Tunashauri kutopinga kila kitu, Nampongeza Ridhione Kikwete kwa hili

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
Hoja sio Ridhiwani kukanusha ujumbe uliokuwa kwenye ukurasa wake... hapana, hoja ni huo ujumbe mzito alioutuma kwa Serikali ya chama chake (CCM) kama hujausoma hebu utafute haraka ili upate madini.

Vyovyote iwavyo ni sawa tu, kubwa hapa ni kwamba tayari SMS sent and derived. Alichokifanya Ridhiwani ni kutupa jiwe gizani, kabla hajasikia sauti ya aliyepigwa, amekuwa wa kwanza kujishtukia na kuwauliza alionao kwa mshangao kuwa nani ametupa jiwe!
Ni mbinu nzuri tu na sahihi ambayo Wana-CCM wengi wameichagua ili kufikisha ujumbe kwa wahusika hasa katika kipindi ambacho taifa lipo kwenye anguko kubwa la kiuchumi, uminywaji wa
demokrasia na matumizi mabaya sana ya fedha zitokanazo na kodi za walala hoi.

Mbinu hii ni very technical sana maana mara nyingi huwapoteza wasukumiwa makombora na ghafla hugeuka tena kuwa watetezi wa wasukuma makombora kama huyu Ridhiwani aliyewasukumia kombora lenye uzito wa tani mbili. Wamegeuka kumtetea badala ya kufikiria alichokieleza kwenye ujumbe wake.

Ni rahisi tu, unatupia jiwe zito, halafu unajitokeza unasikitika sana, na siku hizi hawa hackers wamepata promo ya gharama nafuu sana, wewe ni kujitokeza unasema akaunti yangu ilidukuliwa na maharamia, mchezo umeisha, huku tayari kusudio lako la kutuma ujumbe likiwa limekwisha timia.
Hapo mhusika hubakia salama salmini, kama inavyotokea kwa Ridhiwani sasa, huwezi kuvisikia tena vile vichwa vya magazeti vinavyosema "UVCCM yawacharukia wanaoikosoa Serikali mitandaoni" wala huwezi kusikia "Sheria ya makosa ya mitandao kufanyiwa marekebisho mengine Bunge lijalo".

Mpaka kuifikia hiyo 2020, tutakuwa tumeyashuhudia mengi na nimpongeze Ridhiwani kwa jinsi alivyotumia akili kutoka pangoni
walikofichwa ili wasiseme chochote kuhusu haya yanayoendelea.

Niwasihi Wana-CCM wengine waige mfano huu wa Ridhiwani na waitumie mbinu hii aliyoitumia kufikisha ujumbe wake kwa wahusika na amebakia salama.

Amen
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu...........

Ritz umetimiza hiyo kauli kwa vitendo, na ulichikisema kwenye tweet yako ndiyo ukweli wenyewe kwa asilimia 100%

Ingawa hivi sasa unaikana kauli yako "mwenyewe" kwa hofu ya kutumbuliwa!

Kwa kitendo chako hiko umepitia njia ya Ole Sendeka
 
Back
Top Bottom