Dangire
JF-Expert Member
- Oct 5, 2011
- 221
- 68
dakika chache zijazo ntatoka ofisini(mitaa ya mwenge dsm) kuelekea hom, mawazo yamenijaa ni jinsi gani nitapata gari za mbagala. shida ni kubwa sana kupata usafiri. tatizo kubwa zaidi ni jinsi gani nitaweza kupanda kwenye gari bila kashkash? hata lini tutaendelea na hii ''survival for the fittest?" ........serikali kweli inashindwa kuiongoza jamii kuwa na utaratibu wa kupanga foleni (kila mtu anapofika kituo cha anakoelekea)?
hivi hii si ingesaidia watu wote kuuona usafiri wa daladala kuwa ni usafiri bora na ni wa kila mtu? hivi hata wenye magari binafsi wanaoongeza foleni njiani si wangethubutu kuyaacha magari yao na kupanda daladla? lakini kwa hali hii......hakuna atakayesema aache kwenda mjini na 'private car' yake eti kwa kutegemea daladala. usafiri wa daladala hizi hapa jijini umekuwa ni moja ya kero zinazowakumba wakaazi wa dar.
hebu fikiria, mtoto (wanafunzi) anapataje nafasi kwenye gari kwa hali hii?
je, walemavu watapandaje usafiri huu katika hali hii?
je, wanawake wanawezaje kustahimili hali hii?
serikali ikumbuke kuwa wakaazi wa dar nao wana haki ya kusafiri kwa heshima (utu wao ulindwe). Ni lazima serikali iwajali watu wao....sio kweli kwamba watz tumezoea shida....huu ni uzembe tu wa watendaji kuhakikisha hata matatizo haya madogo madogo yanatatuliwa. yaani....badala ya kufurahia kuishi bongo, tunajikuta tunavumilia kuishi hapa. ukiamka asubuhi unawaza ni namna gani utapata usafiri....na jioni nayo tunaanza kuwaza namna ya kufika hom....kweli?
chonde chonde serikali na watendaji wote wa jiji tujengeeni ustaarabu wakazi wa dar ili tufurahie maisha.........