Tunauza miche ya kisasa ya korosho

Nov 19, 2019
9
6
TANGAZO TANGAZO

Miche ya kisasa ya korosho inapatikana sasa. Ni miche bora inayoanza kutoa korosho mapema na isiyoshambuliwa na magonjwa kirahisi.

Toa oda sasa kwa mahitaji yako ya miche korosho. Tunapatikana mkoani Lindi. Na tunafikisha miche popote pale Tanzania.

BEI NI SHILINGI 1500 KWA MCHE MMOJA

Unaweza wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo:
0767 209 695
0759761817
0784 400 308
0754 712 116

Email : mnolelaenterprises@gmail.com
 
Attachments

  • IMG-20190823-WA0015.jpg
    IMG-20190823-WA0015.jpg
    71.9 KB · Views: 19
Imefanyiwa sijui ile wanaita budding au grafting?

Na itapatikana around January?
Ndio kuna iliyofanyiwa grafting na isiyofanyiwa.

Ndio inapatikana January lakini kwa kutoa oda yako mapema .
January/February ni kipindi cha upandaji wa miche.

Maranyingi kipindi hiki huwezi kupata miche kirahisi kama hujatoa oda yako mapema
 
Mkuu MnolelaKorosho , usichoke maswali, pengine majibu yake yatanufaisha na kushawishi wengi, maana kwa sisi watu wa bara korosho ni zao geni kwetu. Nitakuuliza hapa ili na wengine wafaidike na majibu utakayonipa:
1. Hekari moja inaweza kupandwa miche mingapi kibiashara?
2. Yapo makadirio ya mazao kwa mkorosho kwa mavuno yanapochanganya?
3. Kuna muda wa uhai wa mti wa mkorosho unaofahamika? Nikimaanisha labda baada ya miaka mingapi itanilazimu kuchoma mkaa na kupanda miti mipya?
 
Asante mkuu kwa maswali mazuri, nami ndo yalikuwa maswali yangu nilipofunguaa uzi,
Kwa kuongezea
4) Tutajuaje kuwa miche yenu sio fake, (Sorry hapa nilishawahi uziwa Miche ya kisasa ya machungwa, matokeo yake miaka saba Sasa inatoa tutunda tudogo na hatufiki hata tutano kwa mche)
5) Nikiorder kwa Sasa itachukua muda gani kunifikia, Mimi nipo Pwani, Ruvu.
 
Hakuna tatizo Mdau

1.Hekari moja kitaalamu tunashauri ipandwe miche 25 mpaka 27 ,kwa nafasi(space)ya mita 12 urefu na mita 12 upana.

*Hii inawezesha na kurahisisha matunzo bora ya shamba.
*Hii inasaidia kupunguza au kufidia gharama za kuanzisha shamba la Korosho tunapendekeza kuchanganya mazao shambani ili mkulima avune mazao ya msimu na kufidia gharama alizotumia wakati wa kuanzisha na kutunza shamba hususani kabla ya kufikia miaka ya Mikorosho kuleta tija.

2.Makadirio kwa mkorosho unapochanganya ni
Kilo 45 kwa mti mmoja wa mkorosho

*Mavuno yenye tija huanza kuonekana Mikorosho ikiwa na umri wa miaka 5. Mikorosho inaanza kuzaa kuanzia na miaka miwili mpaka mitatu. Lakin pia ikibebeshwa itaanza kutoa maua mwaka uleule wa kupanda. Huduma za shamba ndio kila kitu katika mavuno mazuri.

3.Muda wa uhai wa mkorosho ni miaka 50.

*Lakini tumeweza kushuhudia mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani miti hai na inayotoa mazao bora .ikiwa zaidi ya miaka 60 na kuendelea
 
Mkuu nikisema nipande kwa space ya mita 6x6 nini tatizo??? Inaweza kuaffect mimea???
 
Hahahaaa, mkuu hyo spacing ni ndogo sana haitakiwi iwe less than 12 labda zaidi ya 12M, ambapo baadhi ya wakulima wanaweka hadi 15M kurahisisha mechanization in the field.
Karibu sana kwenye kilimo hiki pendwa kusini mwa Tanzania.
 
Point yangu ni good utilization of the land, Kama zinaanza kuzaa baada ya miaka miwili unaweza kupata faida zaidi hadi miaka nane au kumi then unakuja kukata mti Kila baada ya mmoja ili kupata hii spacing ya 12mx12m. Si Utakuwa umepata faida zaidi hapo?? Au??
 
Ndio kuna iliyofanyiwa grafting na isiyofanyiwa.

Ndio inapatikana January lakini kwa kutoa oda yako mapema .
January/February ni kipindi cha upandaji wa miche.

Maranyingi kipindi hiki huwezi kupata miche kirahisi kama hujatoa oda yako mapema
Hiyo bei ya 1500 ni kwa miche yote iliyobebeshwa na ambayo haijabebeshwa?

Nikihitaji miche kati ya 250 - 300 naweza kusaifirishiwa mpaka Tunduru?
Je kuna additional costs zinazotokana na kusafirisha?
 
Asante mkuu kwa maswali mazuri, nami ndo yalikuwa maswali yangu nilipofunguaa uzi,
Kwa kuongezea
4) Tutajuaje kuwa miche yenu sio fake, (Sorry hapa nilishawahi uziwa Miche ya kisasa ya machungwa, matokeo yake miaka saba Sasa inatoa tutunda tudogo na hatufiki hata tutano kwa mche)
5) Nikiorder kwa Sasa itachukua muda gani kunifikia, Mimi nipo Pwani, Ruvu.
Asante Mdau kwa kuuliza Maswali

4.Utatambua miche yetu sio feki ni kutokana na ubora wa mbegu tunazotumuia kuzalishia miche yetu.
Tunatumia mbegu bora kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele,Lindi.
Pia tunatumia mbegu bora zinazotoka kwenye mashamba yetu ya kisasa.
Ukiweza fika kwenye kituo chetu cha uzalishaji miche Mnolela Lindi,utaweza kuona ubora wa Miti mama ya mikorosho ambazo hizi mbegu za miche huzalishwa.

5.Ukiorder sasa hivi zitakufikia mwezi January .
*Ni vizuri kuorder mapema ili tuweze kuweka taratibu zote sawa
 
Kwa yaliotokea kwenye korosho, nimejikuta napata hasira tu mkuu.....
Bora nikae kimya, maana naweza nikajikuta naingia kwenye kesi na jamuhuri
 
Hahahaaa, mkuu hyo spacing ni ndogo sana haitakiwi iwe less than 12 labda zaidi ya 12M, ambapo baadhi ya wakulima wanaweka hadi 15M kurahisisha mechanization in the field.
Karibu sana kwenye kilimo hiki pendwa kusini mwa Tanzania.
Layout Cashew trees are generally planted with a spacing of 7 to 9 meters adopting square system. A spacing of 7.5 m X 7.5 m (175 plants/ ha) or 8 m X 8 m (156 plants/ ha) is recommended. High density planting of cashew at a closer spacing of 4 m X 4 m (625 plants/ ha) in the beginning and thinning out in stages to maintain a final spacing of 8 m X 8 m in the tenth year is also recommended. This enables higher returns during initial years. In case of sloppy lands, the triangular system of planting is recommended to accommodate 15 per cent more plants without affecting the growth and development of the trees. In undulating areas, the planting should preferably be done along the contours, with cradle pits or trenches provided at requisite spacing in a staggered manner to arrest soil erosion and help moisture conservation.
Mimi nilisoma hivyo sasa hiyo ya kwako sii elewi elewi...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom