Tunaweza kuishauri serekali kunusuru nguvu kazi hawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaweza kuishauri serekali kunusuru nguvu kazi hawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Eeka Mangi, Mar 21, 2011.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wanajamii wenzangu
  Hivi majuzi nimeshuhudia wawili wakipoteza maisha yao mbele ya macho yangu. Sio hao tu niliwahi kuona hata huko nyuma wakipoteza maisha yao na serikali haifanyi jitihada zozote kunusuru nguvu kazi hii ya taifa hili. Kuna hizi pikipiki za kichina ziitwazo TONDA. Hizi zimefanya vijana wengi kupoteza maisha yao kiasi kuwaacha watoto na familia zao yatima bila kujua la kufanya. Kwa nini serikali isichukue hatua kudhibiti wimbi hili la ununuzi holela wa hizi pikipiki? Wao wenyewe wanasema tatizo hawa waendesha pikipiki hawajui kuendesha na bado ukimuuliza mwendesha pikipiki atakwambia na hata kukuonyesha leseni! Nani kampa? Hivi hawa walopewa mamlaka ya kuhakiki kuwa wanawatahini waendesha vyombo hivi wanabanwa na sheria gani?
  Kwa nini tusithibiti uuzwaji holela wa hivi vyombo?
  Tonda moja ya hali ya juu inapatikana kwa shilingi milioni moja na laki mbili na nusu (1,250,000/=). Kwa hali hii hata watoto wa shule wanaweza kununua hii. Sasa tujiulize baada ya muda fulani vijana watakuwa vilema ama marehemu. Sasa tujiulize nguvu kazi hii haiitajiki? Huwezi kumkuta mtoto yeyote wa kigogo anaendesha pikipiki.
  Sasa tufanyeje?
  Mimi nafikiri serekali ipige marufuku pikipiki za tonda na za aina hii ili tuwanusuru vijana wetu. Inatisha kukuta wodi za pale KCMC wodi imebatizwa Wodi ya Tonda. Ndiyo ipige marufuku hivi vyombo. Mtasema haiwezekani lakini nasema inawezekana!
  Serikali inaiagiza TRA kupandisha ushuru wa Tonda! Kama bei yake ni milioni 1 basi kodi nayo inakuwa milioni 1 jumla milioni 2! Mtu hawezi kucheza na fedha yake na watakaomudu ni wachache na lazima wawe watu wenye akili zao. Kwa wale wanaojua pikipiki kuna honda 110 ni shilingi milioni 5. Tujiulize wenye uwezo wa kununua 110 ni wangapi? Wapandishe kodi za vipuri vya tonda pia! Kama wameweza kuongeza dumping fee kwa magari makuukuu wanashindwa nini kuongeza dumping fee kwa Tonda!
  Kwa nitakaowakwaza mnisamehe ni huruma tu kwa vijana wetu.
  Nawasilisha
   
Loading...