Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Marekani walijua kabisa kwamba kulikuwa na kikosi kilichobatizwa jina la "Wasiojulikana" hapa nchini, kikosi ambacho kilijikita katika kuteka watu na hata kuua. Na Marekani waliona wazi kwamba wahanga wa kikosi hiki cha Wasiojulikana walikuwa ni kutoka vyama vya upinzani pamoja na waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla walioikosoa serikali. Pia kulikuwa na wafanya biashara wakubwa ambao walionekana kutenda kinyume na matakwa ya serikali,
Na jambo jingine Marekani waliloona wazi ni kwamba siku zote Polisi hawakuonyesha nia ya dhati ya kushughulikia na kupepeleza kesi au matukio yaliyofanywa na hiki kikosi cha Wasiojulikana. Mara nyingone Polisi walitoa matamko ya kuwalaghai na kuwapoteza lengo wananchi pale ilipohusu matukio ya Wasiojulikana.
Ndipo Marekani wakaamua kuingilia na kuwaokoa watanzania walioendelea kuwa wahanga wa kikosi hiki cha Wasiojulikana. Wakatuma ujumbe. Wakatoa onyo.
Tunawashukuru sana Marekani kwa jambo hili. Ni wazi kuingilia kwenu kumeokoa maisha ya Watanzania wengi na kutoa ahueni kubwa. Tunajua watu wegi walikuwa kwenye "hit list" ya hiki kikosi cha Wasiojulikana na kama sio kuingilia kwenu wengi wangeumizwa au kutoweshwa. Lakini bado tunaomba mwende mbali zaidi na kufunua wazi nani waliohusika na kikosi cha Wasiojulikana, na kiliundwa kwa amri ya nani. Damu za waliopota zinatulilia tuwafanyie hilo.