jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,052
- 28,242
Toka Rais Magufuli aingie madarakani sijasikia maandamano ya wanavyuo kuelekea HELSB kudai fedha za mikopo ya elimu ya juu.
Hii ilikuwa ni kero kuu iliyokuwa inapelekea kuibua migomo ya mara kwa mara vyuoni.
Imesimamiwa na kupatiwa ufumbuzi.
Leo ninapoanzisha thread hii nimejiridhisha kupitia msemaji wa serikali ,wahasibu wa vyuo na baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuwa ule mzigo unaosubiriwaga kwa hamu kubwa hasa hasa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza yaani kwa jina maarufu unaitwa "BOOM" umeingia rasmi kwenye akaunti za vyuo.
Hata hivyo kuna tetesi ya kuwa vipo baadhi ya vyuo vinataka kufanya figisu figisu kwa kujaribu kukatakata hilo boom la wanafunzi kwa sababu mbalimbali zisizo na mashiko ...ni vyema wakaacha kwani katika hili Serikali ya jembe John P Magufuli haitamuacha mtu salama pindi anapochezea haki ya mnyonge.
Wito wangu kwa vijana ambao miezi michache iliyopita walikuwa humu jamvini tukijumuika nao kwa raha na shari na sasa wako kwenye mishemishe za kusaini boom ...wazitunze fedha wanazopata na kuzitumia kwa manufaa ya kielimu zaidi.
Katika kampeni za kuomba kura Rais Magufuli aliahidi kutoa elimu bure hadi sekondari na kwa sasa shule zinapatiwa moja kwa moja fedha za elimu bure.
Vile vile Magufuli aliwaahidi wanafunzi wa elimu ya juu kupata mikopo kwa wakati na kurekebisha utendaji wa HELSB na taasisi nyingine zinazohusiana na elimu ya juu.
Nihitimishe kwa maneno ya Dr Abbas kwamba" Serikali ni Tajiri Sana "
Na hivyo tunaweza kushuhudia Bombardier zikinunuliwa ,Reli ikijengwa,miradi mbalimbali ikitekelezwa kwa fedha za ndani huku wanafunzi wetu wakiwezeshwa kusoma bila vikwazo.
Basi kwa wanavyuo wote njooni hapa tupeane mrejesho wa boom na yanayojiri....
KWA HISANI YA WATU WA TANZANIA!