Tunaruhusiwa kuongelea Saccos? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaruhusiwa kuongelea Saccos?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kotinkarwak, Oct 14, 2011.

 1. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nitauliza tena, kwani topics za Saccos haziruhusiwi kuongelewa hapa? au ni za JE tu? "Great thinkers forum provided you thinking on the lines of the mods!"

  Naona kila thread ninayoanzisha kuulizia threads za JE Saccos (hii sasa ya 3), mods wanaamua kuzitupilia mbali. Juzi nimeuliza swali kwa nini thread ya JE Saccos ambayo ilikuwa humu kwenye ukumbi wa biashara imetolewa, jibu likawa ni, wameamua kuiweka kwenye private forum. Sasa wanaotoa maoni yao kwenye hii public forum mnaonaje kama maoni yenu baadae yanakwanguliwa na kuwa threads kwenye private chats/forums.

  Mod, na hii iondoe, kwani natanguliza kwaheri zangu hapa JE Business Forum (ngoja nikachekecheke celebrities forum) kwani sioni sababu ya kufuatilia threads ambazo baadae zinanyofolewa kwani labda mtu amekerwa na jinsi communication imeendelea au kuwekwa kwenye private forums.
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  hawataki mjadara wa je saccos, mimi mwenyewe nilijaribu kuanzisha thread ikaondorewa fasta.
   
 3. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani ombi langu kuwa thread ambazo chanzo chake kilikuwa in an open forum isije kuhamishwa kwenye private forum. Nimeisoma tena sheria inayotumika JF kuhusu threads na uchangiaji, na sijaona sehemu yoyote inayotoa tahadhari kuhusu hiki kipengele. Ndio kama thread inaonekana kuchafua ishu, hiyo sawa iondolewe, lakini hizi za JE Saccos sioni kama hili limetokea, infact, kama kuna kurushiana maneno, sana sana yanatolewa na hao wanaosemekana kuwa wanachama wa JE Saccos endapo mtu atatoa maoni yake kuhusu mapungufu anayoyaona katika mswada wote wa JE Saccos.
  Hapa tupo kuelimishana na marumbano sio sehemu yake. Wenye maswali wahaki ya kuuliza especially kama anatoa maoni yake kuhusu threads zilizopo in public forum. Ningependa pia ku'note kuwa uchangiaji kwenye hii forum umezorota kidogo nikimaanisha kuwa, topics zinakosa shamrashamra (sp) nikilinganisha na mida ya nyuma kidogo, ukumbi wa Technology hata kupitia inikuwa ni nadra, sana sana unakumbana na ishu za uchakachuaji tu...
  Nitasema tena, Mods mkumbuke usemi wa JF, "Where we dare to speak/talk openly" na kama mtu atakerwa na topics zinavyochambuliwa hapa basi aende sehemu nyingine abembelezwe...
   
 4. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  majibu;
  je saccos ni taasisi ya wanaJF wote watakaokubali kujiunga kwa hiyari. kwasasa ipo katika mkakati wa kujipanga ikiwemo kujisajili na kuwa na website. imewekwa private ili kutoleta mkanganyiko, ukitaka kujadili je saccos lazima uingie je saccos private forum na uchangie ila kama unajadili saccos in general unaruhusiwa.
   
 5. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thanks Hazole,
  As a matter of principle, ningependa tu kuwafanyia haki wote wanaotoa michango yao kwenye Jamii forum kama ifuatavyo.

  Mtu anaomba kujuzwa kuhusu biashara au ishu fulani. Watu wanachangia hiyo topic wakiwa na nia ya kutoa jibu au mawazo kuhusu hiyo ishu, na pia wanajua kuwa, comments zao zitakuwepo hapa JF milele, na pengine zitamsaidia mtu mwingine ambaye atakuja na swali hilo au wazo hilo. Sasa, kukiwa na utaratibu huu wa kuzihamisha topics ambazo zilianza uhai wake in a public forum kuhamishwa private forum, au kufutiliwa mbali bila maelezo zaidi sioni kama tunawafanyia haki wanaotoa hoja/comments na jamii kwa ujumla. kama nataka kuanzisha biashara ya mihogo, nikifanya search hapa nitakuta thread nyingi tu ambazo zinachambua kwa kiasi fulani hiyo ishu. Sasa, kama topics ambazo zinachambua biashara fulani kwa undani kutokana na michango ya wana jamii ziki'binafsishwa JF itabaki na nini?

  Ninachopendekeza ni kuwa, hizo threads zirudishwe hapa in th eopen forum, na kama mods wanaonelea zifungwe basi, ziwepo tu kama kumbukumbu na new comments zisitishwe.
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  sasa kama issue za saccos na mipangilio yake unataka zianikwe hapa? kama uko interested ungeulizia jinsi ya kuingia ingekua na manufaa zaidi kwako
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mkwe haya ni mambo ya pilipili ya shamba...............................
   
 8. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  You missing the point. Mimi naongelea threads mbili au tatu zilizokuwa hapa in an open forum, mambo ya ndani ya JE Saccos inavyoandaliwa sina ishu nayo, na sio lazima mtutangazie in an open forum. Sio lazima mtu ajiunge na JE Sacco, lakini, communication zilizofanyika hapa in an open forum, kwanini zihamishwe? kumbuka unaijengea JE Sacco jina kwa kuwepo hapa in the general forum, au inamaanisha, ishu hata kama ni negative mtu azi puuzie tu, provided yeye amejiunga chama! Tusiwe watu wakukubali mambo tu na kuwa "YES SIR!" people, simaanishi kuna ishu JE Saccos lakini kwa mwendo huu wa ku'pirate topics hapa JF sidhani mnajenga jina zuri.

  Kwa hivyo, JE Sacco itakapofunguliwa rasmi, na mtoe thread hapa JF, mnataka tuikubali tu, na kama mtu atatoa ulakini fulani , mtaifunga hiyo thread? Kumbukeni, katika kujenga biashara adverts nyingi tu zinahitaji kufanyika, na tegemeo la response sivyo mnavyotarajia, watu 100 wanaweza kusema wanaipenda idea, lakini kati ya hao 10 tu ndio watakao jiunga, hence msione kama mmekosea kwani thats how business operates.

  Mimi kama private member hapa JF na pengine JE Saccos nalalamikia haki ya JF kwa ujumla. Threads zisibinafsishwe! na kama zinatolewa humu tuelezwe ni kwa misingi ipi!
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
   
 10. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani, mbona hii inakuwa ngumu kueleweka?

  Naanzisha thread yenye subject "Kufyatua matofari ya kuchoma"

  Watu wanatoa michango yao kuhusu hii idea, wengi wanatoa ideas jinsi ya kuiboresha hiyo idea, wanaofahamu mfumo huu wa ujenzi wananipa ideas za wapi na wapi udongo unafaa, pengine bei ya mauzo, manunuzi.

  Anatokea mwenye idea mbadala, anaonyesha ni jinsi gani hii haiwezekani, mfano labda miji mikubwa mabayo wanaweza kuisupport the business hawatummii au hairuhisiwi kutumia mawe ya kuchoma. Mbio mbio nina i'privatise hiyo thread yote, kwani hapo juu ideas zilizotolewa ni positive, na nisha ji'commit kuifanyia kazi (hapa tayari nishavaa blinkers, ninachoona ni mbele tu, sitaki kusikia left au right inasemaje).

  Ninachopigania hapa ni haki ya wale, waliochangia hii thread, with their feedback hukusu hii biashara (positive au negative). Miezi kadhaa baadae, atakuja member wa JF anaulizia mawe ya kuchoma, sasa, unataka naye aanze upya kuuliza au afanye search tu? lakini kama nime i'privitise ile thread, basi inabidi aanze upya... Na hapo ndipo mimi sioni kama kuondolewa hizi threads kunaisaidia JE Saccos, ndio labda siyo watu wa YES SIR!, lakini, nani anayewawakilisha hapa JF na kufanya haya madudu ya kuondoa threads? Kama members wanaona hii kitu ni sawa, basi wote ni YES Sir people, na napendekeza hii iwe discussed kwenye mkutano ujao.

  Topic: Kotin Karwak anapinga ku'pirate topics zilizokuwa main forum hata kama zinawahusu JE Saccos.


  Sina vita na JE Saccos, sina ishu kabisa, ninalilia haki za forum...

   
 11. R

  Richardbr Senior Member

  #11
  Oct 15, 2011
  Joined: May 29, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mmmmhhhhhh.......................


  Humor brings insight and tolerance. Irony brings a deeper and less friendly understanding.
   
 12. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Ipotezee Tu dada
   
 13. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Red: Usitumie mwavuli wa kusaka haki kama nia ni kujadili JE... Vile vile sidhani kama umezuiwa kuanzisha mjadala kuhusu JE (wenye kujenga au kubomoa)...!!Vilevile hujazuiliwa kuwasiliana na mods wakupe access to he subforum...!!!

  Blue: Endelea kususa... binafsi naamini uliongeza uelewa wako kwa kusoma maoni ya wale waliochangia kuhsu JE haiyumkini wamejisajili /hawakujisajili... ndio ukweli!!

  NB: Jenga hoja... Usilazimishe hoja..!!
   
 14. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haki ninayoigombania ni kuhakikisha kuwa, threads hazi binafsishwi regardless kama ni ya kujenga au kubomoa mfano umejitokeza tu kwenye thread ya JE Saccos ndio maana naitumia kama mfano, na sio kuwa kuna ishu na Saccos yenyewe. Nimetumia maneno yako mwenyewe kwani naona mtu akisema tofauti na mwondoko mzinma wa thread basi inaonekana kama ni kubomoa, hata kama ni challenge tu mtu anatoa. Kwa hiyo mtu akiona mapungufu kwenye suggestions zinazotolewa asiseme kwani, mtu au watu fulani wanakasirika!!!!

  Umenipata pia kuwa nimejuzwa mengi kutokana na kuisoma hiyo thread (amongst many threads) na natumai hii ndio idea ya Forum nzima, na hapo ndio shida ilipo. Kwani waliotoa maoni wote ni members ndio hiyo thread iwe privitised? Kama kuna comments za wengine humo ambao sio members basi hiyo thread sioni kwanini itolewe humu kwa kigezo kuwa thread inaihusu JE Sacco. Kama imefutwa na sio kuhamishwa basi Mods watueleze vigezo vilivyotumika.

  Nadhani ile hela ningeigeuza pombe tu nijue kimoja!

  Kigezo: Anzisha hoja: sijakuelewa mkuu... vipi kuchangia/kuichambua/kui'challenge/kuikosoa, au lazima uianzishe mwenyewe?
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Oouch!!! Very interesting, interesting indeed.......
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kukufahamisha mkuu ni kuwa kwenye hili Jukwaa la Biashara na Uchumi kuna Sub-Forum ambao ndani yake ndio kuna thread zote za JE Saccos, hiyo sub-forum ilitengenezwa mahususi kwa ajili ya JE Saccos sasa imekuwa haitumiki kwa muda mrefu, tumeona itakuwa busara ikianza kutumika officially ndio imeanza kutumika na thread zote za JE Saccos ziko kule
   
 17. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona Mods hawajatoa jibu kuhusu ishu ninayoiongelea, sio JE jamani... Threads zilizokuwa hapa should have been copied to the new sub forum, na hapa main forum zifungwe (no more contributions). Kuhamishwa kwa ujumla ndio chanzo cha hili swali.
  Narudia tena, hili sio swali kuhusu JE Saccos. Swali ni kwa nini threads kufutwa kutoka public forum na kuhamishwa.
   
Loading...