Tunavyoishi: Mila, tamaduni au mazoea: Uliwahi kukwazika na kauli 'mgeni utaondoka lini?'

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
28,108
37,641
Wanabodi Salaam Sana!

Ama baada ya Salaam, kicha cha somo hapo juu cha husika.

Ni nini ukakasi wa kauli hii? Ukiulizwa (Mgeni) Utaondoka lini? Unajiskiaje? Wewe uliemuuliza Mgeni, Utaondoka lini, ulikuwa na msukumo gani? Ni sahihi kukaa na Mgeni pasi na kujua ataondoka lini? Kwa nini Mgeni asiulizwe? Kwa nini aulizwe?

Mila, Tamaduni, Lugha gongana au hata Mazoea yetu yametuathiri, inawezekana umewahi kukwazika na kauli: ''MGENI UTAONDOKA LINI?''

Tuelimishane!
 
Bro mImI nilishawahi kupigika wakati natoka mkoa kuja Dar nikafikia kwa baba mdogo ila alikuwa ameoa jike sio mke kwa hiyo alikuwa ameshameza sumu ya jike lake kwamba usiupende hata ukoo wako. Kufika tu baba mdogo mwenyewe ananiuliza utaondoka lini? Kila chakula kikitengwa naona vifumbo "huu unga wa ugali naona unaisha haraka kuliko kipindi cha nyuma itabidi tuanze kufunga kula" inshort baba yangu mdogo kwa sasa anaishi kwangu baada ya kukoswa kuuwawa na yule jike kwa ajili ya Mali zake ambazo zimebaki historia. Nitarudi ngoja nampeleka baba mdogo kuchukua dawa zake kwani sasa hivi kawa alcoholic.
 
Samahani mkuu Mimi kabla hujapanda kitandani utakutana na hili swali yaani lazima, nikiwa na maana nipe ratiba na mipangilio yako ukiwa kwangu sio nakaa na mtu sijui ataondoka lini. Nikiona ratiba yako ndeefuu nakuombea ufupishe uindoke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo real. Hupendi unafiki that's good. Sio mtu anakaa kimya anakuchekea kumbe rohoni kinamuuma anatamani uondoke muda wote. Btw ndio maana napenda ishi mm mwenye, sio kutembea tembea kwa ndugu. Unless waniite

Kwa hiyo wakifunga ndio unga hauisha!
Pumbavu sana Mama Mdogo!

Pole sana Mkuu. Kila chakula kikitengwa naona vifumbo "huu unga wa ugali naona unaisha haraka kuliko kipindi cha nyuma itabidi tuanze kufunga kula....

Sent using Jamii Forums mobile app
Bro hii dunia sitakuja kumdharau binadamu mwenzangu kwa lolote.yaani nilikuwa nalala chumba Cha store kwenye wanaweka vyakula vya mifugo!!!wakati ana nyumba kubwa kuna vyumba havina watu.
 
USHAURI.akija mgeni kwako msome kwanza ana uhitaji gani!!kuna wale hasa wa pwani wanapenda kuhamia kwa mtu haijulikani wataondoka lini.HAWA NI TATIZO!!pili kuna yule kaja kwako anatafuta go on au msaada atoke alipo,huyu mpe support Kama unayo bila kumfitini,ukiona kila support unayompa anaikataa either umemtafutia kazi anatoa sababu za ajabu mpe EXIT.
 
Sijawahi kuulizwa japo kuna kipindi katika nyakati mbili tofauti niliishi kwa muda mrefu na watu ambao sikuwa na uhusiano wa karibu wala undugu nao (mmoja mwaka mmoja mwingine miezi sita) na hata familia yangu haikuwahi kujua ila sikuulizwa swali hilo kwa sababu walimaanisha niishi nao kwa muda mrefu zaidi. Na hata nilipohitaji kuondoka haikuwa rahisi wao kukubali.
Ila kuuliza unaondoka lini ni swali la muhimu. Inamsaidia mwenyeji kuweka ratiba sawa japo kiafrika inaonekana ni unyanyasaji kwa mgeni.
 
Upo real. Hupendi unafiki that's good. Sio mtu anakaa kimya anakuchekea kumbe rohoni kinamuuma anatamani uondoke muda wote. Btw ndio maana napenda ishi mm mwenye, sio kutembea tembea kwa ndugu. Unless waniite

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hadi sasa Mimi au ndugu yangu yeyote akienda nyumbani anaulizwa au Kwa ndugu yangu wa tumbo moja hilo swali utaulizwa tu na tarehe au siku uliyotaja ikifika lazima uondoke, tena umuahidi bi mkubwa ndio jasho litakutoka utasikia " ulisema kesho unaondoka? Uende mama/Baba siku zimeisha, ukijibu siendi hadi wiki ikijayo utamsikia aaaah (ya kukataa) ulisema mwenyewe nenda tu sasa unabaki unafanya nini? Utatimuliwa tu. Kuepuka usumbufu ukifika tu unamwambia bi mkubwa siondoke Leo wala kesho kwani vipi? Ila kwa Kaka/dada isizidi wiki utatimuliwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi Salaam Sana!

Ama baada ya Salaam, kicha cha somo hapo juu cha husika.

Ni nini ukakasi wa kauli hii? Ukiulizwa (Mgeni) Utaondoka lini? Unajiskiaje? Wewe uliemuuliza Mgeni, Utaondoka lini, ulikuwa na msukumo gani? Ni sahihi kukaa na Mgeni pasi na kujua ataondoka lini? Kwa nini Mgeni asiulizwe? Kwa nini aulizwe?

Mila, Tamaduni, Lugha gongana au hata Mazoea yetu yametuathiri, inawezekana umewahi kukwazika na kauli: ''MGENI UTAONDOKA LINI?''

Tuelimishane!
Kaka umenikumbusha like shairi linalozungumzia mgeni siku ya kwanza mpaka ya kumi

Jr
 
Bro mImI nilishawahi kupigika wakati natoka mkoa kuja Dar nikafikia kwa baba mdogo ila alikuwa ameoa jike sio mke kwa hiyo alikuwa ameshameza sumu ya jike lake kwamba usiupende hata ukoo wako. Kufika tu baba mdogo mwenyewe ananiuliza utaondoka lini? Kila chakula kikitengwa naona vifumbo "huu unga wa ugali naona unaisha haraka kuliko kipindi cha nyuma itabidi tuanze kufunga kula" inshort baba yangu mdogo kwa sasa anaishi kwangu baada ya kukoswa kuuwawa na yule jike kwa ajili ya Mali zake ambazo zimebaki historia. Nitarudi ngoja nampeleka baba mdogo kuchukua dawa zake kwani sasa hivi kawa alcoholic.

Jr
 
Mgeni siku ya kwanza, mpe mchele na panza, mtilie kifuani, mkaribishe mgeni,

Mgeni siku ya pili, mpe ziwa na samli, mahaba yakizidia, mzidie mgeni,

Mgeni siku ya tatu, jumbani hamuna kitu, mna zibaba zitatu, pika ule na mgeni,

Mgeni siku ya nne, mpe jembe akalime, akirudi muagane, enda kwao mgeni,

Mgeni siku ya tano, mwembamba kama sindano, hauishi musengenyano, asengenyao mgeni,

Mgeni siku ya sita, mkila mkajificha, mwingine vipembeni, afichwae yeye mgeni,

Mgeni siku ya saba, si mgeni ana baa, hata moto mapaani, hutia yeye mgeni,

Mgeni siku ya nane, njoo ndani tuonane, atakapotokea nje, tuagane mgeni,

Mgeni siku ya kenda, enenda mwana kwenenda, usirudi nyuma, usirudi mgeni,

mgeni siku ya kumi, kwa mateke na mangumi, hapana afukuzwaye, ni yeye mgeni...

Jr
 
Cheki hii kuna ndugu yangu alikua ana kaa home alikaa mda mwingi tuu Kama miaka 7 hivi Alitokea kijijini Mpka akapata kazi sehemu akawa anapata hela vizuri ni Bishoo hatari.
Huyu jamaa yeye bwana Siku nyingine akiambiwa amchukue Dogo asubuhi ampeleke shule badae yeye aendelee na mishe zake. Basi usiku akirudi anakuja kumdai hela mshua (anamtuma dogo akamwambie mzee ampe Chake) Yani nauli yake aliyompelekea Dogo shule Hata Kama ni buku 3 bajaj anadai Au 2 ya boda boda na wakati hapo anafanya kazi

Vile vile unakuta kitu kama dawa ya meno imeisha Au Maji makubwa hanunui Mpaka Mzee anunue
Akaja akaambiwa yote hayo Lakini bado hasikii ni Mwendo ule ule..Mpaka alipokuja kuondoka Mwenyewe
 
Huyo mgeni mgando?
 
Aiseee

Rudi Nyumbani Kumenoga.
 
Back
Top Bottom