Tunaweza kuacha kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma kama tulivyoacha mengine ya Nyerere

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,366
45,746
Kwa nini linaonekana ni jambo jema sana la kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma lakini hatumuenzi kwa kubadilisha katiba yetu kutokana na maneno yake aliyosema “Katiba hii imenipa madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu” ?

Kama tumeamua kuipa kisogo katiba mpya wakati Nyerere alipata kuonya kuhusu katiba aliyoicha tunaweza pia kuacha kutekeleza mchakato wa kuhamia Dodoma.

Au tumekubali kuhamia Dodoma kwa serikali ni muhimu kuliko katiba mpya?
 
Kuhamia Dodoma kuna shida gani?kwani imebaki nn mpaka uanze kuwaza kurudisha majeshi nyuma?
 
Wanaofaidika na kuhamia Dodoma ni wengi sana kuliko wanaharakati wachache wenye kuililia katiba mpya kwa sasa.

Dodoma ni karibu kwa watu wa kanda ya ziwa, kwa wale Kigoma, Katavi na Rukwa. Katiba ina umuhimu wake lakini nchi kuwa na maendeleo mtawanyiko yanayogusa kila kona kwa msingi wa Dodoma kuwa makao makuu ni jambo la muhimu zaidi.
 
Watu wanahudumiwa na kufikiwa kwa wepesi zaidi katika Tawala za mikoa na serikali za mitaa. Hakuna mwananchi wa kawaida anayehitajika kwenda Dar es Salaam au Dodoma kufuata huduma za serikali kuu.

Huwezi kuukwepa uwepo wa makao makuu ya nchi hata kama zipo ofisi za tawala za mikoa.
 
Miji inakua yenyewe na technology inaondoa uhitaji wa mtu kuwa kwenye physical location fulani, pia in a very near future idea ya working places or office premises itaisha. Covid 19 imetuonesha kwamba si lazima kuwa confine watu sehemu moja ili kazi ifanyike au huduma zitolewe save for huduma zinazotaka physical contact.Kwa mantiki hiyo,napata wasi wasi na utimamu wa fikra za viongozi wetu pale wanapochezea kodi za wananchi kwa manufaa ya kisiasa.
 
Kwa nini linaonekana ni jambo jema sana la kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma lakini hatumuenzi kwa kubadilisha katiba yetu kutokana na maneno yake aliyosema “Katiba hii imenipa madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu” ?

Kama tumeamua kuipa kisogo katiba mpya wakati Nyerere alipata kuonya kuhusu katiba aliyoicha tunaweza pia kuacha kutekeleza mchakato wa kuhamia Dodoma.

Au tumekubali kuhamia Dodoma kwa serikali ni muhimu kuliko katiba mpya?
Majority ya Watanzania hawajawahi soma either Rasimu mpya ya Warioba wala Katiba tuliyonayo,
Majority hawana hata nakala,
Suala la Katiba mpya ni motive ya Wanasiasa ambao kimsingi wanaona kabisa kwa Katiba iliyopo ni ndoto kwao kushika dola, Katiba iliyopo anaipa nafasi ccm kuendelea kutawala..
Deep down kwa wananchi wanahitaji Masoko ya uhakika kwa ajili ya Mazao yao ya Kilimo, wanahitaji makazi ya kuishi, wanahitaji huduma bora za Afya, elimu, Ulinzi na usalama, wanahitaji huduma za uhakika za Umeme na maji, miundombinu bora ya Usafirishaji,
Hizo porojo za Katiba ni za wanasiasa wanalala wakiota kutawala nchi, ambapo yamkini nao wakitawala watafanya lolote jambo mradi wabaki madarakani.
 
Miji inakua yenyewe na technology inaondoa uhitaji wa mtu kuwa kwenye physical location fulani, pia in a very near future idea ya working places or office premises itaisha. Covid 19 imetuonesha kwamba si lazima kuwa confine watu sehemu moja ili kazi ifanyike au huduma zitolewe save for huduma zinazotaka physical contact.Kwa mantiki hiyo,napata wasi wasi na utimamu wa fikra wa viongozi wetu pale wanapochezea kodi za wananchi kwa manufaa ya kisiasa.
You may be right but in real sense binadamu ni social animal just like other animals,
Working from home in isolation is devastating,
Physical gatherings zinaanza kurudi kwa kasi hata kwenye nchi za Ulimwengu wa kwanza.
 
Majority ya Watanzania hawajawahi soma either Rasimu moya ya Warioba wala Katiba tuliyonayo,
Majority hawana hata nakala,
Suala la Katiba mpya ni motive ya Wanasiasa ambao kimsingi wanaona kabisa kwa Katiba iliyopo ni ndoto kwao kushika dola, Katiba iliyopo anaipa nafasi ccm kuendelea kutawala..
Deep down kwa wananchi wanahitaji Masoko ya uhakika kwa ajili ya Mazao yao ya Kilimo, wanahitaji makazi ya kuishi, wanahitaji huduma bora za Afya, elimu, Ulinzi na usalama, wanahitaji huduma za uhakika za Umeme na maji, miundombinu bora ya Usafirishaji,
Hizo porojo za Katiba ni za wanasiasa wanalala wakiota kutawala nchi, ambapo yamkini nao wakitawala watafanya lolote jambo mradi wabaki madarakani.
Acha kutusemea wewe! Watanzania tulio wengi tulishiriki kwenye huo mchakato wa kupata katiba mpya. Na tunaihitaji kwa haraka ili nchi yetu ipige hatua ya maendeleo katikaa maeneo mbalimbali.

Hizi akili zenu za kiccm huwa zinatukera sana sisi wapenda maendeleo ya nchi yetu. Tume ya katiba ilizunguka nchi nzima na wananchi kutoa maoni yao, halafu unakuja kuleta porojo hapa! Eti ni matakwa ya wanasiasa!
 
You may be right but in real sense binadamu ni social animal just like other animals,
Working from home in isolation is devastating,
Physical gatherings zinaanza kurudi kwa kasi hata kwenye nchi za Ulimwengu wa kwanza.
why in isolation?that was preventive measure kwasababu ya covid 19. Im not convinced either an office premise facilitates a desired social cohesion,very professional gathering to achieve objectives za employer.
 
Miji inakua yenyewe na technology inaondoa uhitaji wa mtu kuwa kwenye physical location fulani, pia in a very near future idea ya working places or office premises itaisha. Covid 19 imetuonesha kwamba si lazima kuwa confine watu sehemu moja ili kazi ifanyike au huduma zitolewe save for huduma zinazotaka physical contact.Kwa mantiki hiyo,napata wasi wasi na utimamu wa fikra wa viongozi wetu pale wanapochezea kodi za wananchi kwa manufaa ya kisiasa.
Biolojia inasema mamals wote wanawasiliana kwa facial expression. Unayeamini simu au email au zoom inatosha, rudia kisomo cha sayansi.
 
Si hoja! Ubalozi wetu Kenya umehamia Mombasa
Nchi yenye matatizo ya forex exchange kujiingiza katika anasa za kisiasa za kuhamisha mji mkuu, ni moja ya sababu tunaendelea kuwa masikini.

Tunatatua matatizo ambayo hayapo, kama tatizo la kuhamisha mji mkuu, wakati matatizo ambayo yapo, kama kuondoa umasikini, ujinga na maradhi, hatujaweza kuyatatua.

Kulikuwa hakuna sababu ya msingi ya kuhamisha mji mkuu. Hususan kwa sababu zoezi hilo lina gharama nyingi za ziada ambazo haziendani na faida zozote za ziada kiuchumi.
 
Kwa nini linaonekana ni jambo jema sana la kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma lakini hatumuenzi kwa kubadilisha katiba yetu kutokana na maneno yake aliyosema “Katiba hii imenipa madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu” ?

Kama tumeamua kuipa kisogo katiba mpya wakati Nyerere alipata kuonya kuhusu katiba aliyoicha tunaweza pia kuacha kutekeleza mchakato wa kuhamia Dodoma.

Au tumekubali kuhamia Dodoma kwa serikali ni muhimu kuliko katiba mpya?
Nahisi una ufala wa Dar!
Kuna watu wanaamini kila mtu anatakiwa aishi Dar. Kila jema liwe Dar. Kila ofisi iwe Dar. Hiyo ilikuwa enzi ya Kikwete. Na ni ujinga wa kutojua maana ya nchi. Siyo kila mtu ajue mdundiko bhana! Mbona Historia inatueleza makao kuhama Kilwa, Bagamoyo na hatimaye Dar. Unaona shida gani enzi hizi za Tanzania kuhamia Dodoma?
 
Kwa nini linaonekana ni jambo jema sana la kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma lakini hatumuenzi kwa kubadilisha katiba yetu kutokana na maneno yake aliyosema “Katiba hii imenipa madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu” ?

Kama tumeamua kuipa kisogo katiba mpya wakati Nyerere alipata kuonya kuhusu katiba aliyoicha tunaweza pia kuacha kutekeleza mchakato wa kuhamia Dodoma.

Au tumekubali kuhamia Dodoma kwa serikali ni muhimu kuliko katiba mpya?
Kwa nini yeye Nyererr hakuleta Katiba mpya kabla hajatoka madarakani?
 
Back
Top Bottom