Tunataka mabadiliko gani katika nchi ya kiuchumi? Kiiasa au Kiutamaduni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunataka mabadiliko gani katika nchi ya kiuchumi? Kiiasa au Kiutamaduni?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Profesa, Sep 12, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Kama ni ya Kisiasa je siasa gani tunataka? Na je siasa hiyo ndiyo itakayoweza kubadili hali duni ya wengi na kuleta hayo yanayodaiwa kuwa ni maisha bora? Na hayo masha bora ni yapi? Ni ya kisasa au ya asili? Ya kisaa ni yapi na ya asisli ni yapi? Je ya kisasa yna faida gani ukilinganisha na ya asili? Na ya asili yanafaida gani kulinganisha na ya kisasa?

  Kama ni uchumi, je nchi hii ina utajiri wowote wa rasilimali asili au za kutengenezwa zinazoweza kutumika kukuza uchumi? Kamahatuna tufanyeje? kama tunazo Je Uchumi tulionao sasa unatuletea matumaini yeyote? Hali ya matabaka ya kuchumi yakoje? Kuna usawa katika kupata huduma za afya? Elimu? Maji? Chakula? Kama ni ndiyo au hapana, kwa nini?

  Kama ni utamaduni, tatizo ni nini? Je kuna utamaduni tunaoutaka ambao tunaamini unaweza kutunufaisha kwa hali yoyote ile? Kwanini tunahitaji huo na tusiukuze utamaduni tulionao sasa? Mfano Nyumba za Tembe ni utamaduni au ni umasikini? Ufugaji huria ni utamaduni au ni umasikini/uharibifu wa mazingira (ssina uhakika kama mbogo na swala na punda milia wanalaumiwa kwa hili pia maana tunataka waongezeke kwa wingi na kupunguza hawa wakwetu wa asili, tuongeze wa kigeni na kufuga kwa "kisiasa")? Je Kuvaa Rubega (Uhuru wa kuvaa na kuvua na kumudu hali zote za hewa) ni utamaduni au ni kupitwa na wakati? Ngoma zetu za asili zina kasoro gani? Ngoma za wenzetu zenye technolojia ya komputa zina kasoro gani? Ni kipi kinadumishwa kwa sasa? Kwanini?

  Je kwa sasasa nhi yetu iko huru? Uhuru wa kisasa? Kiuchumi? Kiutamaduni? Au tuko utumwani kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni? Nani ndivyo nani ni mkoloni? Kama sivyo, nini tunachojivunia kujitawala?
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Prof,
  Umekuja na topic nzuri. Juzi nilikuwa nasoma juu ya Mongolia. Raia wengi wa nchi hii ambayo ni kama jangwa la baridi ni wafugaji. Lakini katika miaka ya karibuni yamegunduliwa madini huko na Russia, China na hata Marekani wanapiga hodi, kama unakumbuka Hillary Clinton alikuwa huko karibuni. Kitu kilichonivutia ni lugha aliyotumia kiongozi wao ambaye ni American educated. Kuna kitu aliita "resource nationalism" yaani kuhakikisha kuwa madini waliyo nayo yana transform si Mongolia peke yake bali pia maisha ya raia wake. Kwa hiyo hivi sasa wanafanya mikataba ambayo itasaidia kubadilisha hali ya maisha katika nchi hii ya jangwa la barafu. Maybe we can learn from them.
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mabadiliko yanayotakiwa Tanzania, na nchi nyingine yoyote ambayo raia wake wanahangaika kila siku kama ilivyo Tanzania leo ni ya aina moja tu: UTAMADUNI.

  Ni lazima tujenge utamaduni imara unaowaona viongozi kama watumishi wa umma badala ya kuwaona kama miungun watu; halafu utamaduni wetu uwe wa kuheshimu na kuogopa sheria tunazojiwekea. Sasa chini ya utamaduni huo tutajiwekea sheria zinazohusu uchumi wetu na siasa za nchi tukazifuata.

  Tanzania ya leo ambapo bado tuna utamaduni wa kushangilia upuuzi wote unaofanywa na vigogo wa serikali, na kuwapongeza wanaoiba au kuuza mali za umma kwa manufaa yao binafsi haiwezi kunufaika chochote kutokana na mabadiliko ya aina yoyote ile ya kiuchumi au kisiasa. Tulipofanya mabadiliko ya kisiasa miaka 20 iliyopita kutoka one party system kuwa multi-party system bila kubadilisha utamaduni wetu hatukunufaika na lolote kama nchi kwa muda mrefu sana mpaka pale wananchi walipoanza kubadilika kiutamaduni pole pole.
   
 4. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Profesa.
  Mimi naomba niongeze swali,je kweli tunataka au tunahitaji mabadiliko? Tuna nia ya dhati katika hili? Tunalenga kupata nini katika hayo mabadiliko? Na je tukijua lengo tunaweza kuchagua njia ya kufikia hayo mabadiliko na tukachagua kama the end will justify our means or our means will justify the end?
  Katika hayo yote,kwangu mimi naona mabadiliko makubwa tunayoyahitaji( sio tunayoyataka) ni mabadiliko ya FIKRA, FIKRA SAHIHI zitatupeleka kwenye mabadiliko chanya na zitatusaidia kujua maana na thamani ya UTU. Na njia pekee ya kuleta mabadiliko sahihi ya FIKRA ni ELIMU bora.
   
 5. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Kabla hatujaangalia ni mabadiriko yanamna gani tunayataka tungezungumzia mabadiriko kwanza, tunahitaji kubadirika? ni lazima wote tubadirike?
   
 6. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Pamoja sana Mkuu Kichuguu:
  Strong CULTURE shapes Uchumi na Siasa, lakini ni kazi sana kwa Uchumi ama Siasa imara ku-shape Utamaduni, Tamaduni mbovu ni sumu kwa Uchumi na Siasa imara! Namaanisha hivi :- Tukiwa na Tamaduni imara tutafikia Siasa na Uchumi imara! Lakini hatuwezi kufikia Uchumi ama Siasa imara kama tu hatuna utamaduni imara kwanza! Na tukumbuke kuwa Utamaduni ni MAHUSIANO ndani ya FIKRA zetu juu ya UCHUMI na SIASA! Hapa ndipo tunapopata Fikra Huru au Utumwa wa Kifikra!
  Ni sahihi kabisa kama alivyosema Mkuu Morinho, mara zote ELIMU inabaki kuwa mkombozi wa binadamu! Na tukumbuke Elimu si kumaliza vidato na kujaza vyeti lukuki kwenye masanduku kama ilivyo leo, bali ELIMU ni Uwezo wa mtu KUTAMBUA JAMBO, KULIMENG'ENYA, MWISHOWE KULIFANYIA MAAMUZI SAHIHI+UTEKELEZAJI/KUCHUKUA HATUA STAHIKI! Hiyo ndio tafsiri ya elimu inayoweza Kumkomboa mtu!
  Uwezo huo unajengwa ama pia kujijenga wenyewe fikrani! Binafsi naamini vitu vitatu katika kujenga Utamaduni imara, SANAA, HABARI, na SHULE. Hizo ndio nyenzo kuu za kubadilisha FIKRA zetu kufikia mabadiliko tunayoyataka!
  Ni muhimu pia tukaafikiana wapi tunapotaka mabadiliko yatufikishe...ili tujenge msingi kama njia ya kutufikisha huko tunakota!
  Binafsi kama alivyodokeza Mkuu Morinho, kufikia siasa, uchumi na utamaduni(ndio maisha yenyewe) unapothamini THAMANI YA UTU ndio mabadiliko SAHIHI tupasayo kuyapigania. UTU ndio kipimo cha Maendeleo kwa MTU MWEUSI!
  UTU ndio MANTIKI KUU na ndio ELIMU MAMA!
  Mungu wetu anaita sasa!
   
 7. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kichuguu.
  Naomba kuuliza kidogo, hivi Utamaduni ni nini? Utamaduni wa Mtanzania ni upi? Unawezaje kuubadili utamaduni na kwa muda gani?
   
 8. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #8
  Nov 14, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kwa mtazamo wangu TATIZO kubwa ambalo pia linachangia matatizo katika jamii yetu ni Jamii ya Tanzania pia… Yaani sisi kama wananchi. Kwa kiasi kikubwa wengi wetu tunadhani kuwa viongozi wakiwajibika na kubadilika ipasavyo basi inatosha; swala ambalo sio kweli. Tukitata mabadiliko ya Dhati na Kweli katika jamii yetu tuelewe kuwa kila mmoja wetu (Iwe Viongozi ama Wananchi) wote tunatikiwa kubadilika for the better mana tumekuwa wote vimeo ikija katika uzalendo kwa inchi yetu.

  Mabadiiko yanahitajika kwa kiasi kikubwa na karibu katika kila entity ambayo inagusa taasisi yoyote ile iwe kwa level ya familia ama serkali. Kutafuta na kuhaha nini kibadilike katika list ya vinavyotakiwa kubadilika haisaidii.. Tumefika mahala ambapo karibu kila mahala pameoza na pana chechemea. Dawa pekee ni kuangalia ni yepi msingi yanayotakiwa kubadilika ili kuwezesha kila penye kuhitaji mabadiliko pabadilike na kuwa bora zaidi.
   
Loading...