Tunataka viongozi wa namna hii kama, zho rongji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunataka viongozi wa namna hii kama, zho rongji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Major, Jan 10, 2010.

 1. M

  Major JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2010
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Bila ya huyu bwana China ingekuwa kama Tanzanian ya leo, lakini yeye aliua mawaziri wanne ambao walikuwa vigogo wa rushwa,aliua watu wengine 21 kutoka idara mbalimbali za serikali ambao walikuwa wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi.Alikuwa waziri mkuu kabla ya aliyepo sasa Wu jia bao.hivi sasa yuko beijing na ni ktk watu wanaoheshimika sana China, hivi sasa ana miaka 82.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  [​IMG][​IMG]

  Uko sawa Mkuu..Tanzania inahitaji kichaa wa hivi kwa sasa, maana njia zingine zooote za utawala bora ndo zinatupeleka huku tuliko, ambako nchi iko kwenye mafuriko, wengine wako mahotelini wanakaribiishana dinner!
   
 3. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mungefanya hivyo mara tuu baada ya uhuru kwa kumuuwa Nyerere, amelostisha Tanzania kwa miaka 22 akihubiri ujamaa :D
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Jan 10, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,607
  Likes Received: 3,909
  Trophy Points: 280
  Mbona hao china na russia nao walikuwa wajamaa na wameendelea, you need to decribe in details your allegations, at least kwa level yako.

  Nao waliofuata baada ya Nyerere walikuwa wanatumia siasa gani? na tumeendelea kwa kiasi gani?
   
 5. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Pengine alikuwa anahubiri kitu asikochokijua, na ndio maana Russia na China ziliendelea na Tanzania ilikwama kwa sera zake za mgando na ubishi wake aliokuwa nao.

  Kwa mtazamo wangu mie, kama Tanzania ingelianza na sera zilizotumika wakati wa Mwinyi tokea siku ya uhuru.Tungelikuwa tuko mbali sasa hivi, kilichoharibu ilikuwa ni mikakati ya Nyerere na jinsi alivyopinga mawazo ya viongozi wote walio karibu nae.Hata kama hizi sera zilizotumika wakati wa Mwinyi alizitengeneza yeye, basi bado anastahili kulaumiwa kwa kuchelewa kugundua kosa.

  Hadi ameshaondoka madarakani, 1995 bado Nyerere alikuwa mstari wa mbele kukandamiza demokrasia isichukue mkondo wake Zanzibar.Maendeleo yakaanza kurudi nyuma ndani ya visiwa hivyo kwa kasi!

  Naamini serekali na viongozi wote wanaendeshwa na sera au katiba, ambazo asilimia zaidi ya 80% zimetokana au zina mizizi ya sera za Nyerere au ujamaa wa kiongozi huyo.

  Huyu kiumbe alichukulia ujamaa kama ni dini, na kuzima kila kinachosimama kinyume na mawazo yake.Kama ni auliwe au kiongozi aliefanya makosa mengi basi yeye anastahili.Licha ya kuwa ametutoka na kutangulia, basi tunatakiwa tuendelee kuondosha sera zake na mawazo yake yaliyobakia humo CCM na serekalini.

  Lakini cha kushangaza, watanzania hawaoni bado wamelala kabisa!
   
Loading...