Tunatengeneza na Kudesign logo, Business card, Websites Pamoja na Android Application

Nembo ya Biashara (Logo) ni nini na inamsaidia vipi mfanyabiashara/mjasiriamali?

Kwa tafsiri rahisi, nembo ni alama zinazoundwa na maandishi na picha ambazo zinatusaidia kutambua bidhaa au huduma tunayopenda kwa kuwasaidia wateja kuelewa nini unachofanya, wewe ni nani na unaamini nini na matarajio yako ni yapi.

Kuna umuhimu mkubwa wa mfanyabiashara au mjasiriamali kumiliki au kuwa na nembo ya biashara.

Unaweza kuwa na biashara nzuri tu ya utoaji huduma au bidhaa lakini watu wasivutike na biashara yako wakaenda sehemu nyingine kununua kwa sababu tu wamependezwa na nembo ya mfanyabiashara mwenzako kutokana na dhima au ujumbe uliopo.

Kwanini unashauriwa kumiliki au kuwa na nembo ya biashara?

Nembo ya biashara ni utambulisho wako. Kitu kitakachoitambulisha biashara yako au huduma yako bila kujali kama ni bidhaa iko katika uzito au ujazo gani na kama ni huduma haitajalisha inatolewa sehemu gani ni nembo. Nembo inatengeneza hisia, fikra, mwamko na hamasa ya kununua huduma au bidhaa kwa mteja. Kwa mfano ni kawaida kusikia mtu akisema nimeona matangazo ya kampuni fulani kwani imefika hadi huku? Mara nyingi kitu cha kwanza kujiuliza itakuwa ni nembo ya kampuni au biashara.

Nembo inasaidia kuonyesha umaridadi na ufanisi wa kampuni. Kampuni yoyote yenye kuhitaji kufanya kazi kwa ufanisi lazima iwe na logo (nembo). Nembo inasaidia kuonyesha uthubutu na umakini wa kampuni au biashara ambayo yaweza kuwa ni ya utoaji huduma au uzalishaji wa bidhaa.

Nembo inabeba ujumbe wa biashara yako. Ujumbe ni muhimu katika nembo yako kwa sababu inabeba kile ambacho kampuni yako inafanya. Ujumbe mara nyingi huwa ni wenye mvuto na utakaowafanya wateja wako kuvutika na kuja kuhudumiwa au kununua bidhaa zako- Mathalani unamiliki duka la mapambo linaitwa “Mwanamapambo” Kisha ukaweka ujumbe huu “ Unajenga tunakusaidia kupamba” Ujumbe tu umeshabeba kile unachokifanya ambacho ni uuzaji wa mapambo mtu hatokuwa na haja ya kuja kuuliza duka lako linahusiana na mapambo ya aina gani.

Nembo inasaidia kuonyesha umiliki. Nembo ni moja kati ya alama zinazoonyesha umiliki wa biashara kwa sababu nembo hubeba jina la kampuni au mmiliki wa kampuni. Mfano Azam, Kiluswa Company Limited, Kafulusu Enterprises na mengineyo. Majina hayo yanaonyesha mmiliki wa kampuni ni nani.

Nembo inasaidia kuonyesha matarajio ya biashara. Nembo inasaidia kubeba maono na muelekeo wa biashara yako na hasa kwa kuwaonyesha wateja watarajie nini huko mbele kutokana na huduma au bidhaa unazotoa. Hii inasaidia biashara yako kuwa na ushindani dhidi ya kampuni nyingine zinazotoa huduma kama yako. Mfano kampuni za mawasiliano. Maneno kama “Yajayo yanafurahisha! Uko tayari” yanasaidia kuwafanya wateja wa kampuni kuendelea kusubiria mambo mazuri ambayo kampuni yao imewaahidi.

Nembo ya biashara (logo) ina umuhimu mkubwa katika kutambulisha biashara sokoni hivyo ni vema mfanyabiashara au mjasiriamali kuwa na logo kwa sababu itakusaidia kujitofautisha na wafanyabiashara wengine wanaofanya biashara kama yako. Nembo inasaidi sana kuonyesha uthamani wa biashara unayoifanya.
 

KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE(TOVUTI) RASMI YA BIASHARA YAKO?​


Hebu fikiria wewe ni mgeni mahali fulani, baada ya kushikwa na njaa unaelekezwa migahawa miwili, mmoja ukiutafuta mtandaoni unaweza kupata taarifa zake mwingine hauna taarifa yoyote mtandaoni. Uelekeo wako utakuwa upande gani?

Kuishi katika ulimwengu wa kidijitali, tovuti ni zana muhimu sana katika biashara na masoko ya kidijitali. Inakadiriwa 35% – 50% ya biashara ndogondogo duniani hazina tovuti zao binafsi, jambo linalozinyima fursa ya kuweka taarifa zao kirahisi mtandaoni na kupata wateja wapya kirahisi.

Kuna wanaosema kuwa matumizi ya Tovuti yanamezwa na uwepo wa mitandao ya kijamii ambayo pia watu wanaweza kuweka na kutangaza biashara zao humo. Ni kweli, aghalabu, kwa kutumia Mitandao ya kijamii hauna uhakika wa kumiliki taarifa na maudhui unayoweka humo milele. Watengenezaji ambao pia ni wamiliki wa Mitandao hio wanao uwezo wa kusimamisha/kufuta akaunti au maudhui yako muda wowote ikiwa biashara/maudhui yako yanakwenda kunyume na matakwa na masharti yao. Vile vile Mitandao ya kijamii unayotumia inaweza kupungua umaarufu au kufilisika muda wowote usioutegemea mfano kuna mitandao ilikua maarufu sana zamani kama Hi5 lakini umaarufu wake kwa sasa umepungua au kupotea kabisa. Hivyo, uwezekano wa kudorora kwa biashara yako kunategemea pia umaarufu wa mtandao wa kijamii unaoutumia, jambo linalichangiwa sana na ujio wa mitandao mipya ya kijamii kama Instagram, Whatsapp na TikTok. Hii kwako unaionaje? Nitaeleza Tofauti katika matumizi ya Mitandao ya Kijamii na Tovuti wakati Ujao.

Leo hii ntakwambia mambo 10 kuhusu umuhimu wa kuwa na tovuti katika biashara yako:

1. 93% YA MAAMUZI YA MTEJA KUHUSU MANUNUZI HUANZIA MITANDAONI:

Ili kuweza kupata wateja wapya, huna budi kuelewa watu huenda wapi kutafuta vitu kama suppliers, bidhaa na huduma mbalimbali kabla ya kufanya manunuzi. Injini za matafuto mtandaoni zimekuwa kimbilio namba moja huku GOOGLE Ikiziacha mbali Injini zingine kama Yahoo, Bing na Ask. Maana yake hii ni kwamba kama huna tovuti, jua mauzo yako ni 7% tu ya soko zima ambalo hujui kuwa unalo. Upo apo? Yani unapoteza 93% ya mauzo yako kila siku bila hata wewe mwenyewe kujua.



2. UWELEDI (PROFESSIONALISM)

Kama una malengo ya kuifanya biashara yako iwe kubwa duniani, halafu bado huna tovuti rasmi, jua kuna sehemu kubwa ya soko haitakupa kipaumbele watakapokuwa na uhitaji wa huduma/bidhaa ulizonazo. Kwa biashara zenye malengo makubwa kuwa na tovuti huwaweka kwenye nafasi za juu katika kupata tenda na wateja, na huonyesha Uweledi bora katika utendaji wa biashara kuanzia katika muonekano na utendaji wa tovuti. Inakadiriwa 80% ya watu duniani huonyesha kutokua na imani na Biashara ambazo hazina tovuti pale wanapotaka huduma/bidhaa fulani mtandaoni.

ITAENDELEA......
 
3. KUPATIKANA KWA URAHISI

Hebu fikira ila ahueni ya kupata kila unachokihitaji kwa urahisi, tena kupitia katika simu yako tu iliyo kiganjani kwako. Ndivyo ilivyo kwa tovuti ambayo inajieleza kwa kila kitu . Ile raha ya kupata taarifa, huduma au bidhaa kirahisi kupitia simu yako ya mkononi, hufanya wateja waongezeke maradufu na kusambaza sifa bora kwa uharaka sana katika jamii na katika mitandao ya kijamii hali kadhalika. Hii huongezwa chumvi ya SEO (Search Engine Optimization) ambayo ni miundombinu iliyowekwa katika Injini za matafuto ya kimtandao inayowasiliana na tovuti yako na kuweka taarifa katika Injini hizo na hivyo kufanya taarifa za tovuti yako kuonekana haraka zaidi katika matafuto. Biashara imerahisishwa sana kupitia SEO kuliko kutumia Mitandao ya kijamii.



4. TANGAZO LA BURE MUDA WOTE

Tovuti yako inapokuwa hewani, maana yake biashara yako ipo wazi na inajitangaza muda wote na kufika sehemu zote duniani ambapo huduma ya internet inapatikana. Tangazo la bure kabisa hili. Kama tovuti yako ina ubora wa kuvutia zaidi katika muonekano, maudhui na utendaji, basi bila shaka biashara yako ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri sokoni na kupata wateja wengi kila siku. Jiulize hivi, unapofunga ofisi/biashara yako wakati wa jioni kila siku, wateja wapya wanaweza vipi kupata taarifa sahihi muda watakaohitaji? Jibu ni tovuti tu.
 
5. KUTENGENEZA MABALOZI (TESTIMONIALS)

Nafahamu wafanyabiashara wengi ambao hulazimika kuonyesha shuhuda/testimonials katika kurasa zao mara kwa mara ili kuendelea kupata wateja wapya zaidi, ni jambo jema kabisa. Kupitia tovuti yako, unaweza kuweka testimonials kwa idadi uitakayo bila kurudia rudia na katika mpangilio maalum na watu wakaweza kuona ushahidi utakaowaridhisha kuendelea kutumia huduma/bidhaa zako. Mara nyingi Mitandao ya kijamii huzuia kuoneka kwa biashara kwa urahisi kutokana na wimbi la watumiaji wenye maudhui tofauti tofauti katika ratiba ya saa (timeline) yako unayopitia katika mitandao hio, hivyo kusababisha usumbufu (distractions) katika biashara yako.



6. UAMINIFU (TRUST)

Hamna kitu muhimu katika uendeshaji wa biashara na kukuza mahusiano na mteja kama UAMINIFU. Ili kupata wateja wa kudumu katika sekta nyingi, kuwa na tovuti hai ni muhimu katika kudumisha mahusianao katika ya mfanyabiashara kwa muda wowte mteja atakaohitaji.
 
7. POSITIVE ROI

Ikiwa ni Return On Investment (ROI) au Rejesho baada ya Uwekezaji, unapoendesha biashara ambayo ina gharama zake kama umeme, kodi, maji, mafuta n.k, ukijiuliza utaweza vipi kurudisha gharama hizo upate faida? Njia moja nzuri ni matumizi ya tovuti bora yenye uwezo kunasa wateja wapya kwa njia ya mtandao muda wote (24/7) kirahisi kabisa.



8. THAMANI INAYODUMU

Uzuri/Faida moja muhimu kuhusu tovuti ni kwamba, unapoitengeneza una uhakika wa kuimiliki milele na kuifanyia marekebisho muda wowote itakapohitajika kufanya hivyo. Hivyo thamani ya biashara yako itaendelea kuwepo muda wote tovuti yako inapokuwa hewani.
 
9. HUDUMA BINAFSI YA MSAADA KWA WATEJA

Tovuti yako inapokuwa hewani 24/7 una uhakika na kutoa huduma bora kwa mteja mmoja mmoja kuhusu maulizo ya huduma/bidhaa ulizonazo, bei, ushauri nakadhalika. Hivyo kuimarisha mahusiano na ukaribu wako na wateja wako wakiwa popote duniani kwa urahisi kupitia miundombinu mbalimbali unayoweza kuiweka katika tovuti yako kama matumizi ya chatbots na barua pepe maalum za kibiashara (zenye jina/domain name ya tovuti yako).



10. MASIJALA (DATA CENTER) RAHISI YA MTANDAONI

Tovuti yako inaweza pia kuwa masijala rahisi kwa wafanyakazi, wateja na mtu yeyote anayehitaji kujua taarifa kuhusu huduma/bidhaa unazohusika nazo.



NOTE: Katika ulimwengu wa kisasa wa Dijitali, ili kutengeneza nafasi ya kupata wateja zaidi huna budi kuwa na Tovuti hai itakayobeba taarifa muhimu kama jina la biashara, anuani, mawasiliano na maudhui kuhusu huduma na bidhaa zako. Zaidi, weka pia matumizi ya SEO kuongeza kasi.

BONUS POINT: Tovuti yako unapoisajili, unashauriwa pia upate kirurushi cha barua pepe yenye jina/domain name sawa na tovuti yako. Mfano, tovuti yako inapatikana katika anwani ya www. mfano .com, hivyo barua pepe yako ya kiofisi unaweza kuchagua kuwa info@mfano .com au maulizo@mfano .com au jinalako@mfano .com. Kwa kutumia barua pepe zenye jina sawa na anwani ya tovuti yako, unajiweka katika nafasi nzuri ya kuimarisha biashara yako na kuongeza wateja wapya na kazi zenya manufaa haraka zaidi katika biashara/kampuni yako.
 
Mkuu mm nikitaka kujifunza ujuzi wa kutengeneza website unanisaidiaje???
 
Kazi Nzuri Ndio Mahara Pake Tutaendelea Kutoa huduma bora kwa wateja Wetu, Nakukuletea Kazi zenye Ubora Zaidi. Wasiliana Nasi sasa. +255.621454246 au +255.711414246
 
Tumetoa punguzo la bei hadi 50%, kutoka 400,000/= paka 200,000/=. Ili kila mfanyabiashara aweze kuafford na kumiliki biashara yake kisasa zaidi.

NOTE: Gharama zinajumuisha

*Free .co.tz Domain for 1 Year
*Free Hosting for 6 Month
*Free SSL Certificate
*15 Business Email
*Full access cPanel
*Free Support etc.

Pia tunatoa huduma yakusajiri Domain pamoja na Kuhost Website kwa Gharama ya Kuanzia TZS 4,000/= Kwa Mwezi Wasiliana nasi sasa.
 
Offa maalumu ya mwezi huu. Je unamiliki biashara ya aina yeyote na ulikua unahitaji kufikia wateja wengi, kujitangaza pia kuuza bidhaa zako kupitia njia ya kidigitali. Tumetoa punguzo kwa kukutengenezea website. Jitangaze, Uza bidhaa zako sasa kupitia website/ Tovuti yako mwenyewe.

Tumetoa punguzo la bei hadi 50%, kutoka 400,000/= paka 200,000/=. Ili kila mfanyabiashara aweze kuafford na kumiliki biashara yake kisasa zaidi.

NOTE: Gharama zinajumuisha

*Free .co.tz Domain for 1 Year
*Free Hosting for 6 Month
*Free SSL Certificate
*15 Business Email
*Full access cPanel
*Free Support etc.

Pia tunatoa huduma yakusajiri Domain pamoja na Kuhost Website kwa Gharama ya Kuanzia TZS 4,000/= Kwa Mwezi Wasiliana nasi sasa.

CONTACTS
Sales Department
CALL/ WhatsApp: +255.621454246 Au +255.711414246




View attachment 1518198

View attachment 1518199

View attachment 1518200

View attachment 1518201


View attachment 1519655
Gharama ya:
Flayers?
3D logo ?
 
Sajili jina la tovuti yako ya .TZ pamoja na vifurushi vipya kuanzia Shillingi 3,000* kwa mwezi tu!
 

Nini faida ya Kumiliki Website au Blog Kwa Biashara Yako?​

1. Kuwafikia watu wengi zaidi.
2. Kuvutia wateja makini
3. Kujenga uhusiano wa karibu na wateja.
4. Kufanya biashara moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom