Tunataka kufanya siasa kwa mujibu wa sheria siyo kwa katazo haramu

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
TUNATAKA KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA KILA MAHALI. LAKINI HATUTASUBIRI KUFANYA SIASA KILA MAHALI KWA SABABU SIASA IPO KILA MAHALI ( POLITICS IS EVERYWHERE)

Na Mwl, John Pambalu

Katazo la kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa kila mahali linakuja likiwa kinyume kabisa na Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Katazo hilo lipo kinyume cha sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.

Katazo hilo liko kinyume kabisa na misingi ya siasa ya kidemokrasia iliyoimarika na kustaarabika.

Katazo hilo linakuja likiwa na lengo la kupoteza kabisa uhuru na haki ya vyama vya siasa kufikisha elimu ya uraia kwa wananchi ili wasiwe na uwezo wa kuwahoji watendaji na wawakilishi wa serikali na wananchi.

Wakati wanasiasa wakikatazwa kukutana na wananchi mahali popote watakapotaka na kwa wakati wowote kwenye shughuli za kisiasa. Waliofanya hivyo wamefanya makusudi kabisa wakiamini kwa kufanya hivyo watazima au kutokomeza kabisa ushindani wa siasa za hoja nchini.

Waliofanya hivyo wamefanya huku wakisahau kabisa kuwa wanaweza wakazuia shughuli za kisiasa na wakashindwa kuizuia siasa.

Wamefanya hivyo huku wakisahau kabisa mwanafalsafa *Aristotle* Alishawahi kusema mwanadamu ni mnyama wa kisiasa *A human being is a political animal*

Nimeamua kuandika andiko hili nikikumbuka wimbo wa *LUCKY DOUBLE* wimbo unaoitwa *Reggae strong*

*Double* anasema

"Reggae in the bathroom
Reggae in the bedroom
Reggae everywhere
Reggae in jail, reggae in church
Everybody likes it
They tried to kill it"

*Double* anasema rege bafuni, rege kitandani, rege kila mahali. Rege jela, rege kanisani, kila mtu anapenda rege.

Wimbo huu utufumbue macho kuwa mwanadamu ni kiumbe wa kisiasa. Ndio maana walivyozuia mikutano ya hadhara. Kwenye mabasi siasa ikapigwa, wakazuia madhabahuni siasa ikapigwa wakazuia, misibani siasa ikapigwa, labda wazuie shunguli za mazishi hata kwenye kahawa siasa ipo tu.

Wakati wa ukoloni walizuia shughuli za kisiasa, wakawafunga wanasiasa lakini siasa ilipigwa.

Wakati wa ukoloni waliwaua wanasiasa, kuanzia tu kwenye mazishi yao siasa ikaanzia hapo.

Walitumia jela, risasi, bakora na kila namna ya unyama walioona utawalinda lakini haikuzuia siasa.

Simama kijana acha kulalamika *Patrick Ole Sosopi* MWENYEKITI WA BAVICHA TAIFA ANASEMA *TO BE IS TO DO*

Rais up. Simama piga kelele dai *Katiba mpya* *Haki za Binadamu* *Uhuru wa vyombo vya habari* *Utawala unaojali Demokrasia na utawala bora* rais up.


Mwl, John Pambalu
Makamu mkt Bavicha Tanzania bara
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom