Tunasubiri mgao mwingine toka CCM

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Wengine wetu tuliingia katika uchaguzi,hadi kwenda kujipanga kupiga kura za maoni za CCM kwa kupewa Sh. 2,000 au Tshet, kanga, skaf au kofia zenye picha ya kikwete na kauli mbiu yake Nguvu zaidi...

Sasa uchaguzi umeisha na sh. 2,000 imeisha isha, tshet, kanga,kofia na skaf zimeanza kuchakaa hata kabla ya mwaka kuisha. Lakini tumewapa ulaji kwa miaka mitano. wengi wa hao tuliowachagua safari zao zitakuwa nyingi ifikapo 2015 kama sehemu ya kusafisha njia yao kwa ajili ya uchaguzi mwaka huo!!

Swali: Je mgao mwingine wa bidhaa hizo Utakuwa lini au mpaka 2015?
 
Magao wa umeme mwingine tena au ? Sasa hivi tuko kwenye mgao tayari, mafuta na bidhaa kibao bei juu ebo?
 
Mgao wa umeme mbona tayali umeanza! Hawa watu wananiboa!
 
It was once and for all mgawo; just wait and see kila mtu akichuka chake mapema kwa kasi before 2015; mgawo sasa ni kwa wale ambao waliochakachua uchaguzi na kujichukulia madaraka, kwa wale wachache waliorubuniwa kwa visenti na vitisheti, mmewasaidia wakubwa hao mmekubali kutumiwa....sasa wote we shall suffer consequence za kukubali to sell your freedom so cheaply....kilio kitakuwa cha walio wengi including walionunuliwa
 
Jamani

Hamjasiki MTERA. KIHANSI na KIDATU maji yamepungua.

Tuatajuta kuipigia CCM kura.

Dar hii ni wiki ya 3 kuna mgao wa Umeme na TANESCO hawajasema chochote kama vile HIWAHUSU.

Badra Masoud vipi mbona kimya sana wakati huu.............uliingia Tanesco kwa Bwebwe sasa hivi ....Maji yamekufika shingoni ama?..Tupe taarifa ni nini kimetokea mbona Dar kuna Mgao wa Umeme
 
Serikali imetuma waraka kwenye kampuni za madini(Migodi) kuwa haina umeme mpaka mwishoni wa december....Duuu
 
Jamani

Hamjasiki MTERA. KIHANSI na KIDATU maji yamepungua.

Tuatajuta kuipigia CCM kura.

Dar hii ni wiki ya 3 kuna mgao wa Umeme na TANESCO hawajasema chochote kama vile HIWAHUSU.

Badra Masoud vipi mbona kimya sana wakati huu.............uliingia Tanesco kwa Bwebwe sasa hivi ....Maji yamekufika shingoni ama?..Tupe taarifa ni nini kimetokea mbona Dar kuna Mgao wa Umeme

Hayo maeneo ambayo unasema hayana maji nipe jibu wakati wa kampeni maji yalitolewa wapi umeme ukawepo kuanzia kampeni zinaanza mpaka mkwere akaapishwa! sasa uchaguzi umeisha hatuna umeme TANESCO TUPENI MAJIBU!!!:thinking:
 
Shida ni TANESCO kuendelea kukumbatia chanzo cha aina moja kwa zaidi ya miaka 30 utadhani wamelogwa !
 
Nakumbuka wakati wa sakata la richmond mkuu alisema kuwa mgao utakuwa hadithi au ilikuwa ni kutafuta ujiko. Inasikitisha miaka 50 ya uhuru na karne hii bado swala la umeme ni kitendawili hivi viongozi wetu kweli wapo makini na hili kwani ni pesa ngapi inapotea kutokana na huu mgao?
 
Inakuaje uchaguzi umeisha na baraza limetangazwa sasa mgao wa umeme umerudi?...Itabidi wananchi tupigie kelele hii issue. It is unacceptable kwa serikali kufanya hivi.
 
jamani tuwape nafasi viongozi wetu 'tuliowachagua' wafanye kazi, tunadai nini wakati kumbe tumeshapewa kanga, skafu, flana, buku2, sabuni, pombe, pilau, tumepandishwa ktk magari bila nauli kwenda ktk mikutano, vocha, sigara, watz mnataka nini tena? au mnataka kuleta uvunjifu wa amani iliyojengwa? allaaa!
 
Kweli watz wakianza kudai hiki na kile, wataambiwa si tuliwapa .... hapo kwenye RED! Kimya.
 
Back
Top Bottom