Tunatafakari athari za uamuzi wa kuwachulia hose na mwanyika kwa familia zao-ikulu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunatafakari athari za uamuzi wa kuwachulia hose na mwanyika kwa familia zao-ikulu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Augustoons, Aug 31, 2008.

 1. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Richmond:Ikulu yatoa tamko hatima ya Dkt. Hosea, Mwanyika

  Na Timu ya Majira Jumapili

  SIKU chache baada ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kuwasilisha Bungeni taarifa ya Serikali juu ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kufuatia kashfa ya kampuni tata ya Richmond na kubainisha kuwa vigogo kadhaa Serikali waliohusishwa na kashfa hiyo hatIma yao iko ngazi za juu, Ikulu imetoa tamko rasmi.

  Miongoni mwa vigogo ambao Bunge liliarifiwa kuwa majaliwa ya ajira zao yako mikononi mwa aidha Rais Jakaya Kikwete mwenyewe au Katibu Kiongozi Ikulu, Bw. Phillemon Luhanjo ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dkt. Edward Hosea, Mwanasheria Mkuu, Bw. Johnson Mwanyika na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Arthur Mwakapugi.

  Ikulu jana imetoa msimamo wake kwa mara ya kwanza juu ya kinachoendelea baada ya kuachiwa dhamana ya uamuzi juu ya vigogo hao.

  Bw. Luhanjo hata hivyo alikwepa swali lililomtaka athibitishe iwapo ofisi yake imekwishapokea maelezo ya utetezi kutoka kwa maofisa hao wote na hatua ambazo itazichukua.

  "Kwani Waziri (Waziri Mkuu) alisemaje? Alisema wamewasilisha maelezo yao kwa kamati ya nidhamu."

  Akiwasilisha ripoti hiyo Bungeni Alhamisi wiki hii, Bw. Pinda akizungumzia suala vigogo hao kwa nyakati tofauti katika ripoti yake alisema: "Ili kutekeleza Azimio hili, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amepelekewa barua ya kutakiwa kujieleza na Mamlaka yake ya Nidhamu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi.

  "...Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa miongoni mwa Watendaji Wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali, suala lake la kuhusishwa kwake katika mchakato mzima wa mkataba huo linashughulikiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu.

  "Bwana Mwakapugi amekwishawasilisha maelezo yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ndiye Mamlaka yake ya nidhamu katika muda uliotakiwa."

  Bw. Luhanjo hakutaka kuingia kwa undani kuhusu muda ambao Ikulu itachukua kabla ya kutoa uamuzi wake juu ya vigogo hao.

  *Habari hii imeandikwa na Said Mwishehe na Reuben Kagaruki. Wadau wangu hebu tujadili.

  SWALI:Hivi ni watumishi wangapi wa serikali ambao wamekwisha fukuzwa kazi au kusimamishwa kazi pending investigation ambao serikali kwa kutumia mkigezo hicho hapo juu ilifikiria maisha yao na ya familia yao baada ya kupoteza kazi? Hivi wadau mlipofukuzwa pale udsm kwa kupewa masaa mawili muondoke hali hamjui kwa kwenda,wengine kwao tandahimba hawana hata ndugu dar,uukiachilia mbali nauli,je serikali ilipata muda wa kufikiria uamuzi wwake wa kuwatimua kwa masaa 2?Yule Mhasibu kule mbinga aliyehukumiwa miaka 240 jela je,uamuzi wa kumfikisha mahakamani ulifikiria athari zake kwa maisha yake na familia yake?Hivi kwa nini hawa wenzetu wanapata fursa hii ambayo ndugu zetu,wazazi wetu,rafiki zetu nk wanaikosa?Yaani hata kule kusema wasimamishwe kazi pending uthibitisho wa tuhuma zao nalo gumu?are these people very bright such that pale TAKUKURU au AG chambers hakuna mtu anayeweza kukasimu nafasi zao wakati wao wamesimamishwa pending investigation?Wanachi wangapi wamedhalilishwa kwa kusimamishwa kazi pending investigation na baada ya kuwa cleared na tuhuma wakarudishwa kazini?Endapo hii ni due process ya sheria kwa nini watendewe wale tu na wale wasitendewe?

  Hali hii inaashiria nini?
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..inamaanisha kwamba, "kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe"!
   
 3. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  HII NI NCHI YA AJABU NA VIONGOZI WA AJABU!
  Naam, wadanganyika wanaendelea kudhihirishiwa kuwa wao si lolote wala chochote zaid ya kufanya lile tukio jema la kuigiza la kuwaweka watu madarakan kwa sanduku la kura then, waendelee kula vyao, na wapiga kura waendelee kutaabika, mambo ya ajabu kabisa!

  Hiyo ndio hali dhahiri kuwa katika nchi ambayo tulio wengi tunaonekana ni wajinga wa mwisho, sjui wa kwanza katika kufikiri, ndipo wanapoonekana wateule na watakatifu wachache ambao wakiboronga lazima kuchukuliwa hatua wao ni kama kupandisha maji kilelen au ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!

  Lakin kutukuzana kwa watu wachache kutaisha lini? ipo siku pale wajinga wengi waliwao watajua jinsi walivyokuwa wakifanywa misukule huku wakiwa na akili zao wengine na degree kedekede za darasani, haya tuone!
   
 4. K

  Keil JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2008
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi Rais huwa ana kamati ya nidhamu ya kujadili wateule wake? Hiyo kamati ya nidhani ina watu gani humo ndani?

  Ikulu imeanza kujichanganya na hakuna hata mmoja ambaye ataguswa kwa kuwa hao watendaji ambao wanatakiwa kushughulikiwa na Ikulu wana details zote na walifanya kazi kwa maelekezo kutoka aidha Ikulu ama PMO. PMO haiwezi kufanya kitu bila ridhaa ya Ikulu na ndiyo maana Mwanyika aling'aka akasema hajiuzulu.

  Msabaha, Karamagi na Lowassa walijiuzulu kwa kuwa walikuwa wanashikilia nafasi za kisiasa, vinginevyo hata nao wasingejiuzulu.

  Iko kwenye rekodi JK aliwaambia waandishi wa habari kwamba baada ya kusikia minong'ono kwamba Richmond ni bomu aliita faili na kusitisha kila kitu mpaka pale Ikulu ilipojiridhisha kwamba Richmond ilikuwa ni safi. Swali ni kwamba je, ni nani aliyei-clear richmond? Ni chombo kipi cha dola kilichotumika kui-clear hiyo Richmond?

  Jibu la Mwanyika kugoma kujiuzulu lilikuwa na msg nzito na hata kitendo cha Hoseah kuendelea kuwa ofisini ni msg kwamba wao walikuwa wanafanya kazi kwa maelekezo kutoka juu. Haiwezekani surbodinate atumwe afanye hiki halafu kesho uje umrudi wakati ana siri zote. Ukimrudi tu lazima atakumaliza na hilo ndilo linalomtisha JK.

  Hao wakuu tusubiri aidha miaka yako ya uteule iishe halafu wawekwe kando ama kuhamishwa kutoka hapo na kupelekwa sehemu nyingine. Hakuna atakayefukuzwa kazi waka kusimamishwa kazi.

  JK anatesa na anafanya hayo madudu kwa kuwa anajua kwamba upinzania imara haupo na hata walio ndani ya CCM ambao wanapiga vita ufisadi huwa wakiwa na nidhamu ya chama na ndio maana kelele zao hazisikiki kwenye NEC wala CC.

  Wenye NEC na CC ndiyo mafisadi wenyewe, sasa utaanzaje kumwambia mwenyekiti wako wa chama kwamba ni fisadi na akakusikiliza? Unawezaje kumwambia mjumbe wa NEC ni fisadi na wakati ufisadi alioufanya ulimuwezesha mwenyekiti wenu kuwa Rais?
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hii kali sijawahi sikia popote....vipi Kasusura hakuwa na familia na watu wanaomtegemea? Huyu tajiri aliyefungwa na Putin, Mikhail Khodorkovsky hakuwa na familia mzee Luhanjo huna tofauti kabisa na Makamba ama Kingunge Mwiru!!
   
 6. M

  Mulugwanza Member

  #6
  Aug 31, 2008
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 89
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Luhanjo ametia aibu, ameonyesha jinsi gani serikali ya jk isivyokuwa na nidhamu kwa wananchi wake. Angejua angenyamaza tu kuliko kuongea maneno ambayo hayana msingi wowote. Waandishi walitakiwa kumuuliza bw luhanjo kuwa inamaana watu wote ambao walishawahi kufukuzwa kazi na serikali yake wakiwemo jamaa wa bot hawakuwa na familia? Jamani viongozi wetu mbona mnakosa nidhamu kiasi hiki?
   
 7. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  UTAWALA WA SHERIA HAUPO TANZANIA:
  Hii inaonyesha hakuna Rule of Law and Good governance hapa Tanzania. Principles zilizowekwa bayana kwenye " The animal Firm" ndo zinazoapply. Nini cha kufanya? Tunachotakiwa kufanya ni kuuelimisha umma kuhusu uozo wa serikali ya JK na group yake ya NEC/CC ya CCM make hawa ndo chanzo cha ubakaji wa rule of law and good gorvernance as I may quote Obam's slogan " Yes we can, change we believe in" and " 2005-2010 is enough" Naomba kuwakilisha
   
 8. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kinachonishangaza mimi,katika kanuni za utumishi wa umma,moja ya makosa yanayomfukuzisha au kumsimamisha kazi mtu ni pamoja na gross negligence,negligence na recklessness au laxity ya kutake action na hivyo kumfanya boss aingie hasara.Kitu kingine pia kinachoweza kumfukuzisha kazi kinachotokana na huohuo uzembe kinaitwa professional negligence,hiki huwakumba sana watu wenye taaluma fulani,mathalani wahandisi,wanasheria,madaktari nk.Aidha ukisoma code of conduct ya wafanyakazi wa TRA kama mfano tu,inatamka wazi kuwa gross nengligence ni moja ya makosa yanayomfukuzisha mtu kazi.Vivyo hivyo watu wengi wamekumbwa na kigezo hiki humo makazini kwa sababu moja hadi nyingine.Mathalani moja ya kesi iliyopo mahakama ya kazi hapo dara na haijaisha inahusu mtu aliyefukuzwa kazi kwa kosa la yeye kukamata gari lililokuwa na mzigo usiolipiwa ushuru na kuliweka kwenye bonded warehouse na hatimaye wakati wa kuwasilisha ripoti,mkuu wake wa kazi alimwamuru aliachilie na yeye alinukuu Bond number tofauti tena kwa human errors tu katika kufile taarifa yake.Wafanyakazi hawa na wengine wanasota kusubiri hatima zao mahakamani,wametoka katika kutembelea magari ya kifahari hadi daladala na saa nyingine kwa mguu,watoto hawaendi shule kama inavyotakiwa nk.

  Lakini hawa wenzetu huko serikalini tunaambiwa kuna athari kubwa sana kwao na kwa familia zao,wakifukuzwa kazi.Wakuu wana jf,hivi niambieni ni watu wangapi pale mahakamani kabla hakimu hajapitisha hukumu huwapa nafasi ya kujitetea na wao wakajitetea kwamba kosa ni la kwanza au mama zao wagonjwa au familia zao zinawategemea lakini mahakama hutupilia mbali sababu hizo na kusema,"kama ulijua hayo kwa nini ulitenda kosa?ungewahurumia watoto wako kwa kutotenda kosa". Isitoshe katika makosa ya jinai ipo falsafa inayosema "the man anticipates the consequences of his actions when committing an offence".Tujiulize tena, hivi ni fedheha gani au usumbufu gani na athari gani azipatazo mtu kama Balozi Mahalu aliyekuwa balozi wetu huko Italy ktk kesi inayoendelea pale Kisutu.Mbona yeye baada ya kutuhumiwa tu,alisimamishwa kazi pending investigation hadi leo.Hadileo yeye ni mtumishi wa umma anapokea nusu mshahara pending determination ya his case.Je hawa wenzetu wawili si wateuliwa wa Rais kama huyu balozi?

  Kwa kweli sasa hivi ile falsafa ya kusema "equality before the law" naona iko eroded. Kama Dar si Lamu alivyosema huku akiwa supported na warioba,hii ina maanisha kuwa sasa tumeanza kuwa na sheria za matabaka na kila mtu atajiju,hali ambayo ni mbaya sana inaweza kuleta anarchy katika jamii ambapo ni kazi ya sheria kuzuia.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Aug 31, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  Augustoons,Ushirombo,Dar-Si-Lamu,

  ..Prof.Mahalu alijifanya mjanja kwa kuiba halafu hakwenda kuchangia kampeni za wanamtandao. he was being too ndependent. ndiyo maana leo yuko matatani.

  ..Mwanyika,Hosea,Mwakapugi,Mrindoko,Msabaha,... walikuwa wakitekeleza maagizo ya wakubwa zao.

  ..kumbukeni ile kauli ya Msabaha kusema kwamba yeye ni bangusilo tu. yaani ametolewa kafara kwa maamuzi ya wengine.

  ..Mwakyembe alidai maagizo ya baraza la mawaziri yalikuwa yakikiukwa. sasa nani aliyetoa baraka za maagizo hayo kukiukwa kuhusu suala la Richmond?

  ..pia Mwakyembe alidai kuna mambo hakuyasema ili kulinda heshima ya serikali. sasa ni mambo gani hayo? ni kina nani ambao hakuwataja ili kulinda heshima?
   
 10. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2008
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  sasa jaribu tafakari ukweli ufuatao......DALADALA za Luhanjo hunyoyeshwa mafuta na TAKUKURU. Wanatumia kituo kimoja. Dezo la mafuta kwa Luhanjo!!!! Sasa cha ajabu nini???
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Kwamba fisadi kamwe hawezi kupambana na fisadi mwenzake. Kiongozi mjasiri katika kupambana na ufisadi kamwe hufikirii familia ya fisadi itaathirika vipi pindi akifukuzwa kazi kwa ufisadi alioufanya. Wanajua fika kwamba wengi ndani ya serikali akiwemo JK mwenyewe ni mafisadi hivyo kuwashughulikia Hosea na Mwanyika kunaweza kuwafanya wakaamua kuongea hadharani uozo wote uliojaa serikalini maana wanayajua mengi. Na wakiamua kuongea basi itakuwa patashika nguo kuchanika.
   
 12. O

  Ogah JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Luhanjo........

  ............wala huna haja ya kuzunguka m-buyu...Ngoja nikusaidie kidogo..........ktk hili

  ........kwa kuwa unazungumzia ubinadamu....i.e affairs za familia zao........ok......Just semeni tumewastaafisha Dkt Hosea, Mh Mwanyika na Arthur Mwakapugi kwa manufaa ya UMMA.....period!

  .....mbona huko nyuma wengi tu wamestaafishwa kwa maslahi ya umma.......hakuna jipya hapa.........na asionewe mtu haya
   
 13. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Quote:
  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Bw. Luhanjo alisema Serikali haitaki kukurupuka juu ya hatima ya akina Hosea, Mwanyika na Mwakapugi akisema ni suala zito linalogusa maisha ya watu na familia zao.
  "Suala hili tunalishughulikia, unaposhughulikia maisha ya mtu haustahili kutoa uamuzi wa kukurupuka...tunashughulikia, hatukurupuki," alisema na kuashiria kuwa kwa sasa kazi iliyoko mbele yao ni kupima uzito na athari za kila uamuzi utakaofanyika.
  "Kabla ya kutoa uamuzi lazima upime kwanza na sio kukurupuka...Hebu fikiria ungekuwa wewe mtu anakuhukumu kufungwa kwa kukurupuka, familia yako na wewe mwenyewe mtaathirika kwa kiasi gani? alihoji.


  Hizi kauli za Luhanjo ni matusi na kwa walalahoi ambao wangeweza kupata huduma bora za jamii kwa mamilioni yaliyoteketea kwenye hili kanyaboya la Richmond. Ina maana hao kina Hosea, Mwakapungi na Mwanyika hawakuliona suala la Richmond kuwa ni zito na linagusa maisha ya watu na familia zao? Mbona walitoa maamuzi yao kwa kurupuka bila kupima?Au ndio mkuki kwa nguruwe.....?
   
 14. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Duh, mkuu kumbe huyu chief anamiliki hadi madaladala?hii kali kwa kweli,ni kioja hicho kwa yeye kupewa mafuta na TAKUKURU.The man is so silent like not a business man,hebu tupe clues zaidi.
   
Loading...