Tunashindwa magari ya kubebea wagonjwa tunaahidiwa laptops kwa kila mwanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunashindwa magari ya kubebea wagonjwa tunaahidiwa laptops kwa kila mwanafunzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Inkoskazi, Jun 30, 2010.

 1. I

  Inkoskazi Member

  #1
  Jun 30, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Serikali kumwaga pikipiki 400 kwa wajawazito

  na Salehe Mohamed, Dodoma

  SERIKALI imesema itanunua pikipiki 400 mwaka 2010/2011 kwa ajili ya kubebea wagonjwa ili kutekeleza Mpango wa Afya ya Mama na Mtoto.

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, alibainisha mpango huo alipokuwa akisoma hotuba ya bajeti ya wizara yake, ambako aliliomba Bunge limuidhinishie sh bilioni 448,442,515 kwa mwaka wa fedha 2010/2011.

  Profesa Mwakyusa alisema pikipiki hizo zitasambazwa kila mikoa na wilaya kulingana na utaratibu utakaowekwa na wizara yake, lakini watazingatia zaidi mahitaji ya eneo husika.

  Aidha, Waziri Mwakyusa alisema wanatarajiwa kusambaza vyandarua milioni 14.6 vyenye viatilifu, ili kupambana na ugonjwa wa malaria, sambamba na kushirikiana na wadau kuwezesha upatikanaji wa dawa mseto ya ugonjwa huo.

  Aliongeza kuwa wizara yake itaboresha upimaji wa vimelea vya malaria kwa kutumia kipimo cha haraka, katika vituo vya kutolea huduma za afya vya umma.

  Alisema katika mwaka wa fedha 2010/2011 wizara yake itaendeleza mpango wa kitaifa wa kupanua huduma za tiba kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, ambako idadi ya watakaopewa dawa itaongezeka kutoka 322,783 hadi kufikia 440,000.

  Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Omar KwaangÂ’, alisema kuwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), inashindwa kusambaza dawa na vifaa vingine vya tiba, kutokana na kudai deni la zaidi ya sh bilioni 36.

  Alisema, MSD haipaswi kulaumiwa kwa sababu haiwezi kufanya kazi kwa ufanisi, wakati inadai deni kubwa ambako kama fedha hizo zingelipwa mapema ingesaidia kuboresha huduma zinazotolewa na bohari hiyo.

  Katika hatua nyingine, kamati hiyo imeishauri serikali kufuta utaratibu wa kuruhusu baadhi ya mizigo ya wafanyabiashara kupita bandarini bila kukaguliwa, kwa kuwa wengine wasio waaminifu wamekuwa wakiitumia nafasi hiyo kuingiza dawa bandia. Aliongeza kuwa moja ya changamoto kubwa inayoikabili Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), ni kuwepo kwa njia nyingi za panya ambazo hutumika kupitisha bidhaa zisizokidhi viwango.

  Kamati hiyo pia imeishauri serikali iongeze kasi kwenye ukaguzi wa dawa za miti shamba, ambazo kwa sasa wananchi wengi wanazitumia bila kujua usalama wake na mkazo zaidi uwekwe kwenye zile za Kichina ambazo zinaonekana kuwa na madhara kwa wananchi.


  My take:
  Tutasikia vioja sana miaka hii toka kwa viongozi. Haya leo mama mja mzito ameshikwa na uchungu atabebwaje kwenye pikipiki???  "Moringe wote ni wamasai lakini sio kila mmasai ni Moringe"
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nadhani ni piki piki za kampeni!
   
 3. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,932
  Likes Received: 21,049
  Trophy Points: 280
  duh......hivi pikipiki inabebaje mgonjwa???
   
 4. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii yote ni kutokana na kufanyia maamuzi Dar-es-Salaam ndani ya ofisi zenye viyoyozi. ]
  Na kutembelea wananchi kwa magari makubwa yenye viyoyozi.
  Haya maamuzi yanaonekana wazi hayakuwashirikisha wadau wakuu, yaani akina mama waja-wazito.

  Labda kama hizo piki piki ziko katika mfumo wa bajaj au kakitu kama hako, lakini sitaki kufikiria jinsi mama mja-mzito atakavyo bebwa katika chombo chochote cha aina hii!!
   
 5. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,932
  Likes Received: 21,049
  Trophy Points: 280
  hii hata ukifanyia maamuzi ndani ya private jet.....its just common sense...pikipiki itabebaje mgonjwa??pata picha mgonjwa kapoteza fahamu...hata ikiwa bajaj na mwendo wa bajaj hadi kufika zahanati hyo mgonjwa si kashakuwa marehemu??
   
 6. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  BAJAJ BOB ziko ZA AINA NYINGI,.Bongo MIUNDOMBINU YETU BADO SIVYO,.NIKIMAANANISHA KUANZIA VIJIJINI ambako BARABARA ZAKE NI ZA KIASILI .,full mabonde na mashimo,..MJINI FOLENI ZA KUTOSHA MFANO UNATOKA MWANANYAMALA KUMUWAHISHA MAMA MJAMZITO MUHIMBILI ,.WAKATI WA FOLENI INAKUWAJE?KINGORA CHA AMBULANCE KITASAIDIA?BAJAJI INAWEZA KULA SHORT CUT./..NA ZIPO ZA AINA NYINGI CHINA nimeziona nyingine zinatumia usukanu kama wa gari,.hizo ni jembe ulaya na matairi ni matatu ,.hata kuwe na tope gani haziitaji msaada ,.na zinabeba uzito mkubwa,...TULIA hiyo program ianze halafu bisha ,.kwa unachokiona
   
 7. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
 8. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  bora kipi subiri picha na aina ya bajaji ndio utaelewa
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni one step forward, five steps backward. I hope generations mbili zijazozisione hiki kituko.
   
 10. MKANDYA

  MKANDYA Senior Member

  #10
  Jul 1, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi kweli hii inaingia akilini! Pikipiki kutoa huduma ya mama mjamzito anayehitaji msaada wa haraka kutokana na matatizo ya kujifungua. Hebu tuangalie Dar; mngojwa kapatwa na matatizo ya kujifungua (Obstructed labour) na yuko Zahanati ya Mbagala ana hamishiwa Temeke Hospitali ili apate huduma ya upasuaji kutoa mtoto.Huyu mama kwa matatizo aliyonayo kumsafirisha inabidi awe kwenye kitanda; pikipiki kitanda kitakaa je? Hata hizo bajaji mpya hazina nafasi ya kuweka kitanda cha mgonjwa. Pikipiki 400 gharama yake inatosha kununua magari zaidi ya 50 ya kubeba wagonjwa; hivyo basi ni heri kununua magari kuliko hizo pikipiki. Viongozi wetu wanatakiwa kuwa makini kuwasaidia watanzania. Na si kutudanya, na makigambo mengi kuwa pikipiki ni mkombozi kwa matatizo ya mama na mtoto.
   
 11. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Unajua, inabidi tuondokane na dhana kuwa ambulance ni gari/ chombo cha KUSAFIRISHA wagonjwa tu. Ambulance inatakiwa mle ndani iwe na vifaa vya huduma ya kwanza pia. Sasa kwenye pikipiki/ bajaj, hivi vifaa vitawekwa vipi? Kwa mfano tenki la oksijeni? Mlingoti wa kushikilia dripu na kadhalika. Tusiridhike na mipango ya daraja la 3 tunayoletewa na hii serikali. Sawa, sisi ni nchi maskini lakini je, mbona tuna uwezo wa kununua VX kwa karibia kila kiongozi wa serikali? Hizo ni ambulance ngapi 'za ukweli'?
   
 12. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Something is better than Nothing
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  hii ndio laana ya kujitakia....................
   
 14. consigliori

  consigliori JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  i am afraid, this is NOTHING. Huwezi beba mjamzito kwenye pikipiki, akitaka kujifungua njiani utakuwa na vifaa vya kumzalishia?
   
 15. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,932
  Likes Received: 21,049
  Trophy Points: 280
  mimi nasubiri nione hizo BAJAJ....kuna mtaalam humu anaitwa BAWA MWAMBA kasema tusubiri tuzione......sijui hio bajaj itakuwa na ukubwa gani kuweza kubeba hivyo vifaa na paramedics na mgonjwa......
   
 16. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
 17. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  883630.jpg haya ni majembe ulaya maarufu zaidi vijijini
   
 18. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hizo bajaj zina ukubwa tofauti na nguvu tofauti.,kama oda ni kubwa basi kiwandani wanapokea nyongeza ya specification,.huyo mitungi ya oksijen na stendi ya drip vitawekwa tu,..na zipo za aina nyingi mno

  KWA vijijini hali ni mbaya zaidi mzee,..BAISKELI NDIO ambulance ,.acheni kuifananisha bongo na ulaya,.bwana,.
  zambia kwa hilo hata zambia tutakuwa tumewapiga bao hembu link bbc uone majirani zetu wanatumia nini
  http://news.bbc.co.uk/2/hi/health/8319163.stm
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mambo ya ambulance ni ya wafadhili jamani, serikali ya CCM yenyewe ni kutafuta pesa, magari, pikipiki, simu na mambo ya campaign!!! hivi hamjui kazi ya donors???

  wao ndio waliotufanya tuwe maskini kwahiyo wao ndio walete hayo magari ya wagonjwa, sie ni kampeni tu, ala!!!
   
 20. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
Loading...