Tunaweza kuchagua upinzani Afrika? Twende pamoja

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
MADHARA YA KUCHAGUA VYAMA VIPYA NA MAWANDA YA DEMOKRASIA.

Na Elius Ndabila

Zikiwa zimebaki siku chache watanzania kuamua aina ya uongozi wanaoutaka, basi ninaomba nitumie fursa kuwakumbusha jambo moja kubwa wapiga kura kabla hawajaenda kupiga kura tr 28/10/2020. Jambo hilo ni Madhara ya kuchagua chama kipya na Mawanda ya Demokrasia.

Ni ukweli usiopingika kuwa moja ya kazi kubwa unapokuwa chama Upinzani ni kuisadia serikali iliyomadarakani Kuto kulala. Maana wakilala basi serikali ni rahisi kuchukuliwa na Upinzani na chama dola kubaki kuwa upinzani. Lakini kutokana na uzoefu wa nchi ambazo nchi zao zimekuwa zikitawaliwa na vyama ambavyo si vyama vya ukombozi hasa nchi ambazo bado zilikuwa zikiendelea tafiti zinaonyesha madhara yake ni makubwa.


Ni dhahiri kuwa Chama kinapokuwa kipya na kinapata bahati ya kushinda uchaguzi/kukiondoa chama tawala huwa havifanyi kazi vizuri na hitumika kama nguzo ya kudumaza maendeleo. Vinadumaza na kufifisha maendeleo kwa kuwa wakisha pata dola basi kazi kubwa inakuwa ya kuimarisha chama ili kiwe na nguvu. Hawafanyi maendeleo ya wananchi. Wanafanya maendeleo ya kujenga misingi ya vyama vyao ili iwe na nguvu sawa au zaidi ya vyama vya ukombozi ili waendelee kusalia madarakani. Hawa hulazimika kuitumia dola kisawa sawa kulinda maslahi ya ujenzi wa chama na si maendeleo ya Taifa. Mathalani chama kinafanikiwa kushika nchi huku kikiwa na misingi dhaifu, ni lazima watakaposhika dola watatumia nguvu kujenga mizizi ya chama ili awamu nyingine ya uchaguzi wawe na nguvu sahihi ya kupambana na chama cha Ukombozi. Hivyo mnapochagua chama kipya mjue kuwa miradi yote mliyokuwa munaendelea nayo basi itafutwa kwani fedha zinaekekezwa kujenga nguvu ya chama.

Jambo la pili ni suala la Watumishi. Duniani kote, vyama vya upinzani vinaamini kuwa watumishi ndio kikwazo cha wao kupata ushindi kwenye chaguzi. Wanaamini kuwa watumishi wanazilinda serikali zilizopo madarakani. Hivyo kwa imani hiyo wakifanikiwa kupata nafasi/ kushinda chaguzi basi wanafanya restracturing upya ya utumishi. Wengi hufukuzwa na wengine kuwa demoted. Na wakati mwingine ukifukuzwa hata haki zao hawapati kwa kuwa watasema serikali iliyokuwepo haikuacha details zozote kuhusu wewe. Wanapokuwa wanawafukuza watumishi basi huamini kuwa wale unemployed ndio walikuwa upande wao. Kwa mantiki hiyo ukiona mtumishi anashabikia vyama vinavyokua basi ujue mtumishi huyo hajui madhara ya Upya.

Jambo la mwisho kwenye madhara ambalo ninatamani pia ku share na ninyi kuwa Vyama vipya mara nyingi hupewa nguvu na mataifa makubwa hasa yanayotamani kuzitumia rasilimali ya nchi hizo. Nchi kubwa/ wawekezaji wa nchi kubwa wanaamini kuwa vyama vya ukombozi kuna mazingira vinawabana hasa katika suala la mikataba ya unyonyaji hivyo wanaamini ni rahisi kuingia makubaliano na serikali mpya ambayo inaweza kuwasaidia kutimiza ndoto zao za mikataba ya kilaghai.

Wasiojua historia ya nchi ya Malawi labda niwakumbushe kidogo. Ninataka nitumie Malawi Kama case study yangu. Mwaka 1994 watu wa Malawi walikiondoa chama cha MCP kilichokuwa kikiongozwa na Kamzu Banda ambacho kuliwasaidia kupata uhuru mwaka 1994. Waliamua kuweka chama cha upinzani wakiamini kupata mabadiliko na maisha bora. Lakini ukweli wa mambo Malawi kwa miaka zaidi 20 waliyoingozwa na Upinzani wamekuwa na maisha magumu kuliko kawaida. Ninakumbuka mwaka 1998 ikifikia hatua mpaka Wamalawi wakawa wanakuja kuomba chakula Tanzania. Ukimpa Debe mbili za Mahindi yupo tayari kukupa mtoto wake umuoe. Malawi baada ya kujifunza janja ya Umagharibi mwaka 2014 waliamua kikirudisha chama cha MCP lakini tume ikawabinya. Mwaka 2019 tena wakakichagua MCP kama hatua ya kujuta, lakini Tume ikachakachua, baada ya hapo Mh Chakwela akiungwa mkono na Salous na Mama Banda walienda mahakamani na kutengua matokeo. Baada ya kutengua matokeo uchaguzi ukafanyika upya mwaka huu na kumpa Mchungaji Chakwela ushindi. Ikumbukwe Chakwela ni Rais kutoka chama kongwe kilichoipatia Malawi UHURU kama ilivyo kwa KANU Kenya, ZANU_PF Zimbabwe, CCM Tanzania na MPLA.

Lakini ninapozungumzia Mawanda ya Demokrasia basi ninajaribu tu kuwakumbusha kuwa demokrasia yoyote inamipaka. Demokrasia bila mipaka ni umasikini. Nchi ambazo kwa kiasi fulani zinajaribu kutimiza elements za demokrasia basi utambue kuwa wao walianza kujenga Maendeleo na baada ya maendeleo wakaja kujenga demokrasia. Huwezi kujenga demokrasia inayofanana na USA wakati wewe ni maskini, vinginevyo ukubaliane kuwa umeamua kuchagua umaskini kama taji lako la maisha. Hii iko wazi kuwa nchi zilizoendelea hazitaki mataifa mengine yaendelee, hivyo hutumia kila Technicalities kuhakikisha kuwa wanaendelea kuyadumaza.

Maamzi magumu ya Singapore ndiyo yameifikisha hapa leo. Walikuwa na kiongozi mwenye sauti. Ambaye hakuogopa kutamka chochote ambacho aliamini kesho kitakuwa na postive impact. Rais wa Singapore aliamini maendeleo yanakuja kwa watu kusoma ndiyo maana alisema mwanamke asiye soma asiolewe. Walimchukia lakini baadaye elimu imekuja kuwa mkombozi kwenye nchi hiyo.

Jambo kubwa ambalo nchi zinazoendelea zinatakiwa kujifunza ni kuwa nchi ziachwe kuendeshwa kwa Sera, nchi ziendeshwe kwa sheria. Nchi zikiendeshwa kwa sheria basi kila mtu atakapopata nafasi ya kuongoza ataikuta miongozo ya kisheria ambayo itambana kila mtu. Hii itasaidia hata vyama vya upinzani vikishinda kufanya mambo ya nchi na si mambo ya kujenga vyama vyao.
 
Back
Top Bottom