Tunaweza kupunguza ongezeko la maambukizi ya virusi vya ukimwi katika jamii

ItsMi

Member
Sep 13, 2021
66
31
Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kukushukuru ewe mdau kuipitia mada hii kwa kunipa muda wako kufwatilia swala hili, lengo kubwa ikiwa ni kuelimishana

Tunapo ongelea kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi tulenga magonjwa ya zinaa ambayo hushambulia kinga za mwili kwa kuingia mwilini hatimaye virusi hivyo vya magonjwa hufungua milango kwa malazi mbalimbali kuingia ndani ya mwili na kuanza shughuli ya kudhoofisha kinga za mwili ambazo ndizo zinapambana na vimelea nyemelezi vya magonjwa mwilini

Ambayo huweza kusababishwa na njia mbalimbali ikiwemo kuchangia vifaa vyenye ncha kali ambavyo tayari vimeshawahi kutumika na waathirika wa maambukizi hayo,

Pia huweza kusababishwa na mahusiano ya jinsi mbili wakati wa kufanya tendo la ndoa na mtu ambaye ni muathirika ambapo mtu ataathirika endapo atapata mikwaruzo wakati wa tendo hilo ambapo itachochea mahusiano ya damu kati ya pande mbili hali itayopelekea mtu huyo kuathirika.

Pia wengine huzaliwa wakiwa tayari wana maambukizi ambayo wameyapata kutoka wazazi wao.

Lakini pamoja na hilo kundi lote hili linahitaji kupewa elimu ikiwa sambamba na wale wasio na maambukizi lengo kubwa likiwa kuwaelimisha kuachilia mbali ngono zembe pamoja na kutokuchangia vifaa vya ncha kali.

Ikiwa ni pamoja na kuwajenga vijana bora katika kujitambua, kujilinda na kuilinda jamii kwa nzima kwa kutathimini mahusiano bora pia kutumia njia salama za kujiepusha na maambukizi hayo.


hata hivyo katika jamii bado kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kuingia katika mahusiano na watu tofauti tofauti lengo ikiwa kukidhi haja za miili yao.
Sasa shida imekuwa kwamba wengi hawana elimu zaidi inayohusu maambukizi na namna ambavyo jamii inaweza kuathirika

Tukiangalia kwa ukaribu kuna athari kubwa zinazoendelea kutokea kwenye kwa jamii kwa sababu ya kukosa elimu inayohusu jinsia,elimu ya maisha pamoja na njia za kujikinga na maambukizi ambapo athari hizo ni kama ifuatavyo.
1.Kupungua kwa nguvu kazi ya taifa 2.Umasikini
3.Wimbi kubwa la watoto wa mitaani
Na zingine nyingi.

Hivyo njia pekee za kupunguza matatizo kama hayo na kupunguza hatari zilizopo ni kuendelea kutoa elimu inayolenga kujikinga na maambukizi. ikiwa ni pamoja na kuhamasisha malezi bora ili kunusuru vijana kuingia katika mikumbo na vishawishi vilivyopo katika jamii zetu

Tunaamini serikali itaweka nguvu katika kutoa elimu hii ili tuweze kujenga taifa bora hapo mbeleni
 
Back
Top Bottom