Tunawatathmini vipi Wanaharakati NCHINI na vuguvugu la kisiasa (Live on Star TV)

Hapo penye nyekundu panahitaji ufafanuzi, ingalau muuliza swali angetoa mifano kuliko kutoa sentensi ya jumla jumla.
magreth sitta alikuwa CWT Kama mwanahasakati leo unamsikia?.then mtazame aliyekuwa Kamanda Kutoka kigoma KABURU leo wapi?
 
Mimi nadhan huyu mama wa cuf asipotoshe ukweli ukweli ni kwamba viongozi wa vya wamekua kama mwingu watu na ukweli ni kwamba wanawakosea fursa wananachi walio wachagua
 
Thanx Yahaya,

Nawapongeza sana wanaharakati kwani wamekuwa msatri wa mbele kuanzisha vuguvugu mbalimbali za kuleta maendeleo na kupinga uzalilishaji unaofanywa na administrative organ (serikali na vyama vya siasa)

Kuhusu kupewa ulaji na kukaa kimya si wote kwani tunao akina Tundu Lissu (MP) amekuwa mwanaharakati hai hadi Bungeni.

Kuwaondoa viongozi waliozembea katika mgogoro wa Madaktari ni lazima wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria ili mambo haya ya uzembe yakomeshwe.

Huyo Nyumba ni kiongozi wa serikali au CUF mbona haeleweki anasimamia upande gani! Amekuwa anaji contradict na statements zake
 
Neno harakati kwa maana rahisi sana ni pilikapilika, wanaharakati wengi wa dunia ya tatu mara nyingi ni vibaraka wa mabepali, maana wanapoomba pesa kufanikisha mambo yao wanapewa masharti ya jinsi gani waendeshe shughuli zao.

Suala la wanaharakati kujiingiza katika siasa liko wazi sana, tunashuhudia kuporomoka kwa ubora wa bunge letu sasa hivi kwa kuwa wabunge wengi waliomo kwa sasa ni wanaharakati (maana walikuwa wanaharaki hapo awali, wa haki za binadamu,) ni si wanasiasa, na mwanaharakati suaa la utaratibu halipo, yeye ni mtu wa kuact on the spot.

Wito wangu mimi ni kuwa wanaharakati wajitoe kutumika kisiasa, wawasaidie kweli wananchi, sio wasubiri issue hotcake kama za dowans,madaktari, katiba na zile zinazowapa umaarufu binafsi ndipo wajitokeze, pia waeende vijijini ambako picha halisi ya tanzania inaonekana na si kukaa mijini.
 
Tatizo ni kuwa kuna baadhi ya wanaharakati wanaifanya kazi hiyo kama sehemu ya kujipatia utajiri.

Hawana ule moyo wa kuleta mabadiliko ya kweli kwa wengi, mabadiliko wanayoyatafuta ni yao binafsi hasa kwenye eneo la kujiongezea ukwasi
 
Wanasemaje juu ya mfumuko wa bei wa sasa? Dar nasikia 'sado' ya nyanya iliyokuwa inauzwa 2,000 mwezi Disemba leo inauzwa 7,000!
 
Jamani wanaharakati mjipange!

Kwanini nasema hivyo? Bila kumung'unya maneno wanaharakati wako kimatukio zaidi kama kawaida ya Tz. Mara Richmond, posho za katiba, madaktari, sasa wapo kwenye mswaada wa katiba, yaani hakuna muendelezo wa mambo hayo. Mbona hawahamasishi upatikanaji wa ajira au mpaka wakosa ajira wakijitokeza hapo utawaona wakitoa matamko!

Kuweni wabunifu.
 
Hatua ya pili Wanaharakati wanasema watahakikisha waliohusika katika uzembe uliosababisha Vifo wanaondoka akiwemo Waziri na Naibu wake - Marcus Albany
Wanaharakati wakumbuke kwamba wanaweza kushinikiza serikali iwaondoe wahusika, lakini serikali haiwajibiki kwao wanaharakati na hivyo inaweza isiwaondoe madarakani hao wahusika. Naikitokea hivyo, wanaharakati watafanya lipi?
 
Nawapongeza wanaharakati kwa kazi yao ila nataka wanijulishe.

1. Hivi Chadema wakikosa wanaweza kutoka nje na kuwapinga?.
2. Kila wakati waalimu wanatishia kugoma kwa madai yao ya msingi, ninyi wanaharakati kwanini Msisaidie CWT kufanikisha madai yao, badala ya kusubiri wagome ndiyo waingilie kati? Bora kinga kuliko tiba

kimboka jina zuri sana usiliaibishe unataka unataka wanaharakati wawasaidiaje walimu kupata madai yao zaidi ya kuandamana na kupiga makelele ndio kazi yao kama pressure group kwani hawana serikali na wala hawana uwezo wa kuwalipa mishahara au posho wanazozidai. kupiga kwao makelele huko huko kunatosha inabidi uwashukuru kwa kukubali kupigwa virungu barabarani kutetea maslahi ya wengine.
 
Juhudi za wanaharakati tunaziona wazi lakini je hao wengine waliokamatwa na kuhojiwa napolisi ni kuudhoofisha uwanaharakati au ni vip?
 
hao waliosababisha vifo hasa mawazir na watu wengine wa ngazi za juu hakuna uwezekano wa kuwashtaki?
 
magreth sitta alikuwa CWT Kama mwanahasakati leo unamsikia?.then mtazame aliyekuwa Kamanda Kutoka kigoma KABURU leo wapi?
CWT ni 'trade union' nasio wanaharakati, mama Sita alichomekwa ktk uongozi wa CWT na serikali ili kupunguza makali ya CWT, na kwa hilo serikali ilifanikiwa.
 
magreth sitta alikuwa CWT Kama mwanahasakati leo unamsikia?.then mtazame aliyekuwa Kamanda Kutoka kigoma KABURU leo wapi?

achana na CWT Yesu mwenyewe alisalitiwa na baadhi ya wanafunzi wake lakini hiyo haikuwa mwisho wa ukristo itakuwa mama Sitta au kaburu kuisaliti CWT hiyo haimaanishi ndio mwisho wa kutetea maslahi ya waalimu .
 
Ahsanteni sana wanaJF kwa michango mizito, Fukuyama J2 ijayo ambapo pia tunategemea kuwa na mama Kijo Bisimba na Mh. Tundu Lissu.

Nawatakieni j2 njema.
 
NDUGU YAHAY,
kwanza hongera kwa mada yako nzuri.
hebu wajameni tusimame katika ukweli.tz hatuna wanaharakati,tuna wafungua vinywa.
kwa sababu,kama wangekuepo,hii nchi isingefika hapo ilipo.kila kona inanuka uvundo.
ukiangalia kuna wanaharakati kila idara,eg wapo wa mazingira,siasa,wanawake etc.ila wamejaa uwoga wa kupindukia,wanaongea ili wapate fedha toka kwa wafadhili.
chek ishu za mswada wa katiba,pongezi chadema.ilikua ipite kama ilivyokua..jukwaa la katiba a.k.a kibamba wanatia kinyaaa.
walaiiiiiini!! hebu wajifunze mfano wa mkenya yule mwana-mama aliefariki majuzi profesa(nimesahau jina).
bonge la fighter!!
 
NDUGU YAHAY,
kwanza hongera kwa mada yako nzuri.
hebu wajameni tusimame katika ukweli.tz hatuna wanaharakati,tuna wafungua vinywa.
kwa sababu,kll!ama wangekuepo,hii nchi isingefika hapo ilipo.kila kona inanuka uvundo.
ukiangalia kuna wanaharakati kila idara,eg wapo wa mazingira,siasa,wanawake etc.ila wamejaa uwoga wa kupindukia,wanaongea ili wapate fedha toka kwa wafadhili.
chek ishu za mswada wa katiba,pongezi chadema.ilikua ipite kama ilivyokua..jukwaa la katiba a.k.a kibamba wanatia kinyaaa.
walaiiiiiini!! hebu wajifunze mfano wa mkenya yule mwana-mama aliefariki majuzi profesa(nimesahau jina).
bonge la fighter!!
Anaitwa Prof Wangari Mathai mkuu
 
kimboka jina zuri sana usiliaibishe unataka unataka wanaharakati wawasaidiaje walimu kupata madai yao zaidi ya kuandamana na kupiga makelele ndio kazi yao kama pressure group kwani hawana serikali na wala hawana uwezo wa kuwalipa mishahara au posho wanazozidai. kupiga kwao makelele huko huko kunatosha inabidi uwashukuru kwa kukubali kupigwa virungu barabarani kutetea maslahi ya wengine.
mkuu jina wala si hoja.ila nitaka wanaharakati pamoja na kazi zao nzuri,waingilie kati matatizo ya waalimu ata kwa maandamano nchi nzima kwa kila alifundishwa na waalimu ajitokeze kupinga unyanyasaji na kupuuzwa kwa madai ya waalimu.tukisubiri mpaka wagome au waendelee na mgomo baridi wa sasa,madhara yake ni makubwa zaidi.kuwa na taifa la wajinga ni hatari mkuu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom