manywangari jean malonkwa
Senior Member
- Mar 17, 2016
- 193
- 188
Ndugu zanguni habari inayobamba kwa sasa hapa Tanzania ni mchuano mkali kati ya serikali inayoundwa na Chama cha Mapinduzi(CCM) dhidi ya vyama vya upinzani( CHADEMA, CUF,ACT Wazarendo na NCCR mageuzi, just to mention the few). Kiini cha muchuano huu ni madai ya upinzani kuwa serikali hii ya awamu ya tano, inaminya democrasia, hasa baada ya kuwafungia baadhi ya wabunge kuhudhuria vikao kadhaa vya bunge, kupiga marufuku mikutano ya hadhara na hata kuitwa Zitto kabwe police central ili kuhojiwa kwa kile kinachoitwa matamushi yanayoonekana kuwa ya uchochezi anayodaiwa aliyatoa wkt akihutubia mkutano wa hadhara pale mbagala ktk uzinduzi wa oparesheni aliyoiita "Linda Democrasia".
Ni mtiti huu ambao umenifanya nijaribu kuangalia hawa viongozi wetu huko wanakotoka mazingira ya democrasia yakoje.
Nikianza na CCM, wao tiketi ya kuwa Mwenyekiti ni urais, labda wanalogic hasa wakizingatia kuwa mtu hadi kuwa rais anakuwa amekubalika, na wanaCCM wamekuwa wamepata nafasi ya kumpigia kura karibu mara mbili.Lkn je? ni kweli kira rais ana uwezo pia wa kuongoza chama na je?, hakuna watu ambao wana uwezo wa kuongoza chama bila ulazima wa kuwa marais kwanza, je? nafasi ya wana CCM wenye nia ya kukiongoza chama hiki kwa level hiyo ya juu kabisa ipo wapi? Kwenye upatikanaji wa wabunge na madiwani ndani ya CCM atleast hatua za kidemocrasia zinaoenekana. Lkn kwenye mchujo wa wagombea urais, hasa namna wale watano wanavyopatikana nako kuna utata, hakuna vigezo vya wazi ambavyo vimewekwa vinavyotumika kumpitisha huyu na kumuacha huyu, ni kwa msingi huu, ndipo linapokuja swala la watu wachache kutumia utashi wao kuamua ni nani aingie na nani asingie, madhara yake ndo kama kilichotokea July 2015, hapa kuna sehemu uwazi unakosekana, je? watu ambao ni matokea ya mfumo wa namna hii wanawezaje kuwa afya ktk ujenzi wa democrasia imara.
Wakati ukiwatafakari hawa, hebu waangalie hawa nao, angalia uchaguzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, NCCR, CUF unavotawaliwa na ubabe, fitina na michezo michafu, Zitto kabwe alipojaribu kugombea uenyekiti aliundiwa zengwe, akaitwa msaliti, akina Ben Saanane wakatumika kutimiza malengo ya Mbowe, Zitto akaamua kujitumbua kabla hajatumbuliwa, Katiba ya CDM haina ukomo wa Mwenyekiti, kweli? Chama kinachojiita cha kidemocrasia na ninachotaka kuongoza mapambano ya kukuza na kuimarisha democrasia. Hebu angalia jinsi Lowassa alivyopewa ugombea urais akiwa mwanachama wa siku zisizidi 10, hv akina Lembeli na Makongoro Mahanga walipataje ticketi za kugombea ubunge?, hv wale vijana waliokipigania chama,hapa wanapata soma gani? Huku nako angalia Kafulila alivyojaribu kutafta uenyekiti naye akaambiwa anataka kufanya Mapinduzi, akafukuzwa kabla ya kuyaweka sawa baadae, Leo Mbatia amekuwa Mwenyekiti wa maisha, chama kinamsambaratikia, anasema yupo kwenye siasa miaka 25, hv miaka hiyo yote ni kipi amefanya ili kukuza democrasia ndani ya NCCR zaidi ya kujitengenezea umungu mtu pale. CUF nao hawa hapa, Kipumba na Maalimu Seif, chama kama kampuni yao vile, watu wamezaliwa, wameoa na wamezaa, hawa jamaa ndo viongozi na ndo wagombea pekee kwenye Chama, democrasia ipo wapi hapa, Hamad Rashid alipojaribu kuutafta ukatibu mkuu, thubutuu, akabutuliwa, Leo naye kaamua kuanzisha ka chama kake, naye atakuwa mungu myu pale, ndiyo! Zitto kajiita mkuu wa Chama, anajitengenezea mazingira ya kumiliki kachama kake, bila shaka yeye uchaguzi haumhusu, unajua kwanini? Kile kilichomkuta kule ndo kinamfanya aweke mazingira hayo, asije akasumbuliwa kama yeye alivomumsumbua mwalimu wake Mbowe, hapa Zitto naye anakwepa matakwa ya kidemocrasia ya kufanya uchaguzi baada ya mda fulani na kuongoza kwa vipindi.
Pale Rwanda yupo Kagame, hapa karibu Uganda yupo Mseveni, hawa ni kama madikiteta hv, siyo?, wamegombana na marafiki zao wengi, hasa pale wanapoonesha nia ya kutaka kwenda pale walipo wao, tofauti yao na akina Mbowe, Lipumba, Seif na Mbatia ni kwamba hawa ni viongozi wa Nchi, hawa wengine ni viongozi wa vyama. Lkn utashangaa, Mbowe, Lipumba, Seif, na hata Mbatia wakiwaita hawa madikiteta kwa kuwa wamekaa madarakani mda mrefu( ukiachilia sifa nyingine nyingi za udikiteta) hv Mbowe, Mbatia, Seif, Lipumba nyingi mmekaa madarakani mda gani, mna tofauti gani na Kagame au Mseveni, you must be kidding! Msiniambie madikiteta ni viongozi wa serikali tu wanaokaa mda mrefu na wala si viongoz wa vyama wanaokaa mda mrefu, eti eeh!.
Ninachotaka kusema, tuanze kujenga democrasia ya kweli na imara kwenye vyama vyetu, huku ndiko marais, wabunge, madiwani na mawaziri wanatoka, na kwa wale vijana akina Ben Saanane mnaosema mko tayari kutoa damu ili kupigania democrasia kwa ajiri ya watanzania, hebu anzieni mapambano hayo ndani ya vyama vyenu kwanza, wapiganieni vijana wenzenu ndani ya vyama vyenu kwanza, kataaeni kutumika kuwakandamiza vijana wenzenu kama mlivyofanya kwa Zitto. Mkishafanya hivo njooni mtuombe tuwaunge mkono sasa kupambana na hili zimwi lingine, bila hivyo you don't make any difference, wote ni mazimwi tofauti ni kuwa hili zimwi liko madarakani nyie hamko madarakani. Period!!