Tunawashukuru Wabunge wa CCM kwa kuendelea kuwajali Watanzania!!

NKUU SINDE KWETU

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
830
91
Jukwaa la Siasa,
Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli. Hakika KAZI yenu ni nzuri na wengi wenu mna Upeo mkubwa na nia ya dhati kupambana na shida za wapiga kura wenu. Kwa spidi hii, CCM itapata ushindi mkubwa tena 2015!

Katibu Mkuu, Mh Kinana na Nape pia kazi yenu tunaiona. Tunashukuru pia kuwatembelea na kushiriki katika kazi za Wananchi kila mnapopita kwa ajili ya shughuli za Chama. Hivyo ndio chama kinatakiwa kuwa, lazima muwe karibu na wananchi.

CCM bado kiko Imara, Serikali yake chini ya Mh Kikwete, Makamu wa Rais na pia Waziri wetu Mkuu, Mtoto wa Mkulima Mh Pinda. Mawaziri Kazi yenu ni nzuri na muongeze spidi kama Katibu Mkuu wa Chama anavyotaka.

HAKIKA; Tanzania Imara inatokana na CCM Imara. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki CCM na Viongozi wake.

NKUU SINDE, Nduguyenu.
 
Hata yale Majimbo ambayo CCM haina Mbunge, bado chama na Serikali imeendelea kuyapigania ili yaende sambamba na Majimbo mengine.
 
unajua ccm na serikali msitufanye wajinga watz mnatujali how? kodi ya line, umeme kupanda 68% kuweka dv 5 kuficha ziro, huduma mbovu za matibabu huku ndiko kutujali, raslimali zetu kuzitafuna ninyi na mizungu na familia zenu acheni upumbavu najua mtasema mimi ni cdm.
 
Wanasema time is money, inaonekana hujalitambua hili, huu muda ulioutumia kuandika upuuzi huu ungeweza kuufanyia kitu kingine cha maana. Mnajiwekea malengo madogo alafu mnajisifu kwa kuanzisha division five!!!
 
Wamewajali kwa lipi?
hahaha kweli watz mnanichekesha tatizo ni elimu au kujidanganya na misifa?

attachment.php
 
Ccm ni chama kinachojua nini kinafanya kwa watu wake maendeleo yanaendelea kumiminika katika jamii.
 
NKUU SINDE KWENU tambua Mungu hadhiakiwi hata siku moja na kwa maneno yoyote yale

Nakushauri utubu dhambi hii mapema sana.
 
Hamna kitu walchofanya ccm zaid ya kuflis maliasil zetu kwa maslah binafsi labda kwa hlo mmeleta mabadiliko!
 
Tunashukuru kwa kuwa hata watakuwa mstari wa mbele kuunga mkono kuwa TANESCO waongeze bei ya umeme kwa zaidi ya asilimia 60%. Wanasema kuiwa watanzania hawataki watumie vibatari tu. Wabunge hawa wanawaletea wananchi maisha bora kwa kila MTZ! Madawa ya kulewa sasa mtindo mmoja! Tembo wetu wanaisha mbugani! Maji hakuna! Umeme wa mgawo! Wizara ya Elimu inaongeza alama ya kufaulu kitendo ambacho ni sawa na kugushi matotokeo! Rushwa kila mahali.......! Bungeni kazi yao ni kusema NDIYOOOOOO hata kwa jambo lisilo na manufaa kwa watz! Tunawashukuru. Kama walifanya mema tutaona 2015!
 
Haja dawa yake ni kuinya tu na sio kuja hapa kuropoka ropoka.
 
Hivi umeachaga ulevi wa kupindukia wa viroba we kijana?
Kumbe hukutaka kumwonyesha huyu mheshimiwa! Akiamka hapo utamsikia akiitikia ndioooooooooooo huku akigonga meza bila kujua kuna hoja gani inaendelea.
 
Teh teh, kwa lipi mkuu, kwa kuutwanga usingizi bungeni na kusema ndioooo? Au kwa kuendekeza matendo ya kidhalimu kama ya ubakaji? Mibunge kama kina komba, kayombo,nchimbi, na mingine ni mizigo ya bure kwa watanzania!
 
unajua ccm na serikali msitufanye wajinga watz mnatujali how? kodi ya line, umeme kupanda 68% kuweka dv 5 kuficha ziro, huduma mbovu za matibabu huku ndiko kutujali, raslimali zetu kuzitafuna ninyi na mizungu na familia zenu acheni upumbavu najua mtasema mimi ni cdm.

Mkuu serikali zote Dunia zina changamoto zake. Hizo ni chache katika mafanikio makubwa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom