Tunawadharau wahitimu wa shule za kata? wanakuja kuleta mageuzi ambayo sisi tumeshindwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunawadharau wahitimu wa shule za kata? wanakuja kuleta mageuzi ambayo sisi tumeshindwa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Jul 10, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Imekuwa ni kawaida kwa watu wengi kuwadharau vijana wanaohitimu katika shule hizi za kata ambazo nyingi zipo vijijini.

  Serikali ya CCM bila kujua kuwa inajitengenezea bomu, ilianzisha shule hizi ambazo kwa sasa zinazalisha wanavijiji ambao angarau wanakuwa na upeo japo kidogo. Hawa ndiyo chachu kubwa ya mabadiliko ya kisiasa hapa nchini.

  Wengi wa vijana hawa ni wale waliozaliwa ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Sisi tuliokulia ndani ya mfumo wa chama kimoja ni lazima tukiri kuwa kazi ya kuitoa CCM madarakani imetushinda.

  Tusiwadharau wahitimu hawa, wanachangia kwa kiasi kikubwa kubadili fikra za vibabu na vibibi huko vijijini ambavyo bado vikienda kupiga kura vinauliza 'chama cha Nyerere kiko wapi?'
   
Loading...