Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Sikatai kwa nchi hata Tanzania kutokuwa na msimamo na kukubali kuyumbishwa ndani na nje ya nchi. Ninachowaambia ni kwamba katika masuala ya mahusiano, ndani na nje ya nchi, tunapaswa tujue namna ya ku balance kati ya kuwa na msimamo, kutoyumbishwa na udiplomasia. Kuwa na msimamo haina maana kukosana na watu ndani na nje ya nchi. Huo sio msimamo, ni kujimwambafai ambako mbele ya safari matokeo yake huwa ni mabaya. Tumefikia mahali Corona inatuvuruga kisiasa ndani na nje ya nchi, ni wazi tuna tatizo na yatupasa tukiri hilo.
Angalia suala la Corona na msimamo wetu dhidi ya nchi jirani na hadi za SADC. Tumeshughulikia suala hili kama vile tuna ugomvi (confrontation) na nchi hizi na mara nyingine hili limeleta hata migongano katika ngazi za chini za madereva wetu au raia mipakani. Kuna wakati tumefanya mambo kama vile kulipiza kisasi na kusababisha migongano na uwezekano wa kukorofishana na jirani zetu kutia ndani Rwanda, Uganda, Zambia na Kenya. Pale ambapo tumealikwa na viongozi wa nchi jirani kujadili masuala ya Corona tumepuuza - kwa kuona hawana la kutuambia sisi tuna msimamo wetu juu ya jinsi tutakavyoshughulika na Corona. Hicho ni kiburi na hakitatusaidia.
Kuna mambo ambayo wala hatukuhitaji kuutangazia ulimwengu lakini tumeona sisi tunajua zaidi na kuitangazia dunia vitu kama mapapai kuonekana na Corona. Kwa nini lakini? Hata viongozi wa nchi jirani ambao inajulikana ni rafiki zetu tumeamua kuwapuuza wanapojaribu kufanya mawasiliano nasi.
Ndani ya nchi Corona imefanya tutukanane viongozi kwa viongozi, na hadi Bungeni kuanza kuitana fulani mbunge wa ovyo na hatarudi Bungeni. Imefikia tunafukuzana hata uanachama au kutumbuana kwa vikosa vidogo na kusahau mazuri watu waliyofanya huko nyuma. Kisa cha yote haya Corona tu?
NI vizuri kuwa na msimamo, lakini haina maana tuonyeshe kuwa na msimamo kwa kuharibu uhusiano na jirani zetu, au hata ndugu zetu ndani ya nchi. Tujifunze namna ya kuwa na msimamo imara lakini kuuonyesha kidiplomasia, sio kujifanya vijogoo vinavyojua kuwika na kuku wa jirani kusikia. Corona inaweza kupita, lakini hawa jirani watakuwapo siku zote. Hivyo basi tuepuke kufanya mambo kwa namna ambapo Corona inabadilisha urafiki uliopo na nchi jirani na kusababisha kutoelewana na hata uadui. Tusikubali kufanya mambo kwa namna ambayo Corona itapoteza heshima ya taifa letu hapo mbele.
Tumkumbuke Nyerere - alikuwa na misimamo mikali lakini bado alikuwa mwanadiplomasia mzuri sana, kiasi kwamba kupinga na kuzishutumu nchi kama Marekani, Uingereza, USA nk hakukusababisha tukosane nao. Aliwashutumu na bado akabaki rafiki yao sana tu na wakamheshimu sana. Awamu hii ya tano ina jambo kubwa la kujifunza kwa Nyerere kuhusiana na mahusiano na nchi na mashirika ya kimataifa, la sivyo Tanzania kama taifa na uongozi wa juu utaishia kudharauliwa na nchi, jumuia za kimataifa na viongozi wa nchi za nje.