Mbowe: Tunawafahamu wote wanaotaka kuzua migogoro ndani ya CHADEMA na kutaka kuhama ila hatutawafukuza

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema wanawafahamu Wanachama wote wa chama hicho wenye nia ya kutengeneza migogoro na baadaye kuhama

Hata hivyo, kiongozi huyo wa Chadema amesema hawawezi kuwafukuza katika chama hicho hadi pale watakapoamua kuondoka wenyewe.

Mbowe aliyasema hayo jana alipohojiwa kuhusu makada wa Chadema waliokihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi hivi karibuni.

Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alidai makada wa chama hicho waliotimkia CCM hivi karibuni, ni majeruhi wa uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana na baadhi yao kushindwa kutetea nafasi zao

“Tunatambua watu ambao wanatengenezwa ili wazue migogoro ndani ya chama chetu, na tunatambua watu ambao wakati wowote wakikamilisha malengo waliyopewa, wataondoka.

“Hatuwezi kuwafukuza kwa sababu hata tukiwafukuza, baadaye watapiga kelele tumefukuzwa... tumefukuzwa... tumeonewa... tumeonewa! Tunawaacha waondoke wenyewe kwa utashi wao," alisema.

Alisema sababu zinazotolewa na makada hao kwa sasa hazina mashiko kwa kuwa chama kinatambua kuondoka kwao kunasukumwa na matokeo ya majeraha waliyoyapata katika uchaguzi wa ndani ya chama hicho na si rahisi kuwazuia.

“Wote hao walipoingia, walitoa kauli nzito nzito, lakini katika kipindi cha miaka mitatu, minne, wanatoka wanakimbia sasa. Leo wakitoka wanapiga kelele, haiwasaidii," alisema.

Mwanzoni mwa wiki, aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji, alikihama Chadema na kujiunga na CCM, akidai chama hicho kikuu cha upinzani nchini hakina uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi na kimekuwa na malumbano na migogoro ya ndani.

Dk. Mashinji alitangaza uamuzi huo ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Chadema katika uchaguzi uliopita, Cecil Mwambe, kutangaza mwishoni mwa wiki kujiuzulu ubunge wa Ndanda na uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM.

Vigogo wengine walioihama Chadema na kurejea CCM walikotoka ni mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
 
Nakumbuka kisa Cha mama mmoja aliyemtishia mume wake kuondoka nyumbani (kuachana), mume hakujibu kitu..baada ya kero na kelele kuzidi yule mume akamwambia, sawa, ondoka..yule mwanamke akaanza kupiga kelele kuwa mumewe kamfukuza. This is analogous to what mh.Mbowe is saying. Wanao-rock boat ya CDM wakiambiwa haya ondokeni..Watapiga kelele kwamba wamefukuzwa. Ubinadamu kazi.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema wanawafahamu Wanachama wote wa chama hicho wenye nia ya kutengeneza migogoro na baadaye kuhama

Hata hivyo, kiongozi huyo wa Chadema amesema hawawezi kuwafukuza katika chama hicho hadi pale watakapoamua kuondoka wenyewe.

Mbowe aliyasema hayo jana alipohojiwa kuhusu makada wa Chadema waliokihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi hivi karibuni.

Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alidai makada wa chama hicho waliotimkia CCM hivi karibuni, ni majeruhi wa uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana na baadhi yao kushindwa kutetea nafasi zao

“Tunatambua watu ambao wanatengenezwa ili wazue migogoro ndani ya chama chetu, na tunatambua watu ambao wakati wowote wakikamilisha malengo waliyopewa, wataondoka.

“Hatuwezi kuwafukuza kwa sababu hata tukiwafukuza, baadaye watapiga kelele tumefukuzwa... tumefukuzwa... tumeonewa... tumeonewa! Tunawaacha waondoke wenyewe kwa utashi wao," alisema.

Alisema sababu zinazotolewa na makada hao kwa sasa hazina mashiko kwa kuwa chama kinatambua kuondoka kwao kunasukumwa na matokeo ya majeraha waliyoyapata katika uchaguzi wa ndani ya chama hicho na si rahisi kuwazuia.

“Wote hao walipoingia, walitoa kauli nzito nzito, lakini katika kipindi cha miaka mitatu, minne, wanatoka wanakimbia sasa. Leo wakitoka wanapiga kelele, haiwasaidii," alisema.

Mwanzoni mwa wiki, aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji, alikihama Chadema na kujiunga na CCM, akidai chama hicho kikuu cha upinzani nchini hakina uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi na kimekuwa na malumbano na migogoro ya ndani.

Dk. Mashinji alitangaza uamuzi huo ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Chadema katika uchaguzi uliopita, Cecil Mwambe, kutangaza mwishoni mwa wiki kujiuzulu ubunge wa Ndanda na uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM.

Vigogo wengine walioihama Chadema na kurejea CCM walikotoka ni mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.

Mbowe has never been a dummy!

He is Michael Jordan of this shyt!

People actually do not understand this,Mbowe has been playing political game like nobody else,his IQ is way above everybody else in politics!

Watu nadhani wanajisahaulisha tu how prolific this motherfvcker is....aint nobody like him,mpende au mchukie,you cant deny his prowess!
 
Duh!!
 
Kwa vile JF ni ya kwanza siku zote na kwa vile mimi ni miongoni mwa watu wachache waliopata list ya majina ya watu hao basi bila shaka NITAYAWEKA HADHARANI baada ya kumalizia mchemsho wangu wa Samaki
 
Ni kweli CDM watakuwa wanawafahamu, kama sisi huku mtaani tunawafahamu sembuse viongozi wa chama.

Especially wale madiwani kule Arusha Mjini wanaoanzisha kelele zisizokuwa na maana kumuhusu Lema, kumbe wameshakalishwa vikao na CCM ndio wanatafuta sababu ya kuondokea.

Wapo akina Komu, na wenzake, hawaaminiki kabisa kwa matendo yao, siri zao zimeshafichuka toka kitambo, sasa sijui wataondoka kwa tambo gani, sidhani kama watamlaumu Mbowe tena, itabidi waseme wanaunga mkono juhudi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa vile JF ni ya kwanza siku zote na kwa vile mimi ni miongoni mwa watu wachache waliopata list ya majina ya watu hao basi bila shaka NITAYAWEKA HADHARANI baada ya kumalizia mchemsho wangu wa Samaki
Huna lolote kibaraka tu unapima upepo,
 
Kwa vile JF ni ya kwanza siku zote na kwa vile mimi ni miongoni mwa watu wachache waliopata list ya majina ya watu hao basi bila shaka NITAYAWEKA HADHARANI baada ya kumalizia mchemsho wangu wa Samaki

Unatuwekea usiku bana
 
Attachments

  • tapatalk_1582289596711.jpeg
    tapatalk_1582289596711.jpeg
    42.6 KB · Views: 1

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom