onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,346
- 1,303
Kitendo cha kumkamata Mbowe na kumtuhumu kuwa ni gaidi tunajaribu kutengeneza dhana mbaya sana mioyoni mwa watanzania masikini wapenda amani.
Tanzania miaka yote haijawahi kufikia hatua hii Wala kuwa na kikundi cha watu wenye kuwaza kuwa magaidi. Sana sana tulichoshuhudia ni utekaji, kubambikizwa watu vyesi vya hukumu uchumi, uchochezi na kuuwawa baadhi ya watu kwa jina ya wasiojulikana.
Kwa miezi kadhaa wananchi wameanza kupumua kwa maana vitendo hivi vya kuteka vilianza kutoweka. Sasa Tena polisi wanatukumbusha enzi za Omary Mahita kupaka visu rangi ya chama cha CUF kisha kuwatangazia umma kuwa chama hicho ni cha kigaidi.
Pia hao polisi katika statements za kujichanganya walisema Chadema wameingiza makomandoo nchini kipindi cha kampeni 2010.
Kwa vitendo na Tabia hizi tunapenyeza habari mbaya kwenye masikio ya wapenda amani. Mbowe awe gaidi halafu wenzake 6 wakamatwe, kwa Nini asitoroke maana njama zimefichuka.
Gaidi gani yuko front bila kuficha uso kwa matendo yake? Kweli naona Kama polisi wanatamani Sana magaidi waingie nchini. Hii nchi tunaabudu Mungu na kila mtanzania ni mcha Mungu.
Tusibambikiane kesi; kikubwa tushirikiane na kumsaidia rais kwa vitendo na kifikra. Amani ni Bora kuliko madaraka.