Tunataka majibu: Ni nani Aliyemtishia Nape Nnauye Bastola?

Daa sikuamini nilivokuja kukutana na huyu mwamba aise na Sehemu niliyokutana naye. Halafu akawa mwana balaa.
Sema jamaa bisho kweli yaani.
Kuna Chaka walienda kumficha. Nape anapajua lakini.
 
Mimi nahisi yule aliyetoa bastola alikuwa ni jiwe mwenyewe isipokuwa alitwaa mwili wa mtu mwingine unajua haya majini na mapepo yanaweza kujibadilisha kadri yatakavyoona inafaa
 
Nimegundua jiwe alikiwa mtu weak sana.....wale watu ukimpiga hoja moja anashika mawe!!
 
Inasemekana alitumwa na le commandent field marshal Daud Albert Bashite.
 
View attachment 1797142
View attachment 1797165
Mnamo tarehe 23 mwaka 2017 Mbunge wa Mtama Ndugu Nape Nnauye alitishiwa bastola hadharani na mtu asiyejulikana.

MARCH 23, 2017, Rais John Magufulli aimteua Harrison Mwakyembe, aliyekuwa Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba, kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Sanaa na Michezo, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Nape Nnauye kwa takriban Mwaka mmoja na nusu.

Baada ya Kutumbuliwa, Nape akaitisha Mkutano na Waandishi wa Habari kuwaeleza wamuunge Mkono Mwakyembe. Hatua hii ilikuja wakati ambapo kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda waziri Nape Nnauye amejiuzulu baada ya kuibuka mvutano kati yake na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliyevamia kituo cha matangazo ya redio na televisheni cha Clouds akiwa na kundi la maofisa wa polisi wenye Bunduki. Hatua ya kutumbuliwa ilikuja Siku moja baada ya kupokea Ripotiiliyo undwa kuchunguza Uvamizi ya Clouds na Kuahidi kuifikisha kwa rais. Nape alilaani kitendo cha mkuu huyo wa mkoa ambapo Jukwaa la Wahariri (TEF) lilimtangaza Makonda kuwa adui namba moja wa uhuru wa habari nchini.

Kulitokea mvutano mkubwa baina ya Nape Nnauye na maofisa wa polisi waliokuwa wakijaribu kumzuia mwanasiasa huyo kutozungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wake baada ya kuvuliwa wadhifa huo na Rais John Magufuli kufikia hatua ya kutishiwa na Bastola ili arudi ndani ya gari na asiongee na Wanahabari. Hadi sasa aliyemtishia Bastola Nape hajafahamika.

Baadaye baada ya Mvutano aliweza kuongea na Wanahabari akiwa juu ya Gari, hakuweza kufika kwenye Ukumbi aliouandaa kwa ajili ya Mkutano huo.

Wakati wa Mkutano huo, haya ndio aliyo yaongea siku hiyo. "Wapuuzi, nimekuja hapa wananitolea bastola eti rudi kwenye gari, nimepigana kuiweka CCM madarakani anakuja mpuuzi eti usishuke kwenye gari, mimi nape sina kinyongo na uamzi wa rais wangu, kama sikumshawishi kunichagua hivyo hata kuniacha ni sawa".

"Nimejitahidikutimiza wajibu wangu, tusihangaike na Nape tuhangaike na Tanzania inapokwenda nimekuwa mzalendo na muungwana, nimekuwa ninatimiza wajibu wangu"

"Mimi ndo nlisimama kuiinua CCM, nitasemakweli daima na fitina kwangu mwiko, kinachotukutanisha sio magwanda ya kijani, ni imani, nimefundishwa na mzee Nnauye kusema kweli na kusimamia ninachokiamini, mimi nlishawahi kufukuzwa CCM"

"Usipopita kwenye matatizoya kisiasa hutakomaa, Ili mbegu iote shuti ioze, nimepandambegu ya kupigania haki, Tanzania ni yetu nchini yetu. Mwalimu, Kawawa waliondoka na sisi tutaondoka".

"Lengo la kuja hapa ni kumshukuru rais kwa alichokifanya, namshukuru kwa kuniamini kwa mwaka mmoja, nampongeza Mwakyembe naye ni mwanahabari".

"Nimefurahi kufanya kazi na nyie, muungeni mkono Mwakyembe na Rais Magufuli"

"Tudumishe amani na upendo wa nchi yetu, Nape ni mdogo kuliko nchi, wakati wa aliyeniteua ameniondoa mimi nitaendelea kuwatumikia
Polisi wamezuia gari ya Nape isiondoke, ameshuka kwenye gari anamsikiliza kamanda wa polisi Kinondoni"

Hadi leo aiyemtishia kwa risasi Nape Nnauye hajafahamika.

Tunataka majibu: Ni nani Aliyemtishia Nape Nnauye Bastola?

Soma:
- Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari


Baada ya tukio hilo Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo Mwigulu Nchemba aliagiza mtu aliyefanya tukio hilo akamatwe.

Soma:
- Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba: Naagiza aliyemtolea bastola Nape Nnauye, achukuliwe hatua


Baada ya muda kupita Mwigulu Nchemba alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Clouds 360 alidai kuwa uchunguzi umefanyika na ikabainika kijana yule hakuwa polisi.

Zaidi Soma:

- Mwigulu Nchemba: Aliyemtisha Nape kwa bastola sio Polisi. Uchunguzi wa Lissu kushambuliwa unaendelea, tutatoa taarifa

- Polisi: Yeyote mwenye taarifa za uhakika za aliyemlenga Nape kwa bastola atujulishe


Hivyo, kutokana na jambo tukio hilo na ufafanuzi wa Waziri wakati huo tunataka kujua mtu huyo alikuwa ni nani?
Tunaanza upyaaaa (in bwege's voice)
 
Kwahiyo amekua waziri ili amjue aliyemshikia bastola??

Ndicho watanzania wanachokihitaji katika Wizara aliyopewa.

Kwa staili hii ndio maana bado hatujaachana na mikopo.
 
2. Pia tunataka kuelezwa, Je, kosa la Nape lilikuwa ni lipi kwenye hilo saga hadi akapelekea kupoteza kazi yake ya uwaziri?
Aliyemtoa Nape madarakani hayupo... Nani tena wa kutoa kosa la Nape zaidi ya yule aliyemteua na kumuondoa?
 
Kwahiyo amekua waziri ili amjue aliyemshikia bastola??

Ndicho watanzania wanachokihitaji katika Wizara aliyopewa.

Kwa staili hii ndio maana bado hatujaachana na mikopo.

Tunakopa kwa maendeleo ya nchi sukuma gang mlituharibia sana
 
Back
Top Bottom