Tunashughulikia afya ya Ngulume’ -UONGO MTUPU

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Tunashughulikia afya ya Ngulume’ Send to a friend Thursday, 11 November 2010 20:23 0diggsdigg

Raymond Kaminyoge

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imesema tatizo la ugonjwa wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, Hawa Ngulume imeanza kushughulikiwa na wizara kabla taarifa zake kuripotiwa na gazeti la Mwananchi.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja, alisema kinachofanyika sasa ni wizara hiyo kwa kushirikiana na familia yake wameanza taratibu ili wampeleke nje kutibiwa.
“ Wakati mwingine ni vizuri kutumia vyombo vya habari, lakini suala la Ngulume lilikuwa likishughulikiwa na wizara hata kabla hamjaandika taarifa zake, hivyo si kwamba tunalishughulikia baada ya kusoma gazetini, ” alisema.
Alisema tatizo ni kwamba wanaotakiwa kuidhinisha rufaa za wagonjwa, wanaotakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi ni madaktari watatu kutoka katika hospitali ya Muhimbili.

“ Sasa kama mgonjwa alikuwa akitibiwa kwenye hospitali binafsi, na rufaa inatakiwa itoke katika hospitali ya Muhimbili, unakuta kuna ucheleweshaji katika suala hilo kwa kuwa ni lazima taratibu zifuatwe,” alisema.

Akizungumza kwa simu jana, Ngulume alisema bado anaendelea kusikia maumivu makali hali inayosababisha ashindwe kulala usiku kucha.

“ Binti yangu amekwenda Wizara ya Afya kufuatilia suala hilo, hata hivyo bado sijafahamu ni lini nitafanikiwa kupelekwa nje kwa ajili ya vipimo na matibabu,”alisema.

Jumapili iliyopita, Ngulume, alizungumza na Mwananchi akiwa nyumbani kwake Goba Kinzudi, kuelezea hali ya afya yake, akiwa hoi kitandani akisumbuliwa na maradhi ya vichomi na mapafu.

Alisema kwa miezi mitatu sasa, amekuwa hoi kiasi cha kushindwa kutembea bila kusaidiwa na kuiomba serikali imsaidie kwenda kutibiwa nje ya nchi.

HAWA WATU JAMANI NI WAUAJI MAJUZI NILIKUWA NA MSHIKAJI TUKAENDA KWA HUYU MAMA ANATIA HURUMA KWA KWELI HAWA MASHETAN WANADANGANYA ANASHUGULIKIWA KABLA YA KUJA MAGAZETINI MAMA ANGEKUWA MJINGA KUOMBA MSAADA KWENYE MAGAZETI GOV DONT B STPD LIKE THAT
 
Back
Top Bottom