Tunaweza kukusanya kodi trilioni 8 kwa mwaka kutoka kampuni za simu tu

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,241
5,442
Ndugu zangu, serikali ikijipanga sasa basi inaweza kukusanya kodi isiyopungua sh tirioni 8 kwa mwaka kutokana na shughuli za makampuni ya simu kwa kutoza 10% ya thamani ya fedha inayopitia kwenye miamala +10% matumizi ya muda wa maongezi.

Faida ya kuanzisha hii kodi inafanya kila mtu achangie uchumi wetu kwa njia moja au nyingine.

Mfano kunawafuga kuku. Nguruwe, Ngome, Wakulima, Machagudoa wa kike na kiume , wafanyakazi kutoka mataifa ya nje wasiolipa kodi, kwani si rahisi kuwafikia.

Lakini sote tunajua hawa wote wanatumia huduma za simu kusafirisha fedha au kuwasiliana. Ili wote hawa waweze kuchangia kwenye uchumi basi napendekeza serikali iweke kodi ya 10% kwa kila fedha inayotumika katika shughuli za mawasiano.

Hii italipatia nchi kipato kisichopungua 8-trilions kwa mwaka kama minimum.

Zinapatikanje hizo pesa, basi angalia hesabu hapa:

1.Thamani ya Miamamala ya fedha eg..mpesa, Tigo pesa, airtel money kwa mwezi ni 4trions na kwa 12 months=48 trions.
Hivyo basi 10%*48tirions=4.8 trilions

2.Pesa itonanayo na matumizi ya muda wa maongezi na internet inayoingia sokoni ni trilioni 4 minimum kwa mwezi hivyo kwa mwaka ni kama trion48.
Mapato ya serikali=10%*48tirions=4.8 tirions kama kodi.

3.Kodi za cooperate tax, faida ya makampuni kwa mwaka =1tirion
Jumla basi tukikubali kuweka kodi mpya ya 10% tutapata mapato yanayo range kati ya trillion 8 hadi tirilion 10.5

Je wadau mnaonaje hapo??
 
Kama Magufuli au Mpango wanafuatilia humu naona watafanyia kazi mawazo yako. Tanzania haya mashirika ya simu yanajitajirisha sana kwa kutumia loop holes zilizopo kwenye system pamoja na corruption.

Hili ni sehemu ambazo Magufuli inabidi abane sana!!

NAAMINI KODI KWENYE NJIA ZA SIMU NDO ZITAFANYA KILA MTANZANIA AU RAIA WATANZANIA KULIPA KODI
 
You're not serious! Yaani mwananchi atume ada ya mtoto, 1m/= say alipie kodi 100,000/=? Tanzania will be the most expensive country to live my friend! At most 1% is acceptable not something above it sembuse 10%! For sure none will use that service watu wataanza kubeba hela kwenye rambo.
 
Kama Magufuli au Mpango wanafuatilia humu naona watafanyia kazi mawazo yako. Tanzania haya mashirika ya simu yanajitajirisha sana kwa kutumia loop holes zilizopo kwenye system pamoja na corruption.

Hili ni sehemu ambazo Magufuli inabidi abane sana!!

Abane sana lakini ajiepushe kumbembesha mwananchi mzigo mzito wa kodi. 10% kama kodi kwa kila transaction unayofanya sio mchezo acheni utani. Kuna gesi, madini, utalii na maliasili nyingine nyingi; hayo ndio maeneo ya kuzoa kodi.
 
Miongoni mwa makapuni yanayochuma pesa bila jasho ni makapuni ya simu.!
 
You're not serious! Yaani mwananchi atume ada ya mtoto, 1m/= say alipie kodi 100,000/=? Tanzania will be the most expensive country to live my friend! At most 1% is acceptable not something above it sembuse 10%! For sure none will use that service watu wataanza kubeba hela kwenye rambo.

HOJA YAKO NZURI SUALA NIKUCHANGIA MAWAZO YA NINI TUFANYE ILI KILA MTU ASHIRIKI KULIPIA KODI KWA NJIA AU NYINGINE
 
mmmh hizo data za 4 trl kuhusiana na miamala ya tigo, m pesa ni za uhakika au za kubuni?? labda tuanzie hapo
 
Maoni chanya. Ni jukumu la mamlaka zinazohusika zifanyie kazi maoni haya kuona kama yanafaa.
 
HOJA YAKO NZURI SUALA NIKUCHANGIA MAWAZO YA NINI TUFANYE ILI KILA MTU ASHIRIKI KULIPIA KODI KWA NJIA AU NYINGINE

Mkuu kila mtu anayetumia mtandao analipa kodi. Suala la msingi ni Serikali kupitia idara na mamlaka zinazohusika kuhakikisha kodi hii inayolipwa na wananchi inafika panapostahili badala ya kuishia mikononi mwa wachache hususan makampuni hayo hayo ya simu. Hata kama tungelipia 100% au zaidi kama kodi kama hakuna udhibiti ni kazi bure.

Swali la msingi ni je, kodi inayolipwa na wananchi kwa sasa inakusanywa kwa kiwango kinachotakiwa? Kama sivyo, nini kifanyike ili iweze kukusanywa? Vyanzo vingine vya kodi ambavyo havimuumizi mwananchi wa chini moja kwa moja vipo au havipo? Kama vipo, tatizo ni nini? Kodi ikusanywe huko badala ya Serikali kukimbilia mahali ambapo ni rahisi "kukwapua" kwa gharama za wanyonge. Serikali iwajibike na moja ya majukumu yake ni kubuni vyanzo vya kodi na kusimamia ukusanyaji wake.
 
Sina nijualo kuhusu maswala ya uchumi ngoja nikae pembeni nione walimu wangu watakavyo tiririka

Nakumbuka Chenge alitaka kuja na kodi ya simcard 1000 kwa mwezi ,sasa kwa hili la 10% sijui
 
Kama kodi ingekuwa kubwa tusingekuwa na hao watega wa mabilioni sababu ya watega kuwa wengi ni bei kuwa ndogo hivyo ni lazima tuwe waangalifu na kujaribu kuwa makini kwani kuongeza kodi ni kuongeza bei
 
Swali ni jee hiyo 10% ya thamani ya pesa (za wateja) zinazozunguka kwa mwezi zinazoitapatikanaje? Kwa kuwaongezea mzigo wateja au ni mzigo wa makampuni ya simu? Hivi majuzi nilikutana na aliyekuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Bodo ya TCRA (Prof Semboja) nikamuuliza why walikuwa hawakusanyi yale mabilioni mpaka wakatumbuliwa? Jibu lake ni kwamba sheria hiyo haikutekelezwa coz ingemaanisha mzigo huo uende tena kwa wateja...
 
Sina nijualo kuhusu maswala ya uchumi ngoja nikae pembeni nione walimu wangu watakavyo tiririka

Nakumbuka Chenge alitaka kuja na kodi ya simcard 1000 kwa mwezi ,sasa kwa hili la 10% sijui

Mkuu afadhali umetukumbusha. T.Shs. 1,000/- kwa mwezi ilizua manung'uniko yasiyo na kifani; huyu anazuka na 10% kwa kila transaction - ukipiga simu, uki-text, ukituma/pokea hela nk.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom