Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 949
- 2,865
Kauli ya Mzee Makamba ya kusema mungu anawaua wabaya na kuwaacha wema na akawataja majina imeniumiza sana binafsi,baada ya kauli hiyo nikawakumbuka wapendwa wangu walioufa,kwa namna ya pekee nikamkumbuka Hayati Rais John Pombe Magufuli aliyekufa akilitetea Taifa kwa damu na nyama hakulala hakupumzika hakuwa na muda wakupoteza kama kiongozi wakitaifa,alifanya kazi kwa uchungu mkubwa na alitaka kuona mabadiliko yanatokea Tanzania sawa sawa na ndoto ya Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere,nikajiuliza hivi Hayati Daktari John Pombe Magufuli alikuwa mbaya!?
Tunawaenzi mashahidi wa imani waaokufa wakitetea imani,tunawaenzi mashujaa wa Taifa letu waliokufa vita vya Kagera,nilitegemea wanaCCM wangemuenzi Mwenyekiti wao aliyekufa akiwa bado Mwenyekiti wao, Hayati Daktari John Pombe Magufuli kwa dhati ya moyo kwa kuwa Magufuli amekufa kwa sababu ya CCM kuendelea kukaa madarakani hii sio siri wala habari yakuficha Hayati Magufuli amekufa akilitetea Taifa lake chini ya sera hizi hizi za chama Chama cha Mapinduzi, Rais Magufuli amekufa akipigania kuitimiza ilani ya chama cha mapinduzi, kama tunajigamba hadharani tena kwenye mkutano Mkuu wa CCM kuwa waliokufa ni wabaya na wanaoishi ni wazuri,sijui unajaribu kupeleka taarifa gani kwa Watanzania? basi umegusa nyoyo zetu zinazowakumbuka wapendwa Baba zetu,Mama zetu,kaka zetu,dada zetu na mashujaa wetu waliotangulia mbele ya haki.
Huyu Mzee anapaswa kuomba radhi Watanzania kwa kutamka matamshi yale,kwa busara za uzee ulipaswa kujua kati ya waliokufa hivi karibuni ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Watanzania bado wanaomboleza mioyoni na kwenye akili zao,sasa kwa nini kuwakumbusha kumbusha habari za kifo,nashauri mjadala wowote wa kumdhihaki Daktari John Pombe Magufuli ufungwe,maana mjadala huo hauna afya kwa Taifa la Tanzania. China walipata bahati ya kuwa na Marais wenye akili ya ubunifu Mao Zedong na Deng Xiaoping,China ya sasa ni matokeo ya Marais hao waliokufa, lakini sijasikia Wachina waliwatukana Marais hao, leo Tanzania tunatukana waliokufa akiwemo Rais Magufuli aliyeipeleka Tanzania katika uchumi wa kati na kutamkwa na IMF na alipokufa Umoja wa Mataifa ukamuenzi kwa jambo hilo la pekee lililofanywa na Mtanzania aliyekuwa Mzalendo kwa asilimia 120% kwa nchi yake ya Tanzania,sisi tunatukana waliokufa,ni vyema kuheshimu juhudi za pekee zilizofanywa na mtu aliyekufa.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.