajili ya kuwaendekeza hawa wabunge waliofukuzwa na chama chao lakini pia hata ule ushahidi wa kuendelea kung'ang'aniza wale wabunge waliokuwa wameshakosa sifa ya ubunge kuendelea kuwepo bungeni mwaka jana.

Tena njia hii ya kupitia Sekretarieti ya Maadili inaweza ikawa nzuri Zaidi kwa sababu sifikirii kama Sheria husika inampa kinga Spika. Katika kuijadili approach hii kuna rafiki yangu anafikiria kuwapa kazi hii wanasheria ili wafungue shauri huko Sekretarieti ya Maadili.

Kikubwa tuelewe kuwa Taifa letu limekoseshwa sana uadilifu kwa kupitia Kiongozi huyu wa muhimili muhimu sana sana. Yeye hajui kuwa hstoria inajiandika. Tunaona Taifa letu linavyoshamiri kuwa na watu waoga na wenye uchu wa madaraka kwa sababu ya kufumbia macho maovu yaliyo dhahiri. Isingeweza kufanyika hivi kuanzia kipindi cha Nyerere mpaka Kikwete. Awamu ya tano ilipenda haya yafanyike kwa manufaa binafsi.

Nitaendelea kushangaa sana kama awamu hii itaendelea na upuuzi wa wa hivi kwa sababu tu ya kumlea lea Spika huyu ambaye ubabe kwake ni kitu cha kawaida tu. Ni sisi wenyewe twapaswa kumwambia kwa uwazi anachofanya sio - tusisubiri Mwenyezi Mungu atusaidie kwa yale yanayorekebishika kwa kumrekebisha mhusika sisi wenyewe. Spika Ndugai ikane nafsi ya ubabe na ya unafiki urudishe hadhi yako.
 
Huyo mwenyekiti wa chama chake na chama Kama hawapendezwi na Tabia zake iyo ya kuvunja katiba KWA kukumbatia wabunge feki, na wanaolipwa pesa feki ,akivuliwa uhanachama si inakua tiyari au Bado nae ataendelea kuwa speeker ali Hali Hana chama , ?? Na Kama atarudi gombea uspeeker bila kutokua mbunge si itabidi awe na chama kitakacho mpendekeza japo hakitakua ccm na mda utakua haupo upande wake
 
Chadema na ACT walikuwa upande wa Job Ndugai 2015 wakati huo CCM walitaka wampumzishe, ikabidi wawe wasikivu wampe Ndugai

Ndugai wakati Mgonjwa India walimsuia Tulia wakawa hawaingii Bungen hadi aliporudi 'Mshakaji wao' Ndugai ndio wakarudi Bungen

Siasa ni Ufirauni sana sema ndio hivyo
 
Hii nayo ni approach nzuri sana sana! Lolote linawezekana!
 
Chadema na ACT walikuwa upande wa Job Ndugai 2015 wakati huo CCM walitaka wampumzishe, ikabidi wawe wasikivu wampe Ndugai

Ndugai wakati Mgonjwa India walimsuia Tulia wakawa hawaingii Bungen hadi aliporudi 'Mshakaji wao' Ndugai ndio wakarudi Bungen

Siasa ni Ufirauni sana sema ndio hivyo
Kweli bhana - nimekumbuka!
 
CCM ndiyo iliyomuweka hapo na ni CCM pekee kupitia vikao vya ndani wanaoweza kumtoa. Kwahiyo move lazima ianzie ndani ya chama tena kwenye top brass. Mengine ni taratibu tu anaondolewa kilaini kabisa.

Mchakato kamili upo kwenye kanuni za kudumu za bunge, zitafute ujionee kuanzia azimio linavyopelekwa na utaratibu mwingine.
 
Hii ipo njema sana lakini ni kazi kweli kweli!
 
Ndugai akifanyiwa kama Alivyofilisiwa Mbowe atakufa hata wiki haifiki ule mwili WA madawa hatuwezi kuhimili mkiki wowote.
 
Ndugai akifanyiwa kama Alivyofilisiwa Mbowe atakufa hata wiki haifiki ule mwili WA madawa hatuwezi kuhimili mkiki wowote.
Au ndiyo maana ameonesha kubabaika sana. Au ndiyo homa inaendelea kusumbua nini?
 
Atake asitake tumuongezee muda spika
IMG_20210511_010957.jpg
 
Back
Top Bottom