Tunasubiri Nchi Wahisani Waje WATUAMURU Hatua za Kuchukua Kwenye Wizi?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,879
2,000
Mkakati wa CCM wa kuwaokoa wezi katika sakata hili la akaunti ya Escrow utatuaibisha kama taifa huko tuendako. Wahisani walisitisha misaada yao ya Kibajeti kwa Tanzania hadi scandal hii ishughulikiwe. Hii inamaana hata ukweli wanaujua ila hatua za kuchukua ni juu ya Bunge na serikali yetu wenyewe
Sasa nafasi hiyo imepatikana lakini kwa mastajabu ya wengi ni kuwa sasa kuna mkakati wa kuwatetea wahusika. Tunajua wazi kuwa hizo fedha za wahisani ni kodi za watu wao sasa kama tunalia shida lakini fedha zetu zinatafunwa tunachekelea basi watakuja na option mbaya sana kwetu kwamba kama hamchukui hatua kwa huyu na yule basi hamna sababu ya kuwapa misaada hii na ile. JEE HILI NDIO WATANZANIA TUMEWATUMA WABUNGE WETU? KWAMBA KUCHUKUA HATUA MPAKA TUSHINIKIZWE NA WAHISANI
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Huo wizi uko wapi, mnabwabwaja na kuhororoja wakati hakuna mahali panapoonesha pameibiwa.

Mlitaka umeme wa bure?
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
7,590
2,000
Huo wizi uko wapi, mnabwabwaja na kuhororoja wakati hakuna mahali panapoonesha pameibiwa.

Mlitaka umeme wa bure?
Ile mahakama ya kimataifa imeleta barua kuwa Tanesco wakokotoe upya deni wanaloidai IPTL, siku 90 zilishapita kwa nini hawakokotoi upya sasa ili hizo pesa za IPTL zilirudishwe kwa Tanesco? TANESCO ni ya nani au ni kampuni mama ya singasinga, mnajikanyaga Kumbe fedha inayotakiwa kukokotolewa ilishaliwa zamani bila kujua ya TRA NI ipi na ya TANESCO ni ipi. Dah hivi hii nchi nibyetu sote je sisi tusio wezi tungekuwa wahamiaji ingekuwaje?
 

wooden flag

JF-Expert Member
Oct 12, 2014
958
1,000
Salamu za kutosha
Wanajamvi wote na wapenda TZ kutakuwa na maandamano makubwa kwa lengo la kuitaka serikali kurudisha fedha zilizoibwa kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL. Na tutaenda Tanesco makao makuu kulitaka shirika hili lishushe bei ya umeme.
SEHEMU YA KUKUTANA
Kwa wakazi Wa dar tutakutana kituo kipya cha daladala cha mawasiliano na tutapiga kambi Tanesco makao makuu pale ubungo.
WAHUSIKA
1. Wote wanaokererwa na bei ya umeme hasa pale unapopata unit 8 utoapo buku kumi.
2. Wote ambao ndugu zao tayari wamepoteza maisha kwa kukosa dawa hospital
3. Vijana wote waliokosa Mkopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu.
4. Wote waliopoteza wake zao kipindi cha kujifungua kutokana na huduma mbovu hospital
5. Wote wanaokerwa na foleni barabarani wakati wezi wakitaka kwenda sehemu barabara zinafungwa
6. Wana mageuzi wote.

Coordinator Wa maandamano :
wooden flag
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,879
2,000
Huo wizi uko wapi, mnabwabwaja na kuhororoja wakati hakuna mahali panapoonesha pameibiwa.

Mlitaka umeme wa bure?
Kwa hiyo kwa uelewa wako ni kuwa miaka yote umeme ulikuwa haulipiwi? Hilo ndilo hata wale wabunge wa CCM kule Dodoma hawalielewi, wao wanadhani malipo hayo ni ya umeme uliotumika. Kweli usilolijua ni bora unyamaze.
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Ile mahakama ya kimataifa imeleta barua kuwa Tanesco wakokotoe upya deni wanaloidai IPTL, siku 90 zilishapita kwa nini hawakokotoi upya sasa ili hizo pesa za IPTL zilirudishwe kwa Tanesco? Kumbe fedha inayotakiwa kukokotolewa ilishaliwa zamani. Dah hivi hii nchi nibyetu sote je sisi tusio wezi tungekuwa wahamiaji ingekuwaje?
Hizo ni recommendations, wakokotoe, walikatazwa?

Lakini si kwa 50 aliyoisema Zitto, yaani ule ni ujuha wa hali ya juu. Hata mtoto mdogo atamcheka, kuna mtambo wa kufua 100MW za umeme kwa 50,000?
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Kwa hiyo kwa uelewa wako ni kuwa miaka yote umeme ulikuwa haulipiwi? Hilo ndilo hata wale wabunge wa CCM kule Dodoma hawalielewi, wao wanadhani malipo hayo ni ya umeme uliotumika. Kweli usilolijua ni bora unyamaze.
Wewe wacha porojo, fedha za IPTL zilikuwa zinapelkwa account ya escrow kuanzia mwaka 2004 na msimamizi wa shughuli hizo wakati wa mgogoro wa IPTL na TANESCO alikuwa ni RITA, sijuwi ni nini usichokielewa hapo?
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
7,590
2,000
Hizo ni recommendations, wakokotoe, walikatazwa?

Lakini si kwa 50 aliyoisema Zitto, yaani ule ni ujuha wa hali ya juu. Hata mtoto mdogo atamcheka, kuna mtambo wa kufua 100MW za umeme kwa 50,000?
Kwa akili za Viongozi wa ccm watashindwa nn kuuza hapa Tanzania kwa bei wanayoitaka?
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,879
2,000
Onesha huo wizi uko wapi? kwa ushahidi si kubwabwaja bila mpango.
Kwanza usiniambie nabwabwaja. Kutuo fedha bila kufuata taratibu zilizowekwa kisheria huo nao ni wizi hata kama ni zako. Weka milioni mia CRDB kisha nenda kavunje utoe hizo hizo mia zako bado huo utakuwa wizi.
Kwenye Escrow umeshaambiwa bado ruksa ya kutoa fedha iliyotolewa na AG ilisema pia hakuna kodi wakati 30bil zilipaswa kutozwa hazikutozwa nao sii wizi?
 

lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
21,199
2,000
Waulize Tanesco walipozipeleka escrow zilikuwa za nini.
Kuna malipo ya aina mbili ambayo TANESCO wanakatwa kwenye mkataba wa IPTL....

1. Gharama za ununuzi Wa umeme (kwa unit) hizi hazikua na mgogoro na TANESCO wamekua wakinunua umeme unaozalishwa na kulipa bila shida.


2. Capacity charges ( gharama za uwekezaji) hizi IPTL izalishe ama isizalishe lazima walipe...

Katika fungu la 2 ndipo palipoibuka mgogoro kwamba TANESCO wamelalamika kutozwa zaidi ya gharama halisi.

Kabla ya kuendelea naomba tu nikwambie hela hizi hazihusiani na ubure Wa umeme kwakuwa TANESCO inanunua tena si kwa IPTL pekee wapo symbion aggreco songas etc....

Fedha inayoongelewa ni hiyo iliyokua na mgogoro ambapo wizara iliamuru ilipwe ktk kiza kinene na Shaka kubwa.....

PAP walilipwa fedha kabla ya kununua hisa za VIP na walilipa fedha za ununuzi Wa hisa kwa VIP Mara tu baada ya kulipwa mabilioni ya escrow sasa jiulize je PAP walipewaje PESA zote bila kununua kwanza hisa zote?

Pili ni kodi gavana Wa BOT aliuliza Mara nyingi juu ya tozo ya VAT akaambiwa hailipwi wakati kisheria ilipaswa ilipwe je huu si uhujumu??

Sijui Kama unachangia kwa utashi ama unatania lakini ishu hii itatugharimu Sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom