Tunavyorudi Bungeni Dodoma Hoja Ziamuliwe Maslahi ya Chama au ya Taifa?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunavyorudi Bungeni Dodoma Hoja Ziamuliwe Maslahi ya Chama au ya Taifa??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uwezo Tunao, Jan 24, 2011.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  TUNAVYORUDI BUNGENI: 'NGUVU YA UMMA' TUNAAGIZO 'UTII' NA 'UTETEZI' WAKE MBUNGE UWE NI KWA MASLAHI YA CHAMA CHAKE AU MASLAHI YA WAPIGA KURA???

  Miaka mingi tumekuwa tukitabasamu vizuri na wanasiasa kwa kipindi cha siku 90 wanapokuja kutuomba kuna na kila raia kujihisi mfalme na mwenye nchi kweli huku wazee hawa wakiwaangukia SHIKAMOO hata kwa watoto wadogo.

  Kipindi kirefu baada ya hapo hata salamu tu ya Mungu hugeuka mbinde, kuonana na mwakilishi wako ni kama kwenda kuomba kitu msaada na kukimbiwa mbani. Kama si hilo tu, vile vile hutokea kwamba wanapojadiliana bungeni au kutoa maamuzi mbalimbali yanayohusu maisha yetu wala HAWATUTAFUTI KWANZA MAONI.

  Wao hujiamulia tu ama kwa kuegemea zaidi kunakotoka zawadi wanazozipata kutoka kwa watu au vikundi binafsi vyenye maslahi ya wachache tu.

  Katika BIASHARA HII KWA KUTUMIA VITI VYETU VYA UWAKILISHI BUNGENI, waheshimiwa wabunge, mawaziri na raisi hutumia jina letu kukamilisha mipango binafsi migongoni mwetu hata bila ya ridhaa yetu.

  Maslahi unaoonekana kutetewa zaidi huwa ni UTII NA UTETEZI WA MASLAHI YA CHAMA (Watu wachahe tu) na sisi tukiachwa solemba bila MTETEZI WA MASLAHI YETU / MASLAHI YA TAIFA kwa kipindi chote cha miaka 5 bungeni. Mwananchi ukihoji sana mara kupatikana ripoti tu ama 'kauwawa na majambazi au kapotea katika mazingira yasiofahamika'.

  Au wakati mwingine wananchi TUNAKOSA HAKI YETU YA UWAKILISHI BUNGENI KWA KIPINDI CHOTE KIKATIBA eti kwa kupewa tu kisingizio cha waheshimiwa wanadai wanazuiliwa kutolea kauli jambo lenye maslahi yetu kubwa eti kwa sababu ya DHANA YA JUKUMU LA PAMOJA Collective Responsibility to MINISTERS).

  Cha kushangaza ajabu pia ni kwa jinsi ambavyo Waziri Mkuu Mhe Pinda (ambaye ni mwanasheria kitaaluma) na vile vijitoto vya mafisadi (UVCCM)wote walivyoamua kutangazia umma jinsi wasivyoelewa hii dhana inavyofanya kazi, mwanzo wake na pale inakokomea hata wakadiriki kuitumia ama kukemea baadhi ya ma-kada ambao taifa lao kutafunwa linawauma sana kama sisi huku uswahilini au hata kusema wafukuzwe kazi.

  Nielewvyo mimi, dhana ya 'Collective Responsibility' kamwe haiwahusu chochote hawa magwiji wa sheria nchini (Six, Dr Mwakyembe, Waziri yeyote au hata Mbunge wa CCM kulitolea uvivu KASHFA YA DOWANS kwa sababu malipo kwa Dowans halijazungumzwa kokote na Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Muungano wa Tanzania.

  Kwa kweli kama kuna mahala Mama Kombani angepashwa kurudia yale maneno yake yalioidhi sana taifa ni hapa kwa swala la Dowans ambalo mpaka sasa hivi ni MAZUNGUMZO YA BARABARANI TU ambapo hivi majuzi tu kikundi fulani kinachojiita CC ya CCM ikimjumuisha Mtanzania mmoja aitwaye Ndg Jakaya Mrisho na washirika wake kadhaa walikutana na kulipigia gumzo chumbani kwake ikulu na hata kujifurahisha kubariki utoaji wa malipo hayo kutoka kwenye mkoba wa kodi za wananchi pasipo kufuata mikondo yote stahiki kikatiba.

  Hadi hapa Watanzania tunasema ya kwamba Waziri yeyote au Mbunge wa CCM atakayeendelea kunyamazia UFISADI WA DOWANS bila kuikemea hadharani kwa wakati huu basi moja kwa moja ukahesabu tu kwamba ama uko na sisi wapiga kura au kujichagulia tu kwa hiari kuwaunga mkono Mafisadi nchini.

  Na uamuzi wowote wa ama Mbunge au Waziri wa CCM kuonekana kupingana na chochote chenye maslahi ya kitaifa ndani yake, ikiwa ni pamoja na kupitisha hoja ya kuanzishwa MCHAKATO WA WANANCHI KUJIANDIKIA KATIBA MPYA na uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi kabla ya 2015 (mambo ambayo hayafungwi kwenu na dhana ya 'Jukumu la Pamoja kwa wajumbe wa Baraza la Mawaziri), basi moja kwa moja ujihesabu kuwa ni adui wa 'Umma wa Tanzania' hivyo kuadhibiwa kwako siku ya uchaguzi wowote kwako, leo au kesho, kusije kukaonekana jambo la kuleta mshituko kwako.

  Chagueni vizuri kabla ya kurudi bungeni Februari ama kunyoa au kufuga nywele kwa gharama au faida stahiki na mkondo utakaouchagua.Isitoshe, wananchi katika kila jimbo nchini tunasubiri mje huku majimboni kuwapeni MAELEKEZO YETU (Si Maelekezo ya vyama vyenu) namna gani ya kujadili nini na ukalipigie vipi kura bongeni Dodoma.

  HOJA YANGU:

  Baada ya sisi Watanzania kunyong'onyezwa kiasi hiki na Ufisadi baada ya Ufisadi nchini mwetu na umasikini kukithiri (licha ya takwimu za kuchonga BoT kuleta taswira maridhawa), yote kutokana na:

  (1) DHANA POTOFU YA UTII NA UTETEZI KWA MASLAHI YA CHAMA (Maslahi ya Mafisadi) badala ya wawakilishi wetu kuzingatia

  (2) DHANA HALISIA YA KIDEMOKRASIA YA UTII NA UTETEZI KWA MASLAHI YA WAPIGA KURA / MASLAHI YA TAIFA,

  Je unamaoni gani, tangu hivi sasa na kuendelea huko Bungeni Dodoma, ungependa Wabunge, Mawaziri na Raisi wanapofanya maamuzi yoyote katika taifa letu na au kwa niaba ya taifa letu maamuzi yao hayo yazingatie mwelekeo gani kati ya misingi hiyo miwili???

  Kumbuka mchango wako kwa hoja hii kwa wingi sana vile vile itasaidia kutuma UJUMBE MURUA kwa viongozi wetu mapema zaidi kabla hoja za
  Mhe Mnyika ya Mchakato wa wananchi kuandika Katiba Mpya moja kwa moja mchakato ukianzia bungeni tu, na ile hoja ya Mhe Kafulila juu ya Dowans na hatima ya hoja hizo.

  Je, endapo bunge hili halitozingatia misingi mtakaochagua hapo chini hasa kuhusu miswada hiyo muhimu kwetu, kwa kuegemea nguzo isiostahili kati ya hayo mawili hapo juu, KITU GANI KIFUATE??
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu, nikitangulia kuchangia hoja, vyama vya siasa vikome kabisa KWA KUTEKA HAKI ZETU KIKATIBA kuwakilishwa bungeni kwa kutii na kulinda maslahi yetu wapiga kura na wala si mbunge kujificha chini ya utii na utetezi wa maslahii ya chama chake cha siasa KWA KUFANYIA BIASHARA za kifisadi mgongoni mwetu na vikundi vyenye nguvu ya hela nje na hata ndani ya bunge.

  Endapo waziri na au mbunge niliyemchagua atakosa kutetea maslahi ya taifa kwa kisingizio cha kujidai kukipenda sana chama chake kuliko mimi niliyempa haki hiyo ya kwenda kuniwakilisha huko basi ujue fika kwamba wakati wowote nakusubiri huku nje ya bunge na adhabu kali sana kwa kutumia kura yangu.

  Hoya ya Katiba Mpya, Tume huru ya Uchaguzi, Tume ya Bunge ya Uchunguzi wa Matokeo ya kura za kinyang'anyiro cha urais 2010, na hoja juu ya Dowans zote zipitishwe bila kukosa kama kulivyokwisha waagizeni kama wawakilishi wetu huko.

  Tangu Februari 2011 na kuendelea, mjue ya kwamba tutakua tukiwafuatilieni kwa karibu sana katika kila maamuzi mtakazotoa ama kama Mbunge, Waziri au Raisi kwa jina letu. Habari ndio hiyo mapeeeeema msije mkageuka bubu baadaye
   
 3. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kwamba kapata ubunge kupitia chama.
  Wengi hatakushinda kwa nguvu za wasingeweza bila ya kubebwa na chama. Kwa hiyo ataona ni bora akitii chama chake.

  Mgombea binafsi ndiyo anaweza kufanya mambo bila kufuta mkondo/mkumbo wa chama ambacho hakiangalii maslahi ya wananchi/wapiga kura.
   
 4. n

  niweze JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Discussion na review za kupitia kwanza:
  1. Matokeo na Uhalali wa Uchaguzi 2010
  2. Utaratibu wa Kuunda Kamati ya Katiba
  3. Kupitwa kwa Mikataba yote - Wizara ya Madini na Nishati
  4. Utendaji Wizara ya Fedha
  5. Utendaji Bank Kuu
  6. Utendaji Ofisi ya raisi
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Sisi ni m, imeshatoa msimamo wake tayari kwamba wabunge wake wazingatie kwanza maslahi ya chama. Hilo kwao ndilo la msingi zaidi.
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Lakini hii dhana ya chama ndicho cha kuheshimiwa, kuenziwa na kutetewa maslahi yake badala ya kufanya hayo yote kwa wapiga kura ndio jambo moja hatari sana ambayo ndio imetufikisha hapa kulipo leo hii kwa masikitiko makubwa mno karibu kwa kila mtu nchini.

  Watu tunapuuzwa kwa kila kitu wakati ni WAHESHIMIWA WAPIGA KURA TUNAOWAPA WATU KAZI KA MIAKA MITANO MITANO lakini inakua vipi katika siku zote 1,825 sisi wapiga tuwe tunakua waheshimiwa kwa wastani wa siku 90 za kutongozwa kura zetu na wanasiasa na kesho yake tunageuka galasha na kuendeleao kuikalia kimya?????????

  Hili JOKA KUBWA LA UFISADI tunalilea sisi wenyewe katika hiki kichaka kinachoitwa CHAMA KIMESHIKA HATAMU na wala MPIGA KURA hayupo in the the picture. Yeye kazi yake ni VOTING MACHINE ambapo akishamaliza sehemu yake hiyo eti ni wa kukaa kimya tu pembeni akiangalia nchi inavyotafunwa. Mtu ukihoji tu, makubwa kuibaka

  Jamani hii demokrasia ya MPIGA KURA kuheshimiwa katika kila kitu ni jambo ambalo liko wazi mno hata katika nchi zilizoendelea sembuse sisi wakati jambo hili halinunuliwi kwa fedha ambapo mtu ataleta visingizio vya 'nchi ni changaa'!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Hapa Watanzania ndipo pa KUFA NA CHAMA chochote kinachoendelea kuishi kwa TAMADUNI ZA KISIASA ZA karne ya 18 na kuzilazimisha zionekane kwamba ndizo fesheni mpya katika karne ya 21 yetu hii.

  Wapiga kura kote nchini bila kujali chama chako, ni humu kwenye hicho MIZENGO PINDA alipokuja kuwafundia wabunge wa CCM pale Ubungo na JAKAYA KIKWETE kutia kofuli mlango huo. Hebu fikiria jinsi ambavyo Mheshimiwa huyu KIKWETE alivyotutenda hata taifa tunakokwenda hakujulikani halafu kesho atumie DHANA YA CHAMA KUSHIKA HATAMU kwa maslahi ya mafisadi Lowassa, Rostam Aziz, Karamagi, Mkono mbegu za magugu wa siasa nyingine za aina hiyo na tukawaachie salama -- hata siku moja. Kama CCM haikujifunza kwa nini walilazimika kuwanunulia wabunge wengi zaidi ubunge wao badala ya kuchaguliwa kwa ridhaa yetu ni kutokana na swala kwamba huyo mbunge alipokua mjengoni Dodoma alikua akimfanyia nani kazi, Rostam Aziz au mimi hapa??

  Hivyo, kama tunaamini kwamba hili ni ndilo SUMU YENYEWE AMBAYO NI UTAMADUNI ULIOFAA ZAIDI KWA MFUMO WA CHAMA KIMOJA na wala si wa kuendelezwa katika kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi (Competitive Politicts si tu kati ya chama na chama bali pia kati ya mbunge mmoja baada ya mwingine katika chama hicho hicho au nje yake) basi TUKAWATANGAZIE KABISA MAPEMA kwamba KILA MBUNGE TUTAMHUKUMU KWA KICHWA CHAKE na wala si kama kundi basi heri wakabadilike sasa hivi kabla ya kuingia mjengoni maana safari hii hadi na WANAHARAKATI MBALIMBALI tunataka bunge linapofunguliwa na wao wahamishie kambi zao pale pale mjengoni na kufuatilia kila tone la jambo.

  Nasema tangu bunge la Februari Mbunge wa mazoea kujificha ficha nyuma ya kivuli cha chama safari hii hicho kichaka tunakifyeka kabisa na watalaani kwa nini walichagua kazi ya ubunge katika bunge la kisasa wakati wao hawajatambua na kubadilika kuendana na ukisasa wenyewe.

  KUANZIA FEBRUARI WANAHARAKANI KUTIA TIMU DODOMA, kushinikiza mambo kwa maslahi ya wananchi na hapo ndipo chama chochote kiwe ni CCM, CHADEMA, CUF, TLP, NCCR Mageuzi au hizo nyinginezo, kitadiriki kuingia katika huu ujinga wa CHAMA KIMESHIKA HATAMU na hata kutumia UHATAMU HUO kwa maslahi ya hicho hicho chama na wala si maslahi ya taifa basi waandike wameumia na safari hii wapiga kura wala hatukai mbali teeeennnnaaaaaaaaaaa na kuachi HII MIFISI KUCHAKAZA UCHUMI wapendavyo!!!!
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Tusidanganyane wakuu, mara nyingi hoja bungeni zinaamuliwa kwa maslahi ya chama. Utasikia mtu akitetea maslahi ya taifa wenzake watamwambia kuwa anakichafua chama. Hasa wabunge wa chama tawala ndo wanakasumba ya namna hiyo. Hoja ikiwa nzito utasikia eti wanamkutano kumbe ni kujaribu kuwaziba mdomo.

  Maslahi ya taifa mbele!
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nyinyi Maspika vijana mama; mama Makinda na Job Ndugai; kazi yenu pia hapo mbele ni kusimamia katika kweli na haki sawa kwa kila mbunge wakati wote na kukianza sura za @MASLAHI YA CHAMA CHETU' ndani ya vikao basi nyinyi nyinyi tutaonana vibaya.

  Jamani listi ya hoja za msingi kwa wananchi ndio kama hivyo zimeanza kuorodheshwa na nyingine tayari tumezipeleka bungeni kufanyiwa kazi haraka. Sasa kinachofuata ni kwamba, kwakuwa mambo tulioyaomba ni mazito, nyeti na za gharama kubwa kuamua mwelekeo ya maisha yetu ama kuondoka kwenye unyanyasaji wa hivi sasa au la laa; napendekeza (1) kila chombo cha habari kijitahidi walau kupeleka watu 4 Dodoma.

  Wananchi tangu sasa (2) TUNAWAAMRISHA WANAHARAKATI WOTE NA ASASI ZA KIRAIA kuhamishia kwa muda shughuli zao Dodoma kila Bunge kunapoanza kazi. Tunasema Ofisi zote za wanaharakati zihamie Dodoma, wakae huko kwa gharama ndogo kadri inavyowezekana kwa sababu wanaendela maslahi ya wanyonge hivyo wasianze kukaa huko kwa gharama za mafisadi (ikiwezekana waende na mitunubai zao za kulalia zitakazoweza tu kufungwa hata ndali ya shule ya CBE Dodoma au msikiti au kanisa lolote huko kuwapa eneo salama pa kuzipachishia).

  Viongozi wa serikali za wanafunzi wote kwenda Dodoma ili wanapotoa maelekezo kwa wanafunzi wenzao vyuoni isiwe ni mambo ya kusoma tu magazetini zikishachakachuliwa (na serikali ya wanafunzi UDOM wakajue viongozi wenzao hawa watakula wapi na kulala wapi).

  Na wakulima nao hakuna kubakia tu mashambani wakati maamuzi mazito ya taifa yakichakachuliwa Dodoma na kusubiri tu kulia msiba kama huu wa Dowans - Watanzania wenzangu nasema mambo safari hii ni kwenda sambamba na mafisadi kila kona hakuna kulala tena!!!!

  Wabunge waliochaguliwa na wananchi na wale walionunuliwa nyadhifa hizo tutawatambua vizuri sana safari hii na kuwawekea msimamo suala lao. Eti jamani, vyombo vya habari vibaki Dar es Salaam vitangaza fuleni zilivyo kubwa kila kona au mafurika kuchukua nyumba za watu jangwani huku wasiende Bungeni Dodoma na kukodolea macho wakati wote ambapo MASLAHI YA NCHI yanapochezewa kitenesi huko??? Safari hii hatukubali hata kwa vyombo vya habari kuendeleza utamaduni mbaya miaka yote kutoa mianya kwa Mafisadi kujifanyia bungeni wanavyopenda tu. Ifike mahala Tanil Somaia akionekana tu akizengea zengea jengo letu Dodoma, Chenge au Werema akinywa bia mahara na watu ambao sura zao hatuzitambui vyema, rais anahudhuria hudhuria hadi birthday za baadhi ya mikampuni tu nchini basi msiishie tu kutuambia mmewaona huko; tuambieni stori nzito nzito nyuma ya hizo stori za kuonekana kwao na hivyo mambo yatakwenda na hata fomu za kugombewa ubunge zitaheshimika sana sana miaka ijayo bila kuchukuliwa chukuliwa ovyo tu hata na vilaza ambavyo miaka yote huku mitaani tunawajua hivyo.

  Nasema TAASISI ZETU MBALI MBALI za kirai kamwe hazijafanya majukumu yao vizuri kuhusu suala zima ya Bunge na ushiriki huko. Na wao kuchagua kulala katika wajibu wao wa kazi (vyombo vya habari, wanaharakati, viongozi wa serikali za vyuo nchini ...) ndio maana tumefikishwa hapa kama taifa; kubezwa ovyo, kuundiwa njama chini ya DHANA YA CHAMA KIMESHIKA HATAMU, na mafisadi kujigawia panono katika rasilmali zetu kwa sababu hizi hizi.

  Nasema taasisi yoyote itakaolazia tena damu 'Nguvu ya Umma' itakufuata huko huko uliko!!! Mjadala huu mzito uendelee na ingefaa kama nazo hizi taasisi tajwa hapo juu zikijibu tuhuma zetu na kutushirikisha kwamba wanao mkakati gani bungeni tangu Februari na kuendelea.

  Na hapa JF inabidi tuweke mikakati wa kuleta ripoti kama mvua si tu kutoka bungeni bali hadi vyumbani watakamokua wanalala baadhi ya wabunge vilaza, mwandishi wa habari au mwanaharakati ambaye kaonekana kalishwa rushwa huko, chama ambacho kimeamua kuunda genge la mafisi kuzuia maslahi ya taifa yasiheshimiwe na kupitishwa huko. Wazee, hakuna kulala tangu mwaka huu!!!

  Hakuna CCM kuachiwa achiwa kuchezea nchi ovyo tu wapendavyo, WAPIGA KURA KWA NINI SIKU ZOTE TUJIHISI WANYONGE katika kila kitu wakati tunajua fika kwamba UWEZO TUNAO??? Kote tuamke na kucheza nafasi zetu kila mmoja kila mahali.
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Huyo anayemshutumu mwenzake ndio haswa tunaowatafuta kama taifa safari hii maana ndio wanaotufanya waheshimiwa wapiga kura tuonekane mabwege tu. Pindi tu mtu wa aina hiyo atakapobainika kuanzia Februari hii kule Dodoma basi ndipo atakavyokitambua 'Nguvu ya Umma' inavyofanya kazi.

  Na wewe unayeshutumiwa kwa kutenda dhami ya KUTETEA MASLAHI YETU KAMA TAIFA na wala usinyong'onyee kitu hata dakika moja maana usalama wako, kurudi kwako bungeni, tangu siku utakapo acha kutetea maslahi ya chama na kuchagua kutetea maslahi ya taifa, yote yanakuwa moja kwa moja ni jukumu letu sisi 'Nguvu ya Umma' usijali.

  Nasema safari hii kila kitu kinachotendeka ndani na au nje ya bunge, kama si kwa maslahi ya umma, wahusika wote mjihadhari maana katika kila watu watatu unaokutana nao barabarani, vyumbani mnakolala, hotelini mnakokula na hata kule bungeni mnakojadiliana ni mwana Jamii Forum na wala haitochukua zaidi ya dakika mbili kabla Wana JF kote duniani hawajapata habari zako jinsi unavyofanya jitihada kutuhujumu Umma wa tanzania kwa maslahi ya kikundi.

  Wabunge bora mzingatie hilo kwani JF ni zaidi tu ya Jukwaa bali ni Movement na wako wenzi kuliko hata askari wote barani Africa wakiwekwa pamoja. na juu ya hili suala la MASLAHI YA CHAMA AU YA TAIFA mjue kwamba wananchi sote tumejiunga pamoja bila kuruhusu itikadi zetu ndogo ndogo za hapa na pale kututenganisha kwa faida ya mafisadi.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM KULENI TUSHENI HAPO UBUNGO JINSI YA KUONGEA BUNGENI LAKINI MTIHANI WA SISI WAPIGA KURA KWAKO NI JE (1) UMEAMUA KUWA MTETEZI WA 'MASLAHI YA CHAMA' AU (2) MTETEZI WA 'MASLAHI YA UMMA / TAIFA KWANZA'??

  Waache wabunge wa CCM wakale TUSHENI YA KUZUNGUMZA BUNGENI PALE UBUNGO lakini mwamuzi wa mwisho wa kutoa mtihani na kuusahihisha kule bungeni Dodoma ni sisi wapiga kura.

  Mtihani tutakaoutoa bungeni ni rahisi mno na bora tuwape Paper ya Mtihani hapa hapa mapema ili atakayefeli huko abaki akijilaumu mwenyewe tu.

  Sisi Mtihani wetu hautoangalie ni nani anajua kupindisha sana maneno bungeni, wala yule anayejua vifungu vyote vya kanuni za mabunge yote duniani, kwetu sisi mtinani ni kuangalia mbunge mmoja mmoja kwamba anachangia huko bungeni (1) KWA MASLAHI YA CHAMA CHAKE au (2) KWA MASLAHI YA TAIFA.

  Watakaobainika kutetea maslahi ya chama badala ya maslahi ya taifa wote wajiandao kung'olewa bungeni wakati wowote ule na 'Nguvu ya Umma' nchini. Hapo hakuna mjadala.

  Nyingi ni wabunge wetu, hata hivyo vyama vya siasa ni vyetu, iweje mali yetu ipate heshima na kutetewa sana kuliko sisi wenyewe wenye mali???
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwa CCM navyojua hoja zitakuwa zinaamuliwa kwa maslahi ya chama hiyo semina ya wabunge wa CCM unafikiri ilikuwa na kipi cha kujadili zaidi ya kuweka na kulinda maslahi ya chama pindi Bunge litakapoaanza na kuweka kuwakabili wapinzani vilivyo ili wasiweze kufurukuta
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Na huyu Spika mbona wapinzani watamkoma nina uhakika kwa aslimia kubwa zile hoja zenye msingi na tija kwa taifa hili lazima zitafunikwa kombe ili mwanaharamu apite
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ndio hapo kutakapochimbika jiji la Dodoma na kila kona ya nchi kuizika jumla CCM na matandiko yake yote, mijini hadi vijijini na kutoweka kabisa katika historia.
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Chama kikongwe kama CCM bila dira mpya kulinda maslahi ya wote, hatima yake ni kaburini!!
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Lakini The Finest, unafikiri wapiga kura na wanaharakati hatuna uwezo wa kubadilisha huu utamaduni na tukarejesha heshima yetu tena?
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WAANDISHI WOTE WA HABARI ZA UCHUNGUZI TANZANIA
  TUTENDEENI HAKI KWA DOWANS HARAKA SANA!!!


  Watanzania, inaelekea GUDUDU wa ajabu tena wa kutisha mno mpaka ikaifanya CCM, pamoja na hasira zetu hizi zote, ituone wa afadhali kidogo wa kukandamiza zaidi kuliko kusema kutokulipa GUDUDU Dowans.

  Waandishi wetu wa habari za uchunguzi za uchunguzi wakatueleze kiundani zaidi kwamba ni kitu gani GUDUDU iliomo ndani ya huyu mdeni hewa Dowans inayomtisha saaana Dr Kikwete na bench zima ya CC ya CCM kiasi cha kuona ya kwamb wakiue Chama Cha Mapinduzi na au wananchi wa Tanzania wengi zaidi kusafirishwa kwenda kwenye umasikini wa kufa mtu kuliko kutokulipa Dowans??

  Ndugu Said Kubenea, Ayub Rioba, Mbaraka Islam, Maggid Mjengwa na 'This Day' team, nyote hapo hamna haki ya kukalia na kutunyima haki yetu ya kujua GUDUDU kitu kinachotisha ajabu kiasi hicho ndani ya Dowans kwa CCM na serikali yake, kiasi kwamba hata kama ingelikua halali kulipwa, ni sharti malipo yake iwahishwe haraka hata kabla ya wadeni wetu wa zamani kama Wazee watumishi wa Afrika Mashariki.
   
Loading...